Mambo mbalimbali ya hovyo kwenye Halmashauri zetu

Nadir Naimuor

Member
Sep 13, 2020
15
15
Nitajikika kwenye halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza imekuwa kawaida sana kwa watendaji wa halmashauri nyingi kutokuwajibika na kuwatumikia wananchi wakati mkuu wa wilaya yupo mkuu wa mkoa yupo mkurugenzi wa wilaya yupo OCDVyupo OC CID yupo DSO yupo mpka Waziri au mhe Rais apite wilaya husika na kusikiliza kero na kutoa maamuzi hii sio sawa kabisa huku wilayani mhe Rais kumeoza sana sana mkurugenzi na watu wake pale halmashauri hawafai kabisa kwa mfano mmejionea wenyewe kuwa jengo la hospital la wilaya ya Sengerema linajengwa kwenye eneo ambalo halijapimwa wakati Serekali ilitoa mil mia tano (500) mwaka 2006 kwa ajili ya eneo na upimwaji. Kuna wananchi waliokuwa kwenye baadhi ya eneo hilo walipigwa pesa zao za malipo

Ukija mradi wa standi ya mabasi Sengerema ni ubabaishaji tu stand inajengwa kwa miaka sasa hakuna kinachoendelea. Njoo mradi wa maji kwenye mikutano ya siasa huongea kuwa Sengerema ilipata pesa nyingi kwenye mradi hu. Njoo kwenye huduma ya maji sasa ni hovyo sana maji wakati mwingine hukatika wiki nzima mpka wiki mbili na kubambikiziwa bili wateja na wafanyakazi wa mamlaka ya maji ni mambo ya kusikitisha sana sana umeme sasa ndo hovyo kabisa ukiwa unataka kuunganisha umeme savea kuja saiti ni mpaka umpe pesa ndo afike saiti

Kweli tunaumia sana Polisi wa Sengerema nao wamekithiri kwa rushwa wakikaa barabarani kila basi au daladala zinazofanya safari ya Sengerema Kamanga au Sengerema Busisi wakisimamisha basi unatoa elfu mbili mpaka tatu kila basi linalopita au Hiace sasa hizi ni kero ndogo tu tunaumia.
 
Kuwa specific kwa Sengerema haswa kwenye kichwa Cha habari ili uzi wako na unachotaka kukiaddress kipate Tiba ya haraka mkuu.
 
Ni kweli halmashauri nyingi zina mambo ya hivyo sana ktk kuhudumia wananchi, wakisikia kuna kiongozi wa ngazi za juu anatembelea halmashauri husika ndio utaona watendaji wanavyohaha.
 
Back
Top Bottom