Mambo ya kuzingatia unapotafuta mapenzi au mchumba mtandaoni

sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
5,272
7,870
Kwanza kabisa tambua watu waliopo mitandaoni ndio hao hao mnaokutana mitaani, vyuoni, kwenye nyumba za ibada, maeneo ya starehe, kazini, ufukweni. Lakini zingatia haya yafuatayo sababu maeneo yote hayo kama ilivyo mitandaoni kuna watu wenye tabia mbaya na za kihuni na kuna wenye tabia nzuri. Mtu anaweza kuwa na nia kweli ya kutaka kupata mke au mume but akakutana na changamoto ya kupata mtu sahihi anayemtaka. So zingatia haya

1.Hasa kwa kinadada kwa mara ya kwanza usikubali kukutana na mwanaume nyumbani kwake, lodge au hotelini unaweza lazimishwa kufanya mapenzi bila ridhaa yako au kubakwa bila kumjua mtu vizuri. Kutana nae sehemu ya wazi yenye watu mkishafahamiana vizuri baadaye ndio unaweza kwenda

2.Kwa kinadada ukienda kukutana na mwanaume sehemu ya wazi hakikisha una pesa yako kidogo japo elfu kumi ili hata ikitokea kutokuelewana uwe na pesa yako ya kukusaidia nauli au uweze kulipia kinywaji mwenyewe ili kuepuka kufanya jambo ambalo moyo wako hautaki. Epuka kula vitu vya gharama kama huna pesa inaweza kukuletea changamoto mwanaume akakugeuka

3.Kwa wote wanaume na wanawake ukiona mtu hata hamjaonana lakini ana kuomba omba pesa huyo hakufai achana nae Kama lengo lako lilikuwa kutafuta mwenzi wa kweli mjenge maisha

4.Ukimwambia uliyeonana nae mkapime afya zenu lakini anakupigapiga chenga hataki kwenda kupima afya huyo hakufai achana nae yeye atakuwa anajijua tabia zake hajatulia. Mitandaoni huku wapo watu waliotulia wanaojiheshimu lakini pia wapo machangudoa na wanaume wanaonunua ovyo machangudoa. Kwahiyo umakini wa afya yako ni muhimu

5.Usiwe na haraka kwenda kumuonesha mtu unapoishi maana Kuna wengine ni matapeli hawana nia ya dhati

6.Kama unatafuta mchumba, mume halafu uliyekutana nae anataka penzi fasta fasta bila kujuana vizuri wala kupima afya huyo hakufai

7.Hasa kwa kinadada, Kama mmeshafahamiana kwa muda vizuri ila jamaa hataki kukupeleka anapoishi au kukutambulisha kwa ndugu zake basi tambua huyo ni mume wa mtu

8.Unapokuwa na nia ya dhati kutafuta mpenzi mtandaoni jieleze vizuri kwa uwazi na hiyo itasaidia kupunguza au kuwachuja haraka idadi ya watakaokutafuta ambao hawana vigezo unavyotaka ili kukupunguzia usumbufu
 
mahusiano ni kwa ajili ya sex
ukitaka kusaidiana jiunge vicoba
 
Kwa wale ambao mnajuana, unakua upo tayari kujiweka wazi..lkn unakuta yeye ni msiri siri hatak umjue, hataki hata kukutumia picha ,ukisema umpigie video call hataki

Yaan kwa ufupi anajificha kama Osama Bi Laden wakat wa uhai wake.

Hao unawashauri nn???

Nahunga mkono Mada yako, hasa ukizingatia siku hizi Si Ke wala Si Me..wote wamekua majambazi na mezi na mauaji tu
 
Nilitoaga post ya kutafuta mwanamke wa kuanza naye maisha ya kulala chini (ya shida na raha), 90% ya wanawake wote walinitolea maneno mabovu. Wanawake wanaotafuta wapenzi mtandaoni ni kama wanaomba misaada
 
hiyo ikakufanya ujue umasikin wa kipato na fikra kwa wanawake ,ni changamoto sana.

Hapo usikute unamaisha yako safi tu, ila ulikua unataka kuona utayari wa ndoa

Wenyewe siku hizi wanasema,wanaishi kwa Macho na Masikio
 
Kwa wale ambao mnajuana, unakua upo tayari kujiweka wazi..lkn unakuta yeye ni msiri siri hatak umjue, hataki hata kukutumia picha ,ukisema umpigie video call hataki

Yaan kwa ufupi anajificha kama Osama Bi Laden wakat wa uhai wake.

Hao unawashauri nn???

Nahunga mkono Mada yako, hasa ukizingatia siku hizi Si Ke wala Si Me..wote wamekua majambazi na mezi na mauaji tu
Huyo hakufai hata kidogo , kwan kuna maovu yake ambayo anayaficha ambayo hataki ww uyajue , sasa kama ameamua kuingia kwenye mahusiano na wewe kwa nini awe msiri kwako
 
hiyo ikakufanya ujue umasikin wa kipato na fikra kwa wanawake ,ni changamoto sana.

Hapo usikute unamaisha yako safi tu, ila ulikua unataka kuona utayari wa ndoa

Wenyewe siku hizi wanasema,wanaishi kwa Macho na Masikio
Zama hizi zimekua mbaya sana kimahusiano, ndiyo maana mitaani siku hizi kunaweza pita muda mrefu bila kusikia vigelegele na shamra za sherehe ya harusi, zamani haipiti mwezi utasikia vigelegele vya harusi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom