Mamilioni ya Magufuli vijijini yavuna kibabe wanachama wanawake wa vyama vya upinzani

MC Chere

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
586
400
Bado siamini kama hili jambo linaweza kutendeka lakini ndivyo ilivyo.

Ikumbukwe kuwa,wakati wa kampeni aliahidi kutoa mil50 kwa kila kijiji,niliposikia ahadi hiyo inataraji kutekelezwa hivi karibuni nikapongeza sana ahadi hiyo kutimizwa.

Aidha,wanatakiwa wanawake waunde vikundi kisha waandike katiba na taratibu nyinginezo ili kukidhi vigezo vya kukopeshwa,hilo mimi halikunishangaza.

Niliduwaa pale nilipoambiwa kuwa,ili upewe mkopo ni lazima uwe mwanachama wa CCM na hivyo tayarh utakuwa mwanachama wa UWT ili upewe kadi maalumu,hivyo kwa mwanachama wa chama kingine itabidi airudishe kadi giyo kwenye hicho chama na ajiunge na CCM kinyume na hapo hakuna mkopo.
Watu wakahoji,hizo pesa ni za Serikali/CCM? Majibu yaliyotolewa ni juwa Magufuki ni wa chama gani?

Labda RAIS wangu wamajipu niambie hizo pesa ni za chama na si za serikali hapo mtakuwa sawa,lakini ikiwa ni za Serikali je hayo masharti umeagiza mwenyewe?

LOCATION.Kilolo-Iringa
 
ccm tunakula pa kulala tunajua wenyewe, kwani hela za ccm au za serikali? Kodi tunalipa wote kwa hiyo ni jasho la wote lazima zichukuliwe tu mradi zimeletwa.
 
Ingekuwa habari imetoka USA ingekuwa ni stori za kufikirika,ila ukumbuke kuwa hii ndiyo TANZANIA,nipo eneo la source ya habari na mimi ndiyo shuhuda.
 
Usiwe na wasiwasi. Watafanya kama vile ilivyofanyika wakati wa Uchaguzi. Kwenye mikutano wanakuwa nyomi/mafuriko lakini matokeo ya kura analizwa mtu!
 
Bado siamini kama hili jambo linaweza kutendeka lakini ndivyo ilivyo.

Ikumbukwe kuwa,wakati wa kampeni aliahidi kutoa mil50 kwa kila kijiji,niliposikia ahadi hiyo inataraji kutekelezwa hivi karibuni nikapongeza sana ahadi hiyo kutimizwa.

Aidha,wanatakiwa wanawake waunde vikundi kisha waandike katiba na taratibu nyinginezo ili kukidhi vigezo vya kukopeshwa,hilo mimi halikunishangaza.

Niliduwaa pale nilipoambiwa kuwa,ili upewe mkopo ni lazima uwe mwanachama wa CCM na hivyo tayarh utakuwa mwanachama wa UWT ili upewe kadi maalumu,hivyo kwa mwanachama wa chama kingine itabidi airudishe kadi giyo kwenye hicho chama na ajiunge na CCM kinyume na hapo hakuna mkopo.
Watu wakahoji,hizo pesa ni za Serikali/CCM? Majibu yaliyotolewa ni juwa Magufuki ni wa chama gani?

Labda RAIS wangu wamajipu niambie hizo pesa ni za chama na si za serikali hapo mtakuwa sawa,lakini ikiwa ni za Serikali je hayo masharti umeagiza mwenyewe?

LOCATION.Kilolo-Iringa
Mkuu umekunywa kiroba gani leo? Nani kakudanganya kuwa zile pesa zimeanza kutolewa?
 
Ingekuwa habari imetoka USA ingekuwa ni stori za kufikirika,ila ukumbuke kuwa hii ndiyo TANZANIA,nipo eneo la source ya habari na mimi ndiyo shuhuda.
Nilipita Lupembe hivi karibuni habari ni hiyo hiyo.... Niliwaambia chukueni kwani chama kipo moyoni mwako si kwenye kadi.
 
Back
Top Bottom