Mamlaka husika fanyeni kazi kuboresha elimu yetu, wanahabari andikeni taarifa za kuboresha elimu

Eudorite

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
1,126
753
Wadao natumai mu wazima na pole kwa waliopatwa na maswaibu mbalimbali ikiwa ni pamoja na wasafiri waliolala njiani kutokana na athari za mvua barabarani.

Nimefuatilia malumbano ya hoja yanayoendelea ITV na RADIO ONE. Nami ninao ushuhuda ufuatao.

Niseme kwamba nina mwanangu yupo kidato cha kwanza katika shule ya kata iitwayo MUGABE iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Nimemdadisi na kugundua shule ina changamoto zifuatazo.

1. IDADI KUBWA YA WANAFUNZI DARASANI.
Hii ndiyo changamoto kubwa inayosababisha mengine mengi mabaya katika shule hii. Darasa lina wanafunzi zaidi ya 100. Sijui sera ya elimu inasemaje katika hili. Ikumbukwe shule hii ipo jijini Dar na eneo lenye vitegauchumi vya kutosha hivyo ukosefu wa vyumba vya madarasa ni uzembe wa mamlaka husika.

2. UTOVU WA NIDHAMU KWA WANAFUNZI.
Nidhamu siyo tena jukumu la mwalimu mkuu na timu yake. Hili nilimuuliza mkuu wa shule alasema yeye hahusiki nalo. Kwa ufupi watoto hasa wa kiume wanatumia MIHADARATI na ni wezi. Na wale wa kike ki WAHUNI au MALAYA. Kwa hili la nidhamu matokeo yale ni kutofaulu vizuri kwa wanafunzi.

3.MAZINGIRA MABAYA/HATARISHO YA KUJIFUNZIA
ukiachana na upungufu wa vyumba vya madarasa. Kuna upungufu wa viti kwa wanafunzi. Vyooni hakuna maji na ni vichafu. Walimu kutofundisha ipasavyo. Ukosefu wa walimu hasa wa fani za Sayansi. nk.

Rai yangu ni kwamba mamlaka husika zifanye kazi zake ili kuboresha hii elimu. Na pia waandishi wa habari watusaidie kuandika habari za uchunguzi kuhusu namna elimu yetu inavyotolewa ili kuoa hiki kizazi.
 
Mtoto akikosa elimu imara sekondari fahamu atataabika sana kielimu huko mbele.

Lakini shule sio tu kusoma mambo ya darasani pia kupata ujuzi wa kuishi kwa kufuata taratibu


Sasa kama mazingira ya shule ni hayo uliyosema, idadi yao, walimu kutoshiriki kujenga tabia njema........hapo mtoto atakuwa duni tu.

Dunia imekuwa ya kushindana sana

Kuanzia 2015 hadi 2035 vijana zaidi ya 15 milioni watakuwa mtaani wanatafuta ajira.

Umemwandaaje mwanao kupambana?

Hiyo ni juu yako.....the government won't come to save your child. Truth many don't like to hear
 
Zipo shule za private ada milioni na zina matatizo kama hayo uliyo yataja kuwa makini na hizi shule za kisasa
 
Back
Top Bottom