Mambo ya kuzingatia kuepuka matukio ya moto unaosababishwa na Umeme majumbani

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,859
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA MATUKIO YA MOTO UNAOSABABISHWA NA UMEME MAJUMBANI.

1.Hakikisha utandazaji nyaya (wiring) inafanywa na mkandarasi aliyesajiliwa na Serikali

2.Hakikisha vifaa vyote vinavyofungwa vimethinitishwa na TBS (K.m: nyaya, soketi swichi, saketi breka na main swichi)

3.Hakikisha waya wa ethi umethibitishwa na TBS na umechimbiwa chini ardhini inavyotakiwa

4.Hakikisha unapotumia pasi usiiache ikiwaka ukaenda kufanya kazi nyingine. Vyivyo hivyo tutumiapo hita za kuchemshia maji na majiko ya umeme.

5.Tusinyooshe nguo kwa pasi ya umeme kitandani

6.Tuepuke utumiaji wa extension cable wa kudumu. Zitumike kwa dharura tu. Pia tusiweke extension cables kwenye mazuria (carpets)

7.Tusichaji simu na kuziweka kitandani. Pia tusitumie kompyuta mpakato (laptops) tukiwa tumezieka kitandani

8.Tusi plagi vitu vingi vinavyotumia umeme kwenye soketi moja kwa mfano TV radio na friji kwenye soketi moja

9.Tusiweke mapazia marefu kwenye madirisha yanayofunika soketi za umeme

10.Tutumie mapazia yasiyoshika moto kwa urahisi; kwa mfano mapazia ya nguo za pamba

11.Tuangalie magodoro ya vitanda yasikaribie au kugusa sokti au swichi za umeme

12.Makochi yetu tusiyaweke yakagusa au kukaribia sana swichi au soketi ya umeme. Yawekwe angalau umbali wa inchi sita (15sm)

13.Vyandarua vya vitanda visisogelee swichi au soketi ya umeme

14.Tupunguze wingi wa vitu vinavyoweza kuwaka moto ndani ya nyumba; kwa mfano, ni vizuri kuwa na seti moja tu ya makochi

15.Kama umeme ulikuwa umezima, ukiwaka tena kitu cha kwanza tuhakikishe mishumaa yote tuliyoiwasha wakati umeme umezimika tumeizima.

16.Kama fyuzi ya umeme itakatika au soketi breka ikajizima, tuhakikishe tumemwita fundi kukagua kwa nini ilizima. Tusiweke fyuzi nyingine au kuwasha tu saketi breka.

17.Tuhakikishe tunamwita mkandarasi aliyesajiliwa kupitia mfumo wote wa umeme kwenye nyumba (hasa maungio yote) kila baada ya miaka mitano

18.Tusiongeze vitu vinavyotumia umeme mwingi kama viyoyozi bila kuwahusisha makandarasi waliosajiliwa kuangalia uwezo wa mifumo yetu ya umeme kuhimili mzingo unaoongezeka.

19.Tusiunganishe umeme kutoka nyumba moja kwenda nyingine au kwenda kwenye banda la kuku bila ya kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa

20.Ikitokea hitilafu yeyote ya umeme kuanzia kwenye mita ya TANESCO, braketi nguzo na kwenye laini ya umeme, tutoe taarifa katika kituo chochote cha TANESCO kwa kutumia namba za dharura.

TANESCO ''TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO''.
 
Elimu nzuri,sisi tunaish gheto tuna mpanglio mbaya sana wa vitu na jinsi ya kutumia vifaa hvyo vya umeme kama heater na pasi pamoja na kompyuta.inabidi kuwa makin sana!
 
Haya yote sawa ila nilichoshuhudia majuzi kwa jirani kuna umuhumu mtu ukijenga jumba lako tafuta insurance. Ni jumba la ukweli liliteketea na moto hadi huruma zimamoto walifika saa 9 moto ulizima saa 12 jion gari likitoka moja jingine linaingia dah

kulikuwemo watoto wamelala kilichosaidia wananchi walifika mapema wakavunja vioo wakawatoa wakiwa hai ila wako hoi kwa moshi ule dah.

kumbe na mabati yanaungua hivyo? Mitungi ya gesi inalipuka kama bomu?

Asante kwa elimu mleta mada tuwe makini.
 
Aiseeeeehhh nimeogopa chanzo cha moto kilikua nn mkuu?
 
MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KUEPUKA MATUKIO YA MOTO UNAOSABABISHWA NA UMEME MAJUMBANI.

1.Hakikisha utandazaji nyaya (wiring) inafanywa na mkandarasi aliyesajiliwa na Serikali

2.Hakikisha vifaa vyote vinavyofungwa vimethinitishwa na TBS (K.m: nyaya, soketi swichi, saketi breka na main swichi)

3.Hakikisha waya wa ethi umethibitishwa na TBS na umechimbiwa chini ardhini inavyotakiwa

4.Hakikisha unapotumia pasi usiiache ikiwaka ukaenda kufanya kazi nyingine. Vyivyo hivyo tutumiapo hita za kuchemshia maji na majiko ya umeme.

5.Tusinyooshe nguo kwa pasi ya umeme kitandani

6.Tuepuke utumiaji wa extension cable wa kudumu. Zitumike kwa dharura tu. Pia tusiweke extension cables kwenye mazuria (carpets)

7.Tusichaji simu na kuziweka kitandani. Pia tusitumie kompyuta mpakato (laptops) tukiwa tumezieka kitandani

8.Tusi plagi vitu vingi vinavyotumia umeme kwenye soketi moja kwa mfano TV radio na friji kwenye soketi moja

9.Tusiweke mapazia marefu kwenye madirisha yanayofunika soketi za umeme

10.Tutumie mapazia yasiyoshika moto kwa urahisi; kwa mfano mapazia ya nguo za pamba

11.Tuangalie magodoro ya vitanda yasikaribie au kugusa sokti au swichi za umeme

12.Makochi yetu tusiyaweke yakagusa au kukaribia sana swichi au soketi ya umeme. Yawekwe angalau umbali wa inchi sita (15sm)

13.Vyandarua vya vitanda visisogelee swichi au soketi ya umeme

14.Tupunguze wingi wa vitu vinavyoweza kuwaka moto ndani ya nyumba; kwa mfano, ni vizuri kuwa na seti moja tu ya makochi

15.Kama umeme ulikuwa umezima, ukiwaka tena kitu cha kwanza tuhakikishe mishumaa yote tuliyoiwasha wakati umeme umezimika tumeizima.

16.Kama fyuzi ya umeme itakatika au soketi breka ikajizima, tuhakikishe tumemwita fundi kukagua kwa nini ilizima. Tusiweke fyuzi nyingine au kuwasha tu saketi breka.

17.Tuhakikishe tunamwita mkandarasi aliyesajiliwa kupitia mfumo wote wa umeme kwenye nyumba (hasa maungio yote) kila baada ya miaka mitano

18.Tusiongeze vitu vinavyotumia umeme mwingi kama viyoyozi bila kuwahusisha makandarasi waliosajiliwa kuangalia uwezo wa mifumo yetu ya umeme kuhimili mzingo unaoongezeka.

19.Tusiunganishe umeme kutoka nyumba moja kwenda nyingine au kwenda kwenye banda la kuku bila ya kuwatumia wakandarasi waliosajiliwa

20.Ikitokea hitilafu yeyote ya umeme kuanzia kwenye mita ya TANESCO, braketi nguzo na kwenye laini ya umeme, tutoe taarifa katika kituo chochote cha TANESCO kwa kutumia namba za dharura.

TANESCO ''TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO''.
 
Aisee inabidi TANESCO wakutunuku walau unit 2 za Luku
kwaajili ya matumizi ya mji wako.
Maana umeongea ukweli mtupu "you spoken the naked truth".
 
Aiseeeeehhh nimeogopa chanzo cha moto kilikua nn mkuu?
wengine wanasema ni umeme wengine wanasema ni gesi ila moto ulianzia chumbani so ni umeme maana tulipofika moto mkubwa ulionekana kutoka chumbani ndipo uliposambaa kwenye vyumba vingine nitungi ya gesi inaripuka, kama bomu.

yaan lile jumba kilikuwa limeungana na vyumba vya wapangaji sasa hiyo mitungi ya gesi si kwa kulipuka kule.

Aisee zima moto wale watu wanafanya kazi yaan wao moto unawaka ndani wamo yaan ilikuwa ni balaa. Mwenye nyumba alizimia uko kazini dah.
 
Aiseee lazma uzimie dahhhh hatari sana hii,shukrani kwa taarifa
 
Back
Top Bottom