Mambo ya Pwani: Bi dada kaahidi kunitoa out kwa Sheikh Mpalange

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,347
11,447
Bi khadija dada wa mjini tupo naye kazini mwaka wa pili sasa, ni mchangamfu mpaka mwisho amepitiliza kama katiwa ndimu.

Nimekuwa mara kadhaa naepuka ukaribu naye maana mimi mtu akichangamka sana naona ana nibore but bi dada huyu wa kitanga ana mwito, macho yake rangi na mitako.

Aargh. Potelea pote na mpunga usiote. Nimeshamtoa lunch mara mbili kwa kumpa pesa tu, sikwenda naye maana ukitembea naye kero, wanaume wanamkodolea macho.

Kuna siku kwenye maongezi hasa suala la mahusiano nilimwambia nimetulia sana na wife, huwa anapenda nitania najifanya mgumu nimeoa.

Ndo kusema atanipeleka kwa Sheikh Mpalange, leo tena akanikumbusha kuwa weekend hii anataka anipeleke kwa Sheikh Mpalange. Nilimuuliza kuna pikwa nini huko akacheka sana mpaka machozi kumtoka.

Miaka zaidi ya 40 DSM hii sijawahi enda kwa Sheikh Mpalange pamekuwa maarufu kuzidi Samakisamaki au KFC. Sijaelewa huko kunakuaje, nikasema pengine wadau mmeshaenda huko nifahamu kidogo nisiwe mgeni sana.

Ni wapi na kunani huko?
 
Back
Top Bottom