mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Gazeti la Mwananchi, Jumapili Mei 15, 2016 limeandika taarifa ya habari hapo juu. Mambo hayo ni:
1) Uuzaji nyumba
2) Boti ya MV D'Salaam
3) Uuzaji mashirika
4) Meli ya uvuvi
5) Skandali kubwa (ufisadi EPA, ESCROW na lugumi)
Nawasilisha bandiko hili kuchangia katika maoni na mawazo ya baadhi wa Wachambuzi wa masuala mbalimbali ambao wamenukuliwa na hilo gazeti kwamba:
1) Dk Magufuli atakuwa njia panda katika mambo mbalimbali ambayo yalitokea katika Wizara alizokuwa akiziongoza.
2) Uchunguzi wa CAG, ulibainisha mapungufu mengi ya kiutendaji na ufisadi katika Wizara ambazo Rais alikuwa Waziri, hivyo inamtaja moja kwa moja kuhusika.
3) Rais Magufuli wakati akiwa Waziri alikuwa akiyajua masuala hayo, je, anaweza kuchukua hatua zinazostahili kwa maslahi ya Taifa.
4) Kama Rais Magufuli ataitumbua Wizara ya Ujenzi tutajua wazi kuwa yalikuwa maamuzi yake - kwa kuwa hatuwezi kujua yaliyotajwa na CAG yalitokana na maamuzi ya nani (Rais au Waziri wakati huo).
Katika uongozi kuna masuala makuu mawili, nayo ni:
1) Kukasimu madaraka hakukuondolei wajibu (delegation does not relieve you responsibility)
2) Uwajibikaji wa pamoja (collective responsibility)
Ieleweke kwamba wa kukasimu, ni mhimu kuacha kiasi fulani cha kutosha cha kudhibiti, lakini kamwe huwezi kukwepa hatua mbali na kuwajibika. Njia moja ya kufanya hivyo ni kuachia madaraka yote lakini kwa kudumisha dhima. Kukwepa mamlaka kwa kukasimu madaraka si njia sahihi ya uongozi wa kidemokrasia.
Je, ni kweli Rais Magufuli yuko njia panda au ni sahihi kumbebesha Rais Magufuli kwa yale aliyoyatenda akiwa Waziri.
Natoa hoja.