Mambo yanavunja mahusiano.

Sungura dume

JF-Expert Member
Mar 28, 2016
440
500
MAMBO YANAYOVUNJA MAHUSIANO
1. Kutokuwa na mawasiliano ya
karibu na mwenzi wako.
2. Kutojali maumivu ya mwenzi wako.
3. Ubishi usiokuwa na maana.
4. Kupenda kujihesabia haki.
5. Kutokubali makosa.
6. Kutokuwa na roho ya msamaha.
7. Kutokuwa muwazi kwa mwenzi
wako.
8. Usaliti wa mapenzi.
9. Kuigiza kupenda.
10. Kutomheshimu mwenzi wako.
11. Kuwa mjuaji kila kitu unajifanya
unajua.
12. Kutokutambua uthamani wa
mwenzi wako katika maisha yako.
13. Kuwa na jeuri.
14. Kutokuwa na kifua cha kuficha
mambo ya nyumbani. [chumbani]
15. Kuto kujali watu wa nyumbani
kwako [ndugu,watoto n.k]
16. Kujiamulia kufanya vitu bila
ushauri wa pamoja.
17. Kutokuwa na faraja na mwenzi
wako [kutokujua jinsi ya kumfariji
mwenzi wako]
18. Kutomridhisha mwenzi wako
kimapenzi.
19. Kuwa na amri kwa mwenzi wako
hata kwa mambo yasiyokuwa na
maana au malengo katika maisha
yenu.
20. Ugomvi wa muda mrefu usiokuwa
na suluhu.
21. Kuwa na ahadi za uongo.
22. Kumdhalilisha mwenzi wako
mbele za watu.
23. Kupenda starehe kuliko kuujenga
uhusiano wa kudumu [love]
24. Uchafu kutojipenda na kupenda
mazingira yako.
25. Maudhi ya mara kwa mara.
26. Kutoonyesha hisia kali
za mapenzi kwa mwenzi wako.
27. Kutokuwa karibu na mpenzi wako
mara anapokuwa katika msongo wa
mawazo.
28. Kutokuwa mbunifu wa maisha mapenzi.
29. Kutokuwa na msimamo katika
maamuzi yako [kutoendeshwa na
watu]
30. Kutokuwa na muda na mwenzi
wako.
31. Kutokuwa na shukrani.
32. Kutokujua gharama za upendo.
33. Kuwa na wivu wa kijinga.
34. Kuwa mbinafsi.
35. Kujifanya kuwa [busy] na
kushindwa kumtunza na kumjali
mwenzi wako
36. Kutokuwa na imani juu ya mwenzi
wako.
37. Kutokubaliana na hali halisi ya
maisha yenu.
38. Kutokukubali kujifunza.
39. Kutokutambua maana ya mapenzi
na umuhimu wake.
Tabia hizo ndizo zinasababisha
mahusiano ya watu wengi kuvunjika,
hata ndoa kuharibika maana huyu
mtu unayemfanyia hivi ipo siku
atachoka, maana hana moyo wa jiwe
bali ana moyo wa nyama. Kuvumilia
nako kunamwisho wake, hizo tabia
ndizo zimechangia maumivu, vidonda
vya mapenzi, vifo vya watu wengi na
kuwafanya watu wengine kuchukia
kupenda na kupendwa katika maisha
yao.
Muwe na siku njema wapendwa.
 

Man Thom

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
717
1,000
Linapokuja suala la mahusiano ya kimapenzi yanayokaribia ndoa au kuishi pamoja, hakuna anayekubali kushindwa hata iweje, ni jukumu la kila mmoja kuwa na hali fulani ya kujishusha na kuvumilia mapungufu ya mwenzako ili mvuke salama, lakini tofauti na hapo..na huu utandawazi..uchumba utaendelea kuvunjika tu! You might think it would be great if you could have a relationship with zero arguing japo ni nadra sana kutokea..watch out
 

PjMarLu

JF-Expert Member
Sep 15, 2014
1,404
2,000
sredi ndefu sana inachosha, points nyingi zinafall under one group. ukichambua unapata sababu 3 tu hapo.
 

Blaki Womani

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
11,225
2,000
Hakuna binadamu mkamilifu atakuwa mahiri kwa 10 atakuwa na pungufu kwa 1 ambalo litakuwa kero kubwa kwa mwenzi wake.


Mengine kuachana nayo maisha yanasonga
 

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
3,659
2,000
mkuu huyu ni malaika otherwise haishi duniani.

kuna kutereza aseee nimekasirika ntaacha kurusha jembe ?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom