jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,140
- 29,670
Jicho letu katika uhai wa chama ni kuhusu sera na misimamo ambayo imeandaliwa kisomi na baada ya uchunguzi wa kina.
Sera na misimamo ndio jambo linalotoa identity ya chama fulani na hatimaye kujijengea ufuasi na pengine baadaye kudefine identity na msimamo wa kitaifa.
Mara nyingi Vyama hutakiwa kuwa na misimamo yenye uimara na yenye kudumu au kuishi kwa muda mrefu.
Tuchukulie mfano wa Imani ya kikatoliki au kirastafari au kiislamu despite kupitia misukosuko mingi.
Imani hizi pamoja na kupokea waumini wapya pengine waliokuwa na imani tofauti kamwe hazijawahi kubadilisha misimamo yao kuntu.
Hivyo basi kama mtanzania nimeendelea kuobserve sera na misimamo ya vyama mbalimbali vya kisiasa na kujikuta nikishangazwa sana na CDM.
Yaani CDM inakengeuka kwenye imani zake zote kwa kasi ya hatari...na katika hili la msimamo au sera basi Chadema inaweza kuwa ya mwisho ukiilinganisha na TLP,NCCR au CUF achilia mbali kubwalao la Taifa The one and only legend in Africa..CCM.
Nisiwachoshe bali niende direct kwenye kuorodhesha baadhi ya mambo makubwa yaliyobadilishiwa gia za anga na Chadema.
1-Mabadiliko ya bendera ya Chama yaliyofanywa na viongozi wachache wa Chadema.Tulishawahi kujadili humuhumu jamvini.
2-Chadema kugeuka kuwa chama cha wafanyabiashara wakubwa na kuwatekeleza wanachama wadogo wanyonge.Mwanachama asiye ma mshiko hana sauti kwenye chama.
3-Msimamo wao dhidi ya utorooshwaji wa rasilimali za umma mfano madini.Msimamo wao wa awali ni kukataa uwekezaji wa kilaghai unaofanywa na wawekezaji kutoka nje na hivyo kuhitaji usitishwaji wa mikataba at all cost bila kujali mahusiano yetu na walami.
4-Ufisadi.Chadema ilipanda chati kwa kuibuwa ufisadi na ubadhirifu hadi kuthubutu kuwataja na kuweka THE LIST OF SHAME kwenye website ya Chama.ingawa baadae na especially 2015 kuamua kuwajaribu watanzania kwa kuwawekea waliyemtuhumu kwa ufisadi kuwa mgombea wao.
5-Uzembe wa watumishi serikalini na uchukuaji hatua ndani ya muda.Chadema ilipinga sana watumishi wazembe serikalini kuachwa ilihali wamefanya makosa.Ni chadema iliyokuwa ikipinga Hamisha hamisha ya watumishi waliokosea badala yake walitaka utumbuaji wa fasta fasta bila kuunda tume n.k.
6-Kuhusu ukwepaji kodi..chadema iliwasema sana wafanyabiashara ambao wengi walijiunga CCM na kukwepa kodi.Magufuli alipoanza kamatakamata ya Makontena chadema ikageuka mtetezi wa wafanyabiashara waliokwepa kodi.
7-Misaada kutoka nje.Wakati MCC wanatupiga ban ya misaada chadema ikaanza kusema nchi itaendeshwa vipi bila misaada na kuitaka serikali kuyakubali matakwa ya wahisani ili tuendelee kupewa msaada na kuepuka hali ngumu.hapo mwanzoni chadema iliitaka serikali kuondokana na utegemezi wa misaada.
8-Kuhusu posho zilizokithiri kwa wafanyakazi wa umma na wanasiasa.Hapa chadema ilituaminisha kuwa bajeti kubwa huenda kwenye posho badala ya miradi ta maendeleo.Magufuli alipoanza kupiga ban miposho isiyo ba tija Chadema tukichukulia mfano wa jiji la Arusha walimuona mkurugenzi ni mbaya kwa kupunguza posho zao.
9-Kuhusu unyanyasaji wa wamachinga na mama ntilie.Chadema iliwasemea sana kuwa hawa wamachinga waachwe wafanye biashara zao kwa uhuru...alipoingia Magufuli na kusema wamachinga wasiguswe chadema ikasema hawa jamaa wanachafua miji.
10-Kuhusu miundo mbinu ya ysafiri.
Chadema ilishutumu sana kukosekana kwa miundombinu ya reli na usafiri wa Anga.Magufuli amefanya uboreshaji na miradi mikubwa katika eneo hili sasa chadema inasema sio priority.
Haya ni mambo machache ninayoweza kuyaoridhesha kwa sasa lakini mengine yapo.
Ukichunguza utagundua kuwa Chadema ni chama kilichokosa msimamo wa kisera ...leo hii wanaweza kujwambia Magufuli anatekeleza sera zetu kesho wanakwambia ni dikteta au atatutia hasara kwa kutekeleza yaleyale kwa njia zile zile walizokuwa wanazitaka.
Juzijuzi walisema Nape na Kinana ni wabaya leo hii Nape na Kinana ni majembe.
Nawasilisha
..KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!!