Mambo ya Kuzingatia ili kufanikiwa Kibiashara

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,480
5,504
Biashara yoyote ile nje ya kuwa na huduma/bidhaa inayokidhi mahitaji ya wateja inahitaji kuwa na upekee ili kuhakikisha kwamba inafanikiwa katika soko.

Katika desturi za kiafrika huwa kuna baadhi ya watu hutumia mitishamba katika kuongeza mvuto wa biashara.Hii yote ni kutokana na ukweli kwamba ili kufanikiwa kibiashara unahitaji zaidi ya bidhaa ili kufanikiwa.Kabla ya kufanya biashara yoyote ni lazima ufanye yafuatayo:
  1. Fanya Utafiti wa soko.Hakikisha utafiti unaofanya ni wa kitaalamu na taarifa unazokusanya zitakuwezesha kufanya maamuzi ya kibiashara hasa ukizingatia ushindani na ubora wa huduma.Iwapo matokeo ya kiutafiti yataonesha kwamba biashara haitafanikiwa basi unaweza kufanya utafiti mwingine ama kuanzisha pilot project(Mradi wa majaribio katika kuthibitisha ukweli wa Takwimu zako).Zoezi la utafiti linaweza kuchukua si chini ya Miezi miwili hadi miaka 3 kwa kutegemea aina ya biashara,kiwango cha mtaji n.k.
  2. Fanya uhakiki wa uwezo wako hapa ni muhimu sana ili kutambua iwapo mtaji wako wa kifedha na kitaalamu utakuwezesha katika kuendesha biashara unayotaka kufanya.Angalia iwapo una uhitaji wa mafunzo au uzoefu fulani ujifunze na iwapo unahitja mtaji zaidi wa kifedha basi tafuta vyanzo vya ziada.Angalia tabia yako ya utumizi ili kuhakikisha kwamba hutumii zaidi ya unavozalisha.
  3. Kuwa makini na chaguo la location
  4. Kuwa makini na ina ya watumishi utakaoajiri
  5. Kuwa makini na hali ya jumla ya soko/ushindani
  6. Kuwa makini na maswala ya kisheria kama leseni,kodi n.k.
  7. Kuwa makini na utumizi wa teknoljia,hakikisha unatumia teknolojia katika kuhakiksha uwekezaji wenye TIJA
Karibuni tujadili kwa pamoja haya namengineyo
 
Back
Top Bottom