Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI
ΤΑΝΖΑΝΙΑ (ΤΡΑ)
TAARIFA KWA UMMA
KUSOGEZWA MBELE KWA KUANZA KWA ADA YA UENDELEZAJI WA MIUNDOMBINU YA BANDARI 2026
MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI
ΤΑΝΖΑΝΙΑ (ΤΡΑ)
TAARIFA KWA UMMA
KUSOGEZWA MBELE KWA KUANZA KWA ADA YA UENDELEZAJI WA MIUNDOMBINU YA BANDARI 2026
Jumatatu Machi 09, 2026
DAR ES SALAAM
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea maombi kutoka kwa Wadau mbalimbali wa Bandari ya kupatiwa muda zaidi kabla ya kuanza kutumika kwa Ada ya Uendelezaji wa Miundombinu ya Bandari (Port Infrastructure Development PID) ambayo iko kwenye kitabu cha Ada za Bandari za Mwambao wa Bahari cha mwaka 2026. Baada ya kupokea na kuchambua kwa kina maombi hayo, TPA imeridhia kutoa muda zaidi kabla ya kuendelea kutumika kwa Ada ya PID hadi tarehe 1 Julai 2026.
Nyongeza ya muda imetolewa ili kuwawezesha wateja wote, wadau, kampuni za usafirishaji wa meli, mawakala wa forodha na usafirishaji, wasafirishaji wa mizigo, waagizaji, wauzaji nje na ndani ya nchi pamoja na umma kwa ujumla kujiandaa vema zaidi ikiwemo:
(a) kumuwezesha kila mmoja kukamilisha masharti ya mikataba aliyonayo baina yake na wateja wake wa ndani na nje ya nchi ndani ya kipindi cha muda uliobaki hadi kufikia tarehe 30 Juni 2026; na
(b) kumuwezesha kila mmoja kurekebisha masharti ya mikataba yake ya kibiashara baina yake na wateja wake wa ndani na/au nje ya nchi ambayo yataendelea kuwa hai baada ya tarehe 01 Julai 2026 ili kuendana na matakwa ya ada ya PID.
Aidha, ikumbukwe kuwa, hii ni mara ya pili TPA inasogeza mbele kuanza kwa Ada ya PID. Hapo awali, Ada ya PID ilikuwa imepangwa kuanza tarehe 08 Februari 2026. Kutokana na maombi yaliyopokelewa kipindi hicho, TPA ilisogeza muda wa kuanza kwake hadi tarehe 08 Machi 2026 kwasababu sawa na hizo zilizoanishwa kwenye ibara (a) na (b) hapo juu.
TPA inaomba yafuatayo yazingatiwe na wateja wote ambao wamepata ankara zao tarehe 08 na/au 09 Machi 2026:
(a) kwa mteja yoyote ambaye ameshafanya malipo ya Ada ya PID tarehe 08 na/au 09 Machi 2026, anaombwa kufika katika Ofisi za TPA - Kitengo cha ankara za bandari (billing office) cha bandari aliyopo kwa ajili ya kupewa utaratibu wa kurejeshewa kiasi kilicholipwa cha PID; na
(b) kwa mteja yoyote ambaye ana ankara ambazo bado hazijalipwa, anaombwa kufika katika Ofisi ya TPA - Kitengo cha ankara za bandari (billing office) cha bandari aliyopo kwa ajili ya kufanyiwa marekebisho ya ankara yake kabla ya kulipia.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)
Pia soma > Ada mpya za Bandari zimeanza kutumika tangu Machi 8, 2026. Ni mwendo wa kukamuliwa mpaka tujute!Mkurugenzi Mkuu, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA)