mambo muhimu katika katiba mpya ni matano !

Tango73

JF-Expert Member
Dec 14, 2008
2,128
1,225
1 -Ujamaa na kujitegemea lazima ufutwe na kulaaniwa
2-kifungu kimkingacho raisi asishitakiwe kifutwe na raisi lazima ashitakiwe kama ana makosa
3-mahakama kuu na bunge lazima ziwe huru na ziwe na nguvu
4-tume ya uchaguzi iwe huru, TAKURU nayo iwe huru
5-adhabu ya kifo kwa MAFISADI

Ndugu zangu watanzania, kama jaji warioba hajaweka mambo haya katika katiba mpya, basi tujue nchi si mali ya wananchi bali ni mali ya watu wachache.

tusije kukubali kumpigia kura raisi ambaye hukingwa na katiba kuwa sishitakiwe kama na makosa. Kama Israel wana haki ya kumshitaki kiongozi wao akifanya makosa na wameendeleo kupita kiasi sisi lazima tuige ili nasi tusije achwa nyuma kimaendeleo.
 
Binafsi nakubaliana na mambo hayo matano lakini ni vizuri pia kupendekeza

1. ideologia mbadala ambayo itachukua nafasi ya ujamaa na kujitegemea ambao kwa maoni yanguu haukutekelezwa hata kwa robo yake na hivyo unahukumiwa bila kuwa ulifanya yale yaliyotarajiwa. Ideolojia mbadala ni ile itakayotoa uwiano kati ya dola ya kidemokrasia ambayo itakuwa imara na dhabiti kusimamia sheria za haki na usawa na pia kurejesha nafasi ya dola katika kupanga maendeleo kwa mfumo wa mpango demokrasi ama dola inayojiendesha kidomokrasia kuhodhi mamlaka kusimamia na siyo kutawala mifumo ya uchumi na haki na usawa katika mgawanyo wa pato la taifa kwa kutaifisha nguzo kuu za uchumi na kuweka mikononi mwa wafanyakazi na walaji ambayo watakuwa wamejengewa uwezo kuendesha uchumi kidemokrasia na kulidemokratisha soko.

Ideolojia ya soko huria haiwezi kubadili uchumi wa Tanzania kama dola itabaki kuwa dhaifu na yenye kuegemea upande wa soko huria huku ikisimamia ukiukwaji wa haki za wazalishaji, wafanyakazi na walaji. Ideolojia ya soko huria bila ushirikishwaji wa wafanyakazi na walaji katika kupanga uchumi imeuleta uchumi wa dunia nzima na Tanzania ikijulishwa katika mwisho wake.

Migogoro ya kijamii, umaskini wa kupita kipimo, malalamiko ya watawaliwa na ugumu wa maisha umetokana na mfumo wa soko huria uliojengwa na ideolojia ya neoliberalism ambapo matajiri wamekuwa wachache na asillimia kubwa ya dunia uwezo wao wakushiriki katika uchumi umeathriwa vibaya hivyo soko huria limekwama hakuna wanunuzi maana kipato hakuna.

Katiba mpya iangalie upya dhana ya wajibu wa dola kulinda ushiriki wa kila mtanzania katika uchumi na kuchukua hatua ya kuwawezesha raia pale dola inaposhindwa kukuza uchumi na kumhahakishia kila mtanzania haki yake ya kimsingi ya kushiriki katika uchumi.

Hivyo serikali iwajibike kuwapa wananchi kipato na kuwalinda wasishuke chini ya mstari wa umaskini kwa kuwapa kipato. Kutokuwa na ajira si kosa la watawaliwa ni kosa la watawala kushindwa kukuza uchumi kwa kutokuweka mifumo dhabiti ya kukuza na kulinda uchumi na kukubali mawazo ya magharibi ambayo wao hawakuyatumia wakati walipoanza kukuza uchumi wao.

Soko huria siyo mkakati uliokuza chumi za magharibi. Ulinzi wa soko ndiyo ulizoziwezesha nchi za magahribi kujenga nguvu ya viwanda na uchumi wao wameanza kufungua masoko yao si zamani sana leo hii maajabu Tanzania inakumbatia mawazo ya kibeberu yasiyo na ukweli wowote.

Pia nina mawazo tofauti nawale wanaotaka dola ndiyo ijiingize kwenye uchumi bila ya kuwa na dola ya kidemokrasia inayokabidhii mamlaka ya kupanga na kuongoza uchumi wazalishaji, wafanyakazi na walaji. Ujamaa wetu ulishindwa kwasababu ulijitenga na wananchi;wafanyakazi na walaji na kusababisha dola kuhodhi mamlaka ya kupanga na kuongoza uchumi.

Matokeo yake tukajenga walaji, na wafanyakazi wategemezi ambao walifikiri uchumi si wao bali wa dola ndiyo maana watu wakaanza kuibia mali za umma wakififikiri wanaibia dola kumbe wanajiibia wenyewe.

Walaji na wafanyakazi wakaamua kukaa kimya watawala walipokuwa wabadhirifu malia zao wakifikiri ni za watawala, wananchi na walaji na wafanyakazi wakaanza kuabudu dola pale walipopata huduma hafifu na kila saa wakasema tunashukuzur viongozi kutafanyia hiki ama kile bila kuelewa kwamba wao ndio waliowaajiri watawala na hi watawala walibidi wawashukuru wao

2. Maadili ya kitaifa ambayo yatarudisha umoja wa kitaifa
 
Misingi ya katiba ni:
1. demokrasia shirikishi yenye viongozi na si watawala
2. umiliki wa ardhi kuwa wa wananchi
3. maliasili kumilikiwa na umma na maamuzi kufanywa na wananchi kuhusu matumizi
4. Muungano kuwa wa wazi unaohusisha serikali mbili na serikali ya shirikisho
5. kupunguzwa madaraka ya raisi na kuanzisha kamati za uteuzi likiwamo Bunge
6. uhuru wa maoni bila kuingiliwa
7. mambo mazito na ya msingi kwa nchi k.m. Muungano, matumizi ya ardhi, maliasili, mgawanyo wa nchi ktk majimbo
kupigiwa kura ya maoni
 
Wana Jamii forum tusaidiane kuishauri Tume ya Katiba Mpya ili iweke uwanja wa majadiliano katika Web ya Tanzania, na ninaomba kuuliza ni Idara gani inayoshungulikia Web ya Tanzania
 
Misingi ya katiba ni:
1. demokrasia shirikishi yenye viongozi na si watawala
2. umiliki wa ardhi kuwa wa wananchi
3. maliasili kumilikiwa na umma na maamuzi kufanywa na wananchi kuhusu matumizi
4. Muungano kuwa wa wazi unaohusisha serikali mbili na serikali ya shirikisho
5. kupunguzwa madaraka ya raisi na kuanzisha kamati za uteuzi likiwamo Bunge
6. uhuru wa maoni bila kuingiliwa
7. mambo mazito na ya msingi kwa nchi k.m. Muungano, matumizi ya ardhi, maliasili, mgawanyo wa nchi ktk majimbo
kupigiwa kura ya maoni
Ndugu zangu mnazungumzia Katiba ipi? Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo kindharia haipo au Katiba ya Tanganyika? Kama ni Katiba ya Tanganyika wengine tukae pembeni na tunyamaze. Kama ya muungano wa nchi basi tuzitafakari Katiba zote mbili, ya Tanganyika na ile y Zanzibar na baade ndio tukusanye maoni ya pande zote mbili tje na Katiba mpya ya Muungano. Tusiburuzane
 
Mambo uliyosema ni ya msingi, ila pa kusemea ni huko wanapokusanya maoni ya katiba mpya.
Kimsingi kama utayasema kule na hayatawekwa basi jamaa hawafanyi kazi inayotakiwa.
 
Kwa ujinga na kutokomaa Kidemokrasia bado Tanzania hatustahili kumpa raisi mamlaka kupitiliza.
topcombofr.jpg

John Leonard Minja

Una chuki binafsi na Ujamaa na Kujitegemea. Kwa hiyo unataka nchi yetu iwe tegemezi?
 
Back
Top Bottom