ilifaa zaidi jukwaa la dini.
Kulingana na uelewa wangu ni jukumu kubwa sana kuwa mama au baba wa ubatizo wa mtu.
Unatakiwa kumsaidia kukua kiimani kuanzia siku unapomsimamia hadi mwisho wako.
Kama ujuavyo, nasaha ya siku moja haimjengi mtu, huwa inakuwa kama 'formality' fulani tu, kinachomjenga mtu ni malezi madogo madogo ya kila siku.
Anyway, kwa siku hiyo ningekuwa ni mie ningemwambia kwanza akiri imani ya kanisa, na ningempa usia kushikilia imani aliyoikiri maana ndio 'uti wa mgongo' wa imani yenu.