Mambo ya kuzingatia unapokuwa Mjamzito

Mambo ya kuzingatia unapokuwa Mjamzito

mjusilizard

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2019
Posts
1,025
Reaction score
1,878
Salaam,

Kipindi cha ujauzito kuna mambo mengi yanatokea kwenye mwili wa mama na kufanya mabadiliko ya mwili wake kwa kipindi cha miezi 9. Mara nyingi huwa na hali tofauti kama kutapika, kichefuchefu na kujisikia mwili umechoka na kuvimba miguu au uso n.k

KUHUDHURIA CLINIC ni vizuri mama akaanza kuhudhuria kliniki mapema pindi atambuapo ana mimba sababu atafanyiwa vipimo vingi kwa kujua afya na maelezo ya kulea mimba yake. Na aendelee kuhudhuria mpaka pale atakapojifungua.

Prenatal vitamins au folic acid ni supplements za vitamins zinazotoka kwenye matunda na vyakula anazotakiwa kutumia mama mjamzito kipindi cha miezi 3 ya kwanza ya mimba au kabla hajapata mimba (pindi akiwa anatafuta mimba) kawaida,wanashauri utumie kwa kipindi hicho ila iwapo ukawa umechelewa hujatumia ongea na daktari wako akupe maelezo uanze kutumia. Ni muhimu sana zitakusaidia wewe na mtoto asizaliwe na mapungufu kama kuzaliwa mgongo wazi, kichwa kikubwa au chenye umbo lisiloeleweka.

LISHE huwezi kuzaa mtoto mwenye afya nzuri bila kula lishe bora, mama mjamzito lazima ule chakula chenye virutubisho mbalimbali vitakavyompa nguvu na afya kwake na mtoto.
Kula matunda ya kutosha, mbogamboga za kijani, mafuta na protein ipatikanayo kwa wanyama kama samaki, kuku na nyama, kula vyakula jamii ya mbegu (maharagwe, njegere, kunde, choroko, mbaazi n.k) Mayai, maziwa, jibini (cheese), mtindi, maboga, viazi, mihogo, magimbi (nduma), (ugali, wali na mkate) vyote hivyo unatakiwa ule mara sita kwa siku ili kukuza mtoto na afya yako.

UWE WA KWANZA KUAMKA siyo kuamka kuwa macho ukae kitandani, hapana, toka nje chukua hata fagio fagia, mwagilia maua kama unayo au toka tu nje ila uwe wa kwanza kuamka ukiwa wa mwisho, siku yako ikifika wenzako nao watakuacha wewe ukiwa bado waugulia maumivu (inategemea)

MAJI mama mjamzito anatakiwa kunywa maji mengi wakati wa mimba humsaidia hutoa sumu mwilini na kutengeneza majimaji ya amniotic fluid kuwa ya kutosha yanayohitajika kwa ukuaji vizuri wa mtoto tumboni kwa mama, hakikisha unakunywa maji ukiwa umekaa, hata kama ni barabani tafuta sehemu yenye kiti kaa tulia kunywa maji yako yateremke vizuri.

MAVAZI mjamzito anapaswa zingatia kuvaa mavazi mazuri yenye kusitiri mwili, uvaaji wa nguo za kubana siyo mzuri utakuwa unafanya uchoke zaidi na kutokuwa comfortable.

UREMBO suala la urembo nalo ni muhimu kuzingatia ili usiweze kupoteza urembo wako na usafi. Mimba inapendeza pale mama anapoonekana msafi na nadhifu, ukiwa kazini au upo nyumbani. Kwa wamama wa nyumbani baadhi wanajiachia, siyo vizuri haipendezi kutokujali mwili wako, kuna wengine hawataki kuoga wala kupiga mswaki hapo utampa wakati mgumu mzazi mwenzako, jitahidi kuwa msafi.

PAKA TUMBO MAFUTA KUEPUSHA MICHIRIZI (streatch marks) kipindi cha ujauzito kinachotakiwa paka mafuta mengi tumboni kama (cocoa butter, mafuta ya nazi au palmer oil) inasaidia sana kuepuka michirizi, usikune tumbo likiwasha, paka mafuta kwa wingi fanyia massage hapo utaepuka stretch marks.

EPUKA KUKAA MLANGONI
au kusimama mlangoni, upite mlango ndiyo usimame, kizingiti cha mlango ni kibaya mtoto naye atakuwa anaishia hapo hapo

USIKAE KILA SEHEMU, makalio yako usiyakalishe kila sehemu yenye mchanga, kaa kwenye kiti, kigoda au mkeka

EPUKA KUFANYA MATANGAZO KWA KILA MTU siyo kila mtu anaifurahia hali ya wewe kupata mtoto, hilo ni pembe la ng’ombe waache waone wenyewe hata ndugu zako wa karibu.

UKIFIKA WAKATI WA UCHUNGU NA UPO NYUMBANI MTONYE MTU MMOJA WA KWENDA NAYE NA UONDOKE KIMYA KIMYA USIAGE MTU.

PENDELEA KULA BAMIA (MABENDA), MLENDA,
katakata bamia weka maji na chumvi koroga mpaka liive kisha kula na ugali au kunywa kama lilivyo, husaidia mtoto kuteleza kwa urahisi

MWISHO NI MAZOEZI, tembea mwendo mrefu ili kulainisha misuli ya kizazi chako. Mazoezi ya kunyoosha mwili (stretching) au Yoga. Mazoezi ya kuogelea. Ufanyaji mazoezi humsaidia mwili usichoke. Yanamsaidia mama kuja kujifungua kwa urahisi bila oparesheni.

Kila la heri!
 
#Lliendie

Pita hapa Mrs barakoa

stidy
 
Back
Top Bottom