Hivi leo mchana wakati meli ya Kilimanjaro ilipokuwa inatokea Pemba, ilipopita kwenye mkondo wa Nungwi basi wimbi moja kubwa lilipiga na maji yaliingia mpaka kwenye boti na kusomba watu kama kumi hivi.
Kutokana na upepo mkali meli haikuweza kusimama na badala yake iliwarushia life jackets, kwani ingesimama basi hatari ingekuwa kubwa zaidi.
Baadhi ya watu wamepoteza maisha.
nimepata habari hii kutoka Pemba na vile vile nilisikia mmoja wa abiria aliyenusurika akihojiwa kwenye clouds