Mambo nane(8) ya kufanya kumsahau mtu aliyekuumiza kwenye mahusiano

Stanboy

JF-Expert Member
Jul 4, 2013
1,114
1,305
MAMBO NANE(8) YA KUFANYA KUMSAHAU MTU ALIYEKUUMIZA KWENYE MAHUSIANO:

Kuumizwa ama kuachwa pale usipotarajia limekuwa ni tatizo linalowakumba watu wengi,suala hili lina madhara makubwa kwa mhusika kisaikolojia,kiuchumi,kijamii na hata kiafya na wakati mwingine linaweza kusababisha KIFO.

Sasa basi ufanye nini unapoachwa ama kuumizwa bila kutarajia?
Zifuatazo ni baadhi ya njia zinazoweza kukusaidia kuendelea kuwa katika hali ya kawaida unapopatwa na hili tatizo...

1.KUMBUKA MABAYA YOTE ALIYOWAHI KUKUFANYIA.
Jitahidi kukumbuka mambo yote mabaya aliyokufanyia huyo mtu kama kukusaliti,kukupiga,kukutukana hadharani,kukudhurumu pesa zako,kukusema vibaya n.k

2.KUMBUKA MADHAIFU YAKE YOTE.
Yakumbuke madhaifu yake yote Uliyokuwa unamvumilia tu ili siku ziende.
Mfano wazazi wako walikuwa wanakugombeza sana kuhusu yeye(kwanini unamng'ang'ania),alikuwa mchafu,mnuka mdomo,mnuka kikwapa,hajui kupika,muongo,msaliti,ana matege,alikuwa anapata magonjwa ya zinaa mara kwa mara,mgomvi,malaya(muhuni),hana hela,baadhi ya ndg zako hawampendi kabisa,anapenda kujipendekeza,hajui mapenzi,uso mpana kama wa mbuzi,maskini,kazi mbaya,hajui kuvaa vizuri n.k
Yaani kwa kifupi hapa tafuta visababu vyote vibaya ulivyokuwa unamvumilia maana vitakufanya uone ulikuwa na jipu lenye usaha kabisa ilibaki kutumbuliwa tu na muda ndo huo limejitumbua lenyewe.

3.SITISHA MAWASILIANO NAYE KABISA.
M-block kuanzia simu za kawaida,facebook,whatsapp,instagram,twitter n.kPia punguza au sitisha kabisa mawasiliano na ndg zake,jamaa na rafiki zake.Kumbuka mawasiliano ni moja ya nguzo kuu za mahusiano,hivyo kama utaendelea kuwasiliana naye mtarudiana halafu atakuumiza tena.

4.EPUKA KWENDA MAENEO MLIYOKUWA MNAENDA PAMOJA.
Usipende kwenda sehemu mlizokuwa mnakwenda pamoja,maana kama utaenda utamkumbuka.Labda utakutana na watu waliozoea kuwaona pamoja watakuulizia yeye yupo wapi?

5.USIANZISHE MAHUSIANO MAPYA KWA HARAKA.
Usikurupuke KUTAFUTA MTU MPYA kwa haraka kwa lengo la kumkomesha maana utajikomesha mwenyewe pale utakapokuwa na mtu wa hovyo na kujikuta unamkumbuka zaidi aliyekuumiza.Tafakari kwanza ulipokosea na kuwa mtulivu kabla ya kuanza upya..Jipe angalau miezi 3 ya kutafakari na kuangalia yupi anafaa kuziba pengo.

6.KUWA MAKINI NA USHAURI WA RAFIKI ZAKO.
Epuka USHAURI WA MARAFIKI ZAKO,marafiki wengi ushauri wao huwa siyo mzuri(hupoteza)..wengine watakuambia tafuta mwingine kumbe wamefurahi umekosa bahati ambayo ungeipata wangeumia maana ungewazidi...sana sana kama unaona wewe huwezi kuendelea na huo mzigo waambie wazazi wako hasa mama zetu huwa wana ushauri mzuri sana maana wanatupenda kuliko mtu yoyote hapa duniani.

7.ONGEZA MUDA ZAIDI KWENYE MAMBO YAKO YA MSINGI.
Ongeza muda zaidi(KUWA BUSY) na mambo yako muhimu kama kazi,biashara,masomo,kilimo n.k hii itakuchosha akili na mwili hivyo hutapata muda wa kuwaza sana mambo ya mapenzi.

8.WAONE VIONGOZI WA DINI NA HUDHURIA KWENYE NYUMBA ZA IBADA(MSIKITINI NA KANISANI)
Unapopata muda waone viongozi wa dini wana maneno ya kufariji mno na kutia nguvu kuendelea na maisha bila shaka utajiona wewe ni wa kawaida na amani na furaha vitarudi kwako..

Kuwa makini,Mapenzi hugeuka vita.

[HASHTAG]#SHAREDBLESSINGS[/HASHTAG]

Kwa ushauri Zaidi nicheki whatsapp Pm
 
Unaeza fanya yote hayo na bado usimsahau, mim nazan cha msingi ni kuamin na kukubali kuwa maisha yanaanza na wewe kwanza, then wengne, who ever comes into your life should not be of much importance than yourself first, ukikubaliana na hili, maisha ya mapenzi yatakuwa mazuri sana na hata kama ukiumizwa, itakua rahis ku-move on

[HASHTAG]#People[/HASHTAG] come and go like seasons
 
Hivi unashindwaje kumsahau mtu mliyeachana. Mie naona hayo ni kama mapungufu au ndio sijui kupenda mie maana siwezi eti mtu aniache nishindwe kuendelea na maisha
 
Rahisi sana kuyaandika.tatizo kama ulimpenda kupindukia haya hayatekelezeki.mwombe tu Mungu akupe moyo wa kutopenda kupindukia
 
Some broken hearts never mend...... Some wounds never heal...... Some tears will never dry.............
 
Kuachwa Kuna maumivu yake jamani,hayo yanawezekana kwa mtu ambae km ulikuwa hujampenda sana. Cha msingi tujifunze kupenda kidogo.
 
Back
Top Bottom