Mambo ya msingi ya kufanya Gari lako linapopasuka tairi

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,824
23,125
UFANYE NINI TAIRI LIKIBASTI?

Kuna hatua sita za kufuata ndani ya dakika mbili tangu kupasuka tairi ambazo unapaswa kuzifuata.

1. USIHAMAKI, tulia kwanza kwa sababu mara baada ya kupasuka tairi gari lako litaanza kwenda kombo na hivyo utahitajika kulimudu.

2. KAMATA USUKANI Kwa nguvu kwa mikono yote miwili, USIPINDEPINDE KONA huku ukiwa makini na barabara na vioo vya gari lako. Wakati huo soma mwenendo wa gari lako, ambapo mara nyingi litakuwa linakuvuta upande uliopasuka tairi.

3. ONDOA mguu wako kwenye eksileleta. USIJARIBU KABISA KUKANYAGA BREKI,Ukijaribu kufanya hivyo utabinuka na gari. Ilhali kama usipokanyaga breki gari litapunguza mwendo lenyewe taratibu, wakati wewe ukiwa makini kuangalia watumiaji wengine wa barabara.

4. ONDOA gia zote na uziweke kwenye nyutro huku bado ukiwa umeshikilia vema usukani wako na macho mbele kwenye barabara.

5. Baada ya muda mfupi, kulingana na mwendo wako, gari ikiwa imefika spidi chini ya 60kph, sasa kanyaga breki zako taratibu huku ukisogea kandoni mwa barabara ili usimame.

6. Hatimaye, itakuwa salama zaidi kusimamisha gari lako na kuzima injini.

Hapo utakuwa umeokoa maisha yako na ya abiria wako kutoka kifo.

NYONGEZA: Inapotokea tairi imepasuka ni mara 10 salama kuongeza mwendo kuliko kuhamisha mguu na kukanyaga breki.

Tafadhali, washirikishe na wenzio kwa kusambaza ujumbe huu. Jambo hili linaweza kumpata mtu yeyote, wakati wowote barabarani. Imetafsiriwa kwa hisani ya RSA TANZANIA.
 
kipengele namba 4 ,utawezaje kubadili gia wakati umesema mtu ashike USUKANI kwa mikono miwili na kwa nguvu?
 
Ndio maana madereva wanashauriwa kupiga push up na kutengeneza stamina za mikono ni katika jali kama hii ndo utatumia stamina ya mikono iliyokaza kwa push up kuhandle gari lako kwenye kimbembe kama hichi barabarani.
 
Mkuu asante kwa uzi huu lakini kwakuwa umeingia katika mambo niyajuayo ngoja nikukosoe baadhi ya mambo!
1.Kwanza dakika 2 ni nyingi ungesema ndani ya sekunde 30-40.
2.Kuondoa gear ni kuliongezea kasi gari
3.Kukanyaga break kuna style yakukanyaga hasa kwa wazoefu wa magari una apply Break kwa mbali na kulingana na speed ya gari iliyopo.Maana ikipata basti kwenye mteremko na mbele kuna kona unawashauri watu wasikanyage break??
4.Ujaeleza ni tyre za wapi mbele au nyuma au?maana kila upande wagari unajinsi yake yakujiokoa
5Ujaeleza ni magari ya ukubwa gani ila nimeona wewe umelenga sedans
Mwisho asante kwa hicho kidogo ulichokitoa na wengine watakuja kuongezea kuliko baki.
 
Ndani ya dakika mbili? Uko 140kph una dakika mbili hapo? Sema ndani ya sekunde kadhaa, na hii kitu sio ya kukariri inahitaji uzoefu, kuna watu hata hawajui tairi imepasuka yeye anaona tu gari inayumba.

Ni sawa na mtu yuko 140kph anakatiza mbwa unamkwepa matokeo yake unapiga sarakasi,ila mzoefu unanyoosha tu unasimama mbele kuangalia nini kimevunjika.
 
Mkuu unaendesha Mbaula??!!! Power steering haihitaji msuli kaka,ni control tu.
 
Mkuu kama haya ni mambo uyajuayo, weka majibu sasa, hasa burst za mbele, kushoto au kulia.
Mkuu asante kwa uzi huu lakini kwakuwa umeingia katika mambo niyajuayo ngoja nikukosoe baadhi ya mambo!
1.Kwanza dakika 2 ni nyingi ungesema ndani ya sekunde 30-40.
2.Kuondoa gear ni kuliongezea kasi gari
3.Kukanyaga break kuna style yakukanyaga hasa kwa wazoefu wa magari una apply Break kwa mbali na kulingana na speed ya gari iliyopo.Maana ikipata basti kwenye mteremko na mbele kuna kona unawashauri watu wasikanyage break??
4.Ujaeleza ni tyre za wapi mbele au nyuma au?maana kila upande wagari unajinsi yake yakujiokoa
5Ujaeleza ni magari ya ukubwa gani ila nimeona wewe umelenga sedans
Mwisho asante kwa hicho kidogo ulichokitoa na wengine watakuja kuongezea kuliko baki.
 
Nina uelewa wa hayo mambo kiasi, nitakukosoa hicho kipengele cha 4. Umekikosea kwa uelewa wangu. Ukweli ni kwamba utakapoondoa gear zote na Kuwa N ujue gari utakua umeiongezea kasi, jambo ambalo litakua gumu sana kuimiliki gari iwe kwenye hali yake, elewa gear inapobaki kwenye position yake itaisaidia gari kupungua kasi kulingana na matakwa ya gear.
 
Uko sahihi mkuu
 
UFANYE NINI TAIRI LIKIBASTI?

Kuna hatua sita za kufuata ndani ya dakika mbili tangu kupasuka tairi ambazo unapaswa kuzifuata.

1. USIHAMAKI, tulia kwanza kwa sababu mara baada ya kupasuka tairi gari lako litaanza kwenda kombo na hivyo utahitajika kulimudu.

2. KAMATA USUKANI Kwa nguvu kwa mikono yote miwili, USIPINDEPINDE KONA huku ukiwa makini na barabara na vioo vya gari lako. Wakati huo soma mwenendo wa gari lako, ambapo mara nyingi litakuwa linakuvuta upande uliopasuka tairi.

3. ONDOA mguu wako kwenye eksileleta. USIJARIBU KABISA KUKANYAGA BREKI,Ukijaribu kufanya hivyo utabinuka na gari. Ilhali kama usipokanyaga breki gari litapunguza mwendo lenyewe taratibu, wakati wewe ukiwa makini kuangalia watumiaji wengine wa barabara.

4. ONDOA gia zote na uziweke kwenye nyutro huku bado ukiwa umeshikilia vema usukani wako na macho mbele kwenye barabara.

5. Baada ya muda mfupi, kulingana na mwendo wako, gari ikiwa imefika spidi chini ya 60kph, sasa kanyaga breki zako taratibu huku ukisogea kandoni mwa barabara ili usimame.

6. Hatimaye, itakuwa salama zaidi kusimamisha gari lako na kuzima injini.

Hapo utakuwa umeokoa maisha yako na ya abiria wako kutoka kifo.

NYONGEZA: Inapotokea tairi imepasuka ni mara 10 salama kuongeza mwendo kuliko kuhamisha mguu na kukanyaga breki.

Tafadhali, washirikishe na wenzio kwa kusambaza ujumbe huu.

Jambo hili linaweza kumpata mtu yeyote, wakati wowote barabarani.

Imetafsiriwa kwa hisani ya RSA TANZANIA.

Kipengele namba 4 umekosea gari inapokuwa free inaongeza speed kwa hiyo itakwenda umbali mrefu hivyo kusababisha lianguke baada ya wewe kuzidiwa na kuchoka kuizuia kwenye usukani siku zote gari ili isimame haraka haitakiwi iwe free unaiweka free ikiwa hatua za mwisho kusimama ili isizimike tofauti na hivyo naomba nakaribisha maoni kutoka kwa madereva mbalimbali
 
Ndani ya dakika mbili? Uko 140kph una dakika mbili hapo? Sema ndani ya sekunde kadhaa, na hii kitu sio ya kukariri inahitaji uzoefu, kuna watu hata hawajui tairi imepasuka yeye anaona tu gari inayumba.

Ni sawa na mtu yuko 140kph anakatiza mbwa unamkwepa matokeo yake unapiga sarakasi,ila mzoefu unanyoosha tu unasimama mbele kuangalia nini kimevunjika.

Hapo bila Shaka mbwa atakuwa ndio kitu kilichovunjika
 
Back
Top Bottom