Bufa
JF-Expert Member
- Mar 31, 2012
- 14,391
- 30,924
1- Nikawaida kabisa kukutana na mmachinga bonge la mtu kama goliati alafu anauza kata kucha na sio nyingi kama tano tu,nikajiuliza huu mwili unalelewa na biashara hii ndogo hivi au kuna lingine?
2- Mgahawani nimeagiza supu nikashindwa kuelewa hii ni supu ya ng'ombe kweli au mchemsho maana imewekwa hadi vitunguu
3- Nikajipa moyo ngoja mchana mlo utakuwa mzuri,haya wali nyama duuuuu hivi nikweli mchele unalimwa mbeya? Au nimeagiza kande? Nikagundua mapishi zero
4-Any way jioni nitakula nyama choma nimwagilie moyo nikalale (mhudumu naomba nyama choma na ndizi mbili hapo) lo mchoma nyama sasa anapaka nyama mafuta kwa kutumia brush lakupigia rangi ukuta then inapokaribia kuiva anaikatakata vipande vidogo anaviweka juu ya wire anavichoma tena[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
5-Plus hili vumbi upepo na baridi lake hapana ngoja nirudi zangu Chugamaica nikamwagilie moyo kwa mworomboo
Hapo No. 1, Mbeya watu ni wapambanaji si wanaume si wanawake. Arusha vijana kazi kutumia mihadarati na kusuka Rasta ili waolewe na mizungu.