Mlolele Mnyilo
Member
- Nov 15, 2015
- 5
- 2
Mamlaka ni kuwa na nguvu/ jukumu la kusimamia taratibu,sheria na miongozo mbalimbali inayochangia kujenga misingi ya Maendeleo katika jamii fulani.
Jukumu hili huwa limeainishwa katika miongozo ya kiutendaji, miongozo hiyo huwekwa ili kulinda maslahi ya umma na Taifa kwa ujumla.
Kwa kawaida mamlaka hujengwa kwa mihimiri mbalimbali kutegemea nguvu ya aina ya mamlaka yenyewe katika kusukuma gurudumu la Maendeleo.
Mamlaka ni mali ya nani?
Mamlaka ni mali ya Taifa ambayo ni Wananchi, hivyo ni vibaya sana kwa mtu yeyote kujiona yeye ni mwenye nguvu kwasababu ya nafasi ya kimamlaka inayoainishwa kisheria kwa lengo la kulinda maslahi ya umma.
Mamlaka si kuwa na nguvu juu ya Watu unaowaongoza, bali kuwa na nguvu ya kisheria katika utekelezaji wa majukumu yenye tija kwa Taifa, hivyo basi Viongozi wanapaswa kufahamu kwamba nguvu waliyopewa na umma ni nidhamu na wajibu katika kutekeza malengo ya Kitaifa, na si Vinginevyo.
Kumekuwa na mazoea ya Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa kuwaweka ndani Wananchi kwa kigezo cha Mamlaka, ni dhahiri kwamba Wakuu wa Mikoa na Wilaya labda kwasababu ya kuteuliwa hawaoni wajibu wao, wajibu wao kwanza uanzie kwenye katiba ya jamhuri ya muungano ya Tanzania, katiba inaruhusu mtu kujieleza, lakini pia wakuu hawa wanaonesha kwa kuteuliwa kwao hawana Maarifa kwani wanatumia nguvu nyingi kusuruhisha mambo madogo.
Pamoja na kuwa Wakuu hawa wamepewa Mamlaka ya Ulinzi na Usalama katika Wilaya na Mkoa, lakini bado wanawajibika kuchukua maamuzi yenye tija na si USHABIKI au kujipendekeza ili kulinda vibarua vyao.
"Nidhamu ni heshima katika kusimamia na kuwajibika katika eneo linalokuhusu, uwajibikaji mzuri ni ule unaolenga kutatua Changamoto na si kumridhisha mtu fulani."
"TUSEME UKWELI TULINDE HESHIMA YETU "
HAKUNA ALIYE JUU YA SHERIA, DUNIANI HATA KWA MUNGU