Mambo ya kuzingatia kabla hujasafiri kwa gari lako dogo

Danken Mbombo

JF-Expert Member
May 30, 2015
651
339
Zingatia mambo haya muhimu, jiulize maswali na upate majibu sahihi kabla hujaanza safari yako ili tusaidiane kupunguza ajali zinazo epukika.

1. Ni lazima usafiri na gari ndogo?

2. Unao uwezo wa kuendesha kwa safari ndefu?

3. Gari yako ina uwezo wa safari ndefu?

4. Tairi za gari yako zinafaa? (zingatia muda wake wa matumizi na siyo kuangalia tu “tread”)

5. Hakikisha unaijua vizuri barabara na kama huijui nenda kwa tahadhari kubwa

6. Usiendeshe gari kwa kasi kubwa - kama ni lazima zingatia: UWEZO wa gari na wa dereva, UBORA wa barabara na wa tairi za gari yako, uwe na kiwango kasi cha juu salama mfano 80km/h na ukiheshimu.

7. Usifanye mashindano na madereva wa magari mengine.

8. Usinywe pombe - kujifanya unaweza kuendesha gari ukiwa umekunywa ni USHAMBA.

9. Chunga sana mwendo wako unaposafiri na gari nyepesi kama NOAH, SALOON (hasa za kijapani) inashauriwa 80km/h.

10. Usiendeshe mfululizo zaidi ya masaa mawili bila kupumzika - ni muhimu sana kwa usalama na kwa afya yako.

11. Ukihisi usingizi machoni mwako paki gari pembeni, jiegeshe kwa muda dk 20, dk 30 hata saa nzima, kwani unakimbilia nini?

12. Usitumie kabisa simu – zima au weka silence hadi ukipumzika.

13. Zingatia na kuheshimu alama zote za usalama barabarani zitakusaidia na kukuokoa.

KILA LA HERI
 
9. Chunga sana mwendo wako unaposafiri na gari nyepesi kama NOAH, SALOON (hasa za kijapani) inashauriwa 80km/

KILA LA HERI
Post nzuri la 80km/h ni spidi ndogo kama unasafiri masafa marefu na gari ndogo. 120km/hour nafikiri ni spidi ya wastani na inafaa.
 
hii elimu ingelikuwa bora kama ingelitolewa wakati kwa krismas wakati watu walikuwa wanenda vijijini huu ulikuwa muda Muafaka kwa watu kujifunza
 
Zingatia mambo haya muhimu, jiulize maswali na upate majibu sahihi kabla hujaanza safari yako ili tusaidiane kupunguza ajali zinazo epukika.

1. Ni lazima usafiri na gari ndogo?

2. Unao uwezo wa kuendesha kwa safari ndefu?

3. Gari yako ina uwezo wa safari ndefu?

4. Tairi za gari yako zinafaa? (zingatia muda wake wa matumizi na siyo kuangalia tu “tread”)

5. Hakikisha unaijua vizuri barabara na kama huijui nenda kwa tahadhari kubwa

6. Usiendeshe gari kwa kasi kubwa - kama ni lazima zingatia: UWEZO wa gari na wa dereva, UBORA wa barabara na wa tairi za gari yako, uwe na kiwango kasi cha juu salama mfano 80km/h na ukiheshimu.

7. Usifanye mashindano na madereva wa magari mengine.

8. Usinywe pombe - kujifanya unaweza kuendesha gari ukiwa umekunywa ni USHAMBA.

9. Chunga sana mwendo wako unaposafiri na gari nyepesi kama NOAH, SALOON (hasa za kijapani) inashauriwa 80km/h.

10. Usiendeshe mfululizo zaidi ya masaa mawili bila kupumzika - ni muhimu sana kwa usalama na kwa afya yako.

11. Ukihisi usingizi machoni mwako paki gari pembeni, jiegeshe kwa muda dk 20, dk 30 hata saa nzima, kwani unakimbilia nini?

12. Usitumie kabisa simu – zima au weka silence hadi ukipumzika.

13. Zingatia na kuheshimu alama zote za usalama barabarani zitakusaidia na kukuokoa.

KILA LA HERI
Good food 4 thought, big up
 
Back
Top Bottom