Mambo ya Simba na Yanga yametoweka kabisa

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
11,187
Reaction score
24,579
Watanzania wamebadilisha upepo sahivi sisikii tena ule ujinga wa Simba na Yanga upo lakini mchache sana.
Alikua ananunuaga magoli ili tuendelee kuwa busy ili aendelee kutuibia wananchi wameshtukia.

Sahivi sioni zile mbwembwe za kupost hayo makitu, sahivi hata trending za mastaa hatuzioni tena

Yaani mpaka najiuliza au wasanii wetu after October 29 hawatumiii tena Simu au wamezificha wapi maana hawavumi tena.

This is Clear message to you Samia Suluhu your time is Coming you will pay a heavy price. Ulionywa hukusikia, hadi rais anafungia comments aisee hali ni ngumu ndugu zangu!!.

Media nyingi zinaenda kufa Tanzania kwa kupoteza mvuto na hamasa na watazamaji.Wanavuna walichopanda.
 
Manina wahenga hawaamini , mtaka cha uvunguni amesogeza kitanda ! Tunachumia kivulini na tunalia kivulini 😂😂 wahenga wamejificha !
Hatusikii la mkuu na guu hatuvunjiki.
CCM walijisahau sana tuseme ukweli hii sio hulka yetu wabongo wametuprovoke vya kutosha na walivyoona hatushtuki wakawa wanakuja na sentensi za hovyo kwenye majukwaa !!
Sasa mchambaji sasa hivi ana sauti kama Jaiver 😂 na issue ya udini imekataa leo nimeenda kanisani na kanzu
 
Nilitaka kufungua uzi kama huu mkuu, umeniwai, zile kelele za simba na yanga zimepungua kwa asilimia kubwa sana. Pita masokoni, vijiweni, makazini kote mijadala ya hizi timu imepungua mno. Tukiendelea hivi, hili Taifa litabadikika pakubwa.
 
Mimi nilikua shabiki wa Simba lialia ila nilijiona mpumbavu baada ya mauaji ya raia ya October 29 sio Ahmed Ali wala official page ya Simba waliopost walau ku recognize vifo vya wanasimba walipoteza maisha badala yake waliendelea kupost issues nyingine kabisa kama vile hakuna kilichotokea.

Nime unfollow takataka zote. Kama ni mpira acha nishabikie clubs za Ulaya walau hizo zinathamini utu.
 
Na hayatarudi.tena. tupo.busy na nchi
 
Kwa kutumia hayo matibu ya hovyo watanzania walipewa upofu sana.
 
Hizi timu zilichangia pakubwa ndugu zetu kuuwawa. Mfano mzuri ni hawa
 
we ushawahi kuona page zinapost kifo cha mhalifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…