Mamla ya Maji safi na Maji taka Chamwino Ikulu yaani CHUWASA imekuwa pasua kichwa kwa wakazi wa Chamwino Ikulu. Mamlaka imekuwa ikisuasua tangu mwaka 2012. Kwa sasa ugawaji wa maji umekwisha na wakazi wa Chamwino Ikulu wamekuwa wakichangia maji na fisi, ng'ombe, punda na wanyama wengine kwa kuchota maji ya visima vilivyo wazi ambayo pia sio safi wala salama.
Hili suala limekuwa la kisiasa sana kiasi kwamba kila mara wakazi hawa wanaambiwa hilo tatizo liko katika mchakato na muda sio mrefu wataletewa maji safi na salama. Wananchi hawa wamefikia hatua ya kufunga mabomba yao ya maji kwa kuwa hakuna huduma ya maji.
Waziri wa Maji Mhe Maghembe alikuja na kutoa ahadi lukuki kuwa hilo tatizo liko mikononi mwa serikali na serikali inachukua hatua stahiki kuhakikisha kuwa wananchi wa Chamwino Ikulu wanapata maji safi na salama ndani ya muda mfupi ujao. Lakini mpaka sasa hilo suala halijapatiwa majibu na kila mtu anakwepa. Watumishi wa CHUWASA wamekuwa wakijificha ili wasionekane machoni mwa wananchi kwa kuona aibu kuwa Mamlaka imekuwa chombo mfu wanasubiri mazishi tu.
Mamlaka hii haina meneja kwa kuwa anayejiita Meneja ni Bwana George ambaye ni Afisa Mipango wa Halmashauri ya Chamwino na hana utaalamu wowote kuhusu maji na mambo yote ya kada hii. Huu si mchezo wa kuigiza? Idara yenyewe inaongozwa na vibarua tu bila hata wataalam wa kutosha wa maji. Wataalam wa Maji ni watatu tu ambao ni Masagasi, Nyawade na Matonya. Waliobaki ni vibarua wote. Je, kuna uwezekano wa Mamlaka hii kufufuka?
Mbaya zaidi hata Ikulu ndogo imekuwa kame sana kwa kukosa maji hata ya kumwagilia maua. Maana hata miundo mbinu yake imekuwa chakavu tangu ilipowekwa enzi za Mwl Nyerere. Na hata hiyo iliyopo bado haitumiki kugawa maji hata kidogo. Maji yakibahatika kutoka mara moja kwa mwezi yanatoka nyumba za barabarani ambazo ni tatu tu na Chamwino nzima inatakiwa ikachote maji kwenye nyumba hizo tatu ambazo ndio zinabahatika kupata maji kwa mwezi mara moja tu.
Kuna wataalamu wa maji wawili walipelekwa na wqizara Chamwino Ikulu ambao ni January na Chibolo. Hawa walikaa muda mfupi tu wakahamishwa na mamlaka ikabaki na vibarua wengi tena waliozoeleka.January alihamishiwa Tabora na Chibolo kahamishiwa Rufiji.
Kama Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino imeshindwa kuendesha mamlaka hii basi wawaachie DUWASA ambayo ni Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dodoma ambayo sasa inafanya vizuri sana katika kugawa maji mjini Dodoma. TATIZO LA MAJI LIMEKUWA GONJWA SUGU SASA CHAMWINO IKULU. NAWATAKIA WATENDAJI WOTE UWAJIBIKAJI MZURI ILI KAMA WAMESHINDWA KUTOA HUDUMA BASI WAJITOE.