Mambo nyeti ya kuzingatia katika mahusiano

Mambo nyeti ya kuzingatia katika mahusiano

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,231
USHAURI TU KWA KINAKAKA (TAKE IT OR LEAVE IT)
UNAPOANZA UHUSIANO MPYA EPUKA WANAWAKE WA AINA HII

1.DEMU WAKO WA ZAMANI-
Ni vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi, kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.

2.DADA WA RAFIKI YAKO KIPENZI-
Epukana na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa, ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.

3.WANAWAKE WENYE MAMBO MENGI-
Kiukweli, kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja kuyajutia kwa maisha yako yote.

4.WANAWAKE WANAOPENDA HELA KUPITILIZA (WACHUNAJI)-
Kuwa mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa zaidi.

5.DEMU WA ZAMANI WA RAFIKI YAKO-
Kama unathamini urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani
 
Mahusiano huwa hayana kanuni.

Fanya utakavyofanya, jidhatiti utakavyijidhatiti, ila pale upepo utakapobadilika kwa kweli huwa hakuna kipangimizi
 
Umesahau moja, wanawake wenye makalio makubwa!! Siku hizi mwanamke akiwa na makalio makubwa anakuwa msumbufu sana na akili zake zinaendeshwa na makalio yake, yaani mwanamke ata awe mzuri vipi akikosa kalio confidence zote zinampotea!!

Hili ni janga jipya kwa waoaji
 
Jamani inauma sanaaa,,ombea isitokee demu wako wa mwaka mmoja abakwe atolewe bikra na apewe mimba hpohpo,inaniuma
 
Back
Top Bottom