Mambo ya Rais Shein,CCM ni ile ile

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Nasema mara kwa mara kuwa CCM ni chama chenye watu wa kutumia kauli za uongo,ulaghai na utapeli. Ni watu wa kusema tofauti na matendo,kutenda tofauti na maneno. Watu wa kubadilikabadilika. Kauli mbilimbili lakini si za mbalimbali.

Alipokuwa akihutubia na kuzindua Baraza la Wawakilishi,Rais wa Zanzibar-Dr. Shein,alisema kuwa ataunda Serikali ya chama kimoja. Serikali ya CCM pekee. Sababu aliyoisema ni kuwa wazanzibari,kwenye boksi la kura,wamevikataa vyama vya upinzani. Akashangiliwa,akaaminiwa.

Rais Shein amemteuwa Ndugu Hamad Rashid kuwa Waziri wa Kilimo na Mazingira. Hamad Rashid ni wa chama cha ADC. Ameingia Serikalini. Hivyo,Serikali aliyoiunda Rais Shein si ya chama kimoja. Si ya CCM tu. Rais ameongea hivi,akatenda vile! Ni walewale. CCM ni ile ile ya siasa za kilaghai na kitapeli!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Mkuu hivi unategemea kauli yoyote ya ukweli itatoka kwa viongozi wa zanzibar?, tuseme ukweli ndugu yangu pamoja na kwamba wewe ni mzee wa lumumba
 
Haahaaaaaaa, kwani kaweka wapinzani hapo? Hao wengine kina Hamad ni ccm ndani ya vyama vyao.. anajua sana upinzani wa kweli ni cuf. wala hajakosea kwaingizi hao wengine.
 
Nasema mara kwa mara kuwa CCM ni chama chenye watu wa kutumia kauli za uongo,ulaghai na utapeli. Ni watu wa kusema tofauti na matendo,kutenda tofauti na maneno. Watu wa kubadilikabadilika. Kauli mbilimbili lakini si za mbalimbali.

Alipokuwa akihutubia na kuzindua Baraza la Wawakilishi,Rais wa Zanzibar-Dr. Shein,alisema kuwa ataunda Serikali ya chama kimoja. Serikali ya CCM pekee. Sababu aliyoisema ni kuwa wazanzibari,kwenye boksi la kura,wamevikataa vyama vya upinzani. Akashangiliwa,akaaminiwa.

Rais Shein amemteuwa Ndugu Hamad Rashid kuwa Waziri wa Kilimo na Mazingira. Hamad Rashid ni wa chama cha ADC. Ameingia Serikalini. Hivyo,Serikali aliyoiunda Rais Shein si ya chama kimoja. Si ya CCM tu. Rais ameongea hivi,akatenda vile! Ni walewale. CCM ni ile ile ya siasa za kilaghai na kitapeli!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
Halafu huyu Hamad si amefukuzwa chama? Msajili wa vyama kimyaa!

Hamad Rashid ana chama! anaingiaje katika SUK?
 
Sijui maamuzi ya Shein na serikalj ya Jecha ni yake mwenyewe au kuna remote controller Lumumba,Msoga au Lushoto?
 
Back
Top Bottom