GIPAMA
JF-Expert Member
- May 21, 2016
- 1,103
- 541
Ndugu wanabodi, heshima kwenu wakuu,
Nadhani wote tunaamini elimu bora ndio msingi wa maendeleo, ila sasa elimu hii inaharibiwa na mamlaka husika zipo kimya zimetulia, sijui kama sababu ni rushwa ama kitu gani........
Mfano hapa Bunda mji, kuna shule za English medium ambazo hazijasajiliwa, na mazingira yake ya utoaji wa elimu siyo mazuri kwa kuanza na miundo mbinu na walimu wenye sifa.....
Watoto hao wamekuwa wakihangaishwa kila kwaka kupelekwa shule za jirani za serikali ili wakafanye mtihani..... Na kwa sababu ya rushwa walimu wakuu wa shule jirani wamekuwa wakiwapokea na kuwasajili hao watoto wakati hawajasoma pale, huku ni kuidanganya mamlaka.
Kwamaana hiyo mamlaka zinazojihusisha na ukaguzi wa shule Halmashauri ya Bunda mji, zichunguzwe huenda zinapokea rushwa ili kuendeleza huu uozo unaowanyima watoto kupata elimu bora kama msingi wa maendeleo.
Kama mamlaka za ukaguzi hazichukui rushwa na kuruhusu uozo huu, basi mamlaka hizi zichukue hatua dhidi ya shule hizi, zifungiwe, taaratibu zifuatwe zisajiliwe, na walimu wenye sifa wawepo, miundo mbinu iboreshwe ili elimu bora iweze kutolewa.
Asanteni.