Mambo muhimu kuhusu Airbus A220-300

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
1) Ndege hii ina urefu wa ni mita 38.7, na kwa jumla inaweza kuketi abiria 141.

2) Urefu wake kutoka chini kwenda juu ni mita 11.5, na upana wa mabawa yake ni mita 35.1.

3) Inaweza kusafiri umbali wa 5,920km safari moja, na inaweza kupaa ikiwa na uzani wa tani 67.6, na kutua ikiwa na uzani wa tani 58.7.

4) Ndiyo ndege kubwa miongoni mwa ndege za familia ya A220.
5) Imeundwa kupunguza gharama ya matumizi yake ya mafuta kwa kila safari na pia kuwa yenye uwezo wa juu.
6) Injini zake zimepunguza matumizi ya mafuta kwa kila abiria kwa asilimia 20 ukilinganisha na ndege za awali za aina yake.
7) Zimejengwa kwa vipande vinavyoweza kutengenezwa kwa haraka kiwandani iwapo vitahitajika wakati wa ukarabati.
8)Injini zake pia huwa za familia moja. Marubani waliozoea ndege aina ya A220-300 na A220-100 hawahitaji mafunzo zaidi kuweza kuziendesha.

**Ndege za Airbus A220 zilikuwa zinafahamika kama Bombardier CS100s kabla ya Airbus kuununua mradi huo wa utengenezaji wa ndege za C Series**

*Tunatekeleza
 
Hii nchi nsg zangu mmh!!.
Jamaa alipopewa vipande vya chupa akaondoka anashangilia kama zuzu..!!
 
Back
Top Bottom