Mamlaka ya maji Kigoma Ujiji ina matatizo haya...

iqnq

Member
Jan 18, 2021
5
1
Kutokana na kupata adha ya kukosa maji mara kwa mara tena kwa kipindi kirefu, mimi kama mwananchi mkereketwa nikaamua kufanya uchunguzi kujua nini kiini cha tatizo katika mamlaka ya maji Kigoma Ujiji.

Katika ofisi ya Wizara ya maji ingeundwa tume maalum ya uchunguzi kuhusu madai haya:-

Mamlaka ya maji Kigoma Ujiji ina matatizo haya:-

UPANDE WA KUTOA HUDUMA KWA WATEJA

1. Wateja wamekuwa wakibambikiziwa ankara za maji bila wao kutumia maji kwa kisingizio cha flat rate.

2. Wenye meter za kusoma maji pia wanabambikiziwa ankara hata kama hawajatumia maji.

3. Wateja wakienda ofisini kulalamika wanapuuzwa na kudharauliwa.

UPANDE WA WAFANYAKAZI

1. Wengi wa waajiriwa hawana ufanisi wa kazi hivyo inapelekea kufanya kazi kiujanja ujanja.

2. Mamlaka ina ajiri watu wasio na vigezo vya kazi husika, kwa mfano Mamlaka za maji zote wameajiri waendesha mitambo ya kusukuma maji ambao wana elimu ya form IV na vyeti vya vya VETA vya grade II na III lakini mamlaka ya maji Kigoma Ujiji hao waendesha mitambo ya kusukuma maji hawajamaliza hata form IV hivyo kupelekea kutoweza kutunza vizuri mitambo ya maji na kupelekea kuharibika na kusababisha usumbufu kwa wananchi kukosa maji.

KUTOKA KWA MKAZI WA KIGOMA MANISPAA.

WAZIRI HAYA NDIO YANAYOTOKEA MAMLAKA YA MAJI KIGOMA UJIJI.
 
Back
Top Bottom