Mambo muhimu kuhusu kujiandikisha

Mambo muhimu kuhusu kujiandikisha

LIKUYU SEKA

Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
53
Reaction score
24
Habari watanzania wenzangu natumai tumeianza wiki vyema,kwa wale wagonjwa nawapa pole mungu awaponye na wenye matatizo pia mungu awape njia ya kutatua matatizo yao.

Ndugu zangu sote tunajua kuwa nchi yetu inaelekea kwenye uchaguzi mkuu oktoba mwaka huu ikiwa ni sambamba na zoezi la uandikishaji kwenye daftari la kudumu la mpiga kura,zoezi la uandikishaji lilianza mwanzoni mwa mwaka huu likizinduliwa mkoani njombe na safari hii tukitumia mfumo mpya Wa uandikishaji unaotambulika kama Biometric Voter Registration (BVR).

Huu ni mfumo mpya Wa uandikishaji kwa hapa nyumbani mfumo huu una uwezo mkubwa Wa kutambua muandikishwaji,Tume ya taifa ya Uchaguzi imesambaza mashine za Uandikishaji katika kanda ambazo zoezi hilo linafanyika.

Mpaka sasa tayari mikoa 5 imekamilisha zoezi la Uandikishaji wa wapiga kura mikoa hiyo ni Njombe,Lindi,Mtwara,Iringa na Ruvuma,yapo mambo muhimu kwa wale ambao bado hawajafikiwa kuandikishwa kuyajua.

Mambo muhimu kwa wale ambao hawajaandikishwa ya kuzingatia mosi ni kuwa zoezi la kujiandikisha limepata muitikio mkubwa sana,wananchi wengi nimeshuhudia wakijitokeza kwa wingi katika vituo vya kuajindikisha,jambo la kwanza la msingi ni kuwahi katika kituo cha kujiandikisha ukiweza uwahi mapema sana uzoefu unaonesha kuwa vituo vinafunguliwa saa mbili asubuhi hvyo kuwahi ni jambo la msingi sana ili waandikishaji watakapofika uwe wakwaza kujiandikisha.

Pili ni kwamba yapo mambo ambayo wakati Wa kuajindikisha unaulizwa,miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na jina lako kamili,mahali ulipozaliwa,tarehe na mwaka pamoja anuani yako ya kudumu haya ni mambo muhimu sana..

Tatu ni kuwa mashine ya BVR kwasiku huandikisha watu wasiozidi 120 na idadi hii ni pale endapo mashine haijaleta hitilafu yoyote,yapo maeneo ambayo mashine inaandikisha zaidi ya watu 120 lakini haivuki 180,hvyo kama umefika kwenye kituo cha kuajindikisha na ukaona wewe foleni yako umepitwa na watu zaidi ya 120 ujue hutaweza kuajiandikisha siku hiyo.

Kwauchache watanzania wenzangu haya ni mambo ambayo tunapaswa kuyazingatia ili kufanikiwa katika zoezi la kujiandikisha,Natoa rai Watanzania wenzangu kujitokeza kwa wingi kushiriki kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la mpiga kura.
 
Mwenyekiti wa NEC amepiga marufuku jitihada za CHADEMA kuhamasisha watu kujiandikisha kupiga kura huko Singida.

CHADEMA walikuwa wanatumia vipeperushi na matangazo ya magari kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi.

Kauli hii ya Mwenyekiti wa NEC inanishangaza kwani kila chama kina haki ya kuhamasisha wafuasi wake kujiandikisha na hiyo ndio kazi ya siasa.

Hii inatupelekea tuhisi Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina agenda ya siri maana katika hali ya kawaida Tume ingefurahi kwa vyama kufanya kazi ya uhamasishaji.

nanukuu maelezo ya Mwenyekiti wa tume DAMIAN LUBUVA aliyoandika katika kitabu alichowaandikia vyama vya siasasa kitabu hicho kinaitwa MAELEKEZO KWA VYAMA VYA SIASA.

UJUMBE WA MWENYEKITI.
"katika uboreahaji wa daftari la kudumu la wapiga kura,ushirikiano mkubwa unahitajika kati ya tume ya taifa ya uchaguzi ,vyama vya siasa na wadau wengine.Vile vile ,ili utekelezaji wa zoezi hili uwe na mafanikio mazuri , ni muhimu kuwepo elimu kwa umma na uhamasishahi wa kutosha juu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, aidha utaratibu wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura hauna budi ueleweke vizuri"

hapa tena akaendelea kuandika

"maelekezo yaliyomo katika kijitabu hiki yameandaliwa ili kuvisaidia vyama vya siasa viweze kushiriki katika kuelimisha na kuhamasisha wananchi juu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura"


hapa akaendelea kuandika

"napenda kutoa wito kwa viongozi wa vyama vya siasa kutumia fursa hii kujielimisha juu ya dhana ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ,utaratibu na hatua zitakazotumika katika zoezi hili"

MAELEZO HAYO YOTE JUU YANAPATIKANA KATIKA UKURASA WA (iii).

katika ukurasa wa 1. kuna maelezo mengine kuhusu swala la uhamasishaji.

nanakiri maelezo hayo.

"vyama vya siasa vina wajibu mkubwa wa kuwaelekeza na kuwaelimisha wanachama wao na wananchi kwa ujumla umuhimu wa kuwemo katika daftari la kudumu la wapigakura ,na utaratibu utakaotumika katika uboreshaji wa daftari hilo.Hivyo ni muhimu kwa vyama vya siasa kuhamasisha na kuelimisha wanachama wao pamoja na wananchi kwa ujumla ili waweze kufahamu na kuelewa uboreshaji wa daftari hilo, haki na wajibu wao"

KABLA NA WAKATI WA UBORESHAJI

"kwa kuwa uboreshaji utafanyika katika kipindi cha siku kumi na nne(14) tu, ipo haja kwa vyama vya siasa kabla na wakati wa kipindi hicho , kuwahimiza wananchi wajitokeze kujiandikisha wakati wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura"

WAKATI WA UKAGUZI WA DAFTARI

"ni wajibu wa vyama vya siasa kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi umuhimu wa kukagua daftari la awali la wapiga kura mara litakapowekwa wazi kwa ukaguzi.

daftari la awali la wapiga kura litakuwa kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura kwa muda usiozidi siku saba.kwa hiyo kuna umuhimu mkubwa wananchi kuhamasishwa kujitokeza bila kuchelewa kukagua daftari hilo.

wananchi pia waelimishwe kuhusu utaratibu mzima wa kuweka pingamizi kama watakuwa na sababu za msingi. vile vile waelimishwe kuwa wana haki ya kukata rufaa kwenye mahakama ya wilaya ,iwapo hawakuridhika na uamuzi uliotolewa kuhusu pingamizi walilowekewa au waliloweka"

baada ya nukuu zote hizo hapo juu ambazo zimetokana na MAELEZO YA TUME YA UCHAGUZI CHINI YA JAJI MASTAAFU DAMIAN LUBUVA.

nitoe masikitiko yangu makubwa kama hili limetokea na kuamrisha CHADEMA ISITISHE UHAMASISHAJI KATIKA HILO ULILOTAJA.

kwa kuwa maelekezo hayo yanaenda kinyume na ujumbe wa jaji huyuhuyu alioutoa kwa vyama vya siasa.

lakini kibaya zaidi yanakiuka taratibu za kanuni na sheria ya uchaguzi.

hivyo vyama vya siasa visitishwe na kauli hiyo ya Lubuva kuzuia uhamasishaji. na badala yake viendelee kuwahamasisha na kuwaelimisha wananchi ili wasipoteze haki yao.

na kwa kuwa hakuna utaratibu uliotolewa ni kwa namna gani uhamasishaji ufanyike. itakuwa si kosa kwa vyama kuandaa na kuchapisha vipeperushi vya kuelimisha na kuhamisha, pia si kosa kutoa matangazo kwa spika, mikutano na hata matangazo kwa njia ya radio na television.

NA:
KATIBU MWENEZI CHADEMA KATA YA MSIGANI(jimbo la ubungo).
Joseph Mshinga.
 
ASANTE SANA, HIZI NDO DONDOO MUHIMU NA NDO KAZI YA TUME KUHAKIKISHA KILA MWANCHI ANA PATA UTARATIBU UNAVYOKWENDA, SIO KULEWA MADARAKA NA KUOTA NDOTO ZA KUPIGA MARUFUKU CHADEMA, UKAWA, CUF n.k. WASIHAMASISHE WATU KUJIANDIKISHA........ Bloooody Fooooool NEC

"..............................................................................Pili ni kwamba yapo mambo ambayo wakati Wa kuajindikisha unaulizwa,miongoni mwa mambo hayo ni pamoja na jina lako kamili,mahali ulipozaliwa,tarehe na mwaka pamoja anuani yako ya kudumu haya ni mambo muhimu sana..

Tatu ni kuwa mashine ya BVR kwasiku huandikisha watu wasiozidi 120 na idadi hii ni pale endapo mashine haijaleta hitilafu yoyote,yapo maeneo ambayo mashine inaandikisha zaidi ya watu 120 lakini haivuki 180,hvyo kama umefika kwenye kituo cha kuajindikisha na ukaona wewe foleni yako umepitwa na watu zaidi ya 120 ujue hutaweza kuajiandikisha siku hiyo........................................................"
 
Back
Top Bottom