Mambo mazuri yanahusishwa na Shetani, Mambo mabaya yanahusishwa na Mungu

Mwanga Lutila

JF-Expert Member
Nov 10, 2016
4,138
13,826
Leo mtu akijibidiisha akafanikiwa akawa na Pesa nyingi, midomo inaanza ahaa yule Mchawi ...alienda kwa mganga ndio akawa tajiri.

But mtu anapokuwa mzembe na kugubikwa na umaskini uliodhariri utaskia ooooh "Tumuachie Mungu" yeye ndio anajua

Au ajali ajali imetokea na watu wamejeruhiwa au hata kufa utasikia "Kazi ya Mungu"

Why mambo mazuri ya kimafanikio yanahusishwa na SHETANI na Mabaya yanahusishwa na MUNGU??

We should stop living by this nonsense philosophy.

When you are poor no one questions your poverty but the moment you get rich everyone starts questioning your wealth.
 
Pengine wana amini upendo wa Mungu kwa watu ni hafifu kuliko wa Shetani,

Ndio maana baya likimpata mtu anasema ni kazi ya Mungu.

Mfano ukikutana na mtu zezeta anayemwaga udenda hadi miguuni utasikia ni mpango wa Mungu.

Lakini sii mara moja watu wamesikia kauli kama ''Ronaldo, Messi, Rihanna au celeb yeyote akiitwa devil worshiper.

Nadhani pia ni kwa sababu watu hawaamini kama ukisali utafanikiwa maana kuna waliosali kwa zaidi ya miaka 20 au 30 lakini maisha yao yapo vile vile.
Lakini ukiwachunguza watu wa namna hiyo utagundua kwamba wengi ni wale walio opt kutumia imani badala ya kufikiri wafanyapo jambo lolote kwenye maisha yao sababu imani inapeleka majukumu kwingine.....Kwahiyo kuamini ni kukwepa majukumu.

Wanapokuja kupima matokeo ya mwaamini na mfikiriaji, wanao amini hujikuta wamepigwa gap na hapo ndo wivu huanzia kwa kuwaita wengine ni waabudu Shetani.
 
Siku hizi Mungu anasingiziwa sana, eti Mungu ndo katupa .......... atuongoze.
 
Duh Ndio mana mungu kajificha.
Mvivu yeyote yule hudingizia mungu hajapanga mara hoo haikuwa lizki na akipata anatumia mpka amalize ndipo anaanza tena kutafuta.
Akiona kuna mwenzie anabidii na juhudi kuliko yeye mara moja huanza kumtafutia sababu ooh yule kaenda kwa mganga yule muabudu shetani.
 
Pengine wana amini upendo wa Mungu kwa watu ni hafifu kuliko wa Shetani,

Ndio maana baya likimpata mtu anasema ni kazi ya Mungu.

Mfano ukikutana na mtu zezeta anayemwaga udenda hadi miguuni utasikia ni mpango wa Mungu.

Lakini sii mara moja watu wamesikia kauli kama ''Ronaldo, Messi, Rihanna au celeb yeyote akiitwa devil worshiper.

Nadhani pia ni kwa sababu watu hawaamini kama ukisali utafanikiwa maana kuna waliosali kwa zaidi ya miaka 20 au 30 lakini maisha yao yapo vile vile.
Lakini ukiwachunguza watu wa namna hiyo utagundua kwamba wengi ni wale walio opt kutumia imani badala ya kufikiri wafanyapo jambo lolote kwenye maisha yao sababu imani inapeleka majukumu kwingine.....Kwahiyo kuamini ni kukwepa majukumu.

Wanapokuja kupima matokeo ya mwaamini na mfikiriaji, wanao amini hujikuta wamepigwa gap na hapo ndo wivu huanzia kwa kuwaita wengine ni waabudu Shetani.
mambo yote huanza na imani.
Imani - ni uhakika wa kitu kisichokuwepo.
Wakina columbus waliamini wanaweza kusafiri na kurudi hata kabla ya safari yenyewe.
Tatizo wengi wanaojiita wanaimani ni wanafiki maisha yao sirini ni reciprocal na maneno yao.
Inahitaji imani kuwa inawezekana ili vitu visivyowezekana viwezekane.
Faith in action == experiments and findings
 
Huwezi kuizuia jamii kuhoji, maana yote yanawezekana mtu kuwa tajiri kwa nguvu za Giza au Mungu. Na pia kuwa maskini wa kutupwa sababu ya shetani au Mungu.
 
mambo yote huanza na imani.
Imani - ni uhakika wa kitu kisichokuwepo.
Wakina columbus waliamini wanaweza kusafiri na kurudi hata kabla ya safari yenyewe.
Tatizo wengi wanaojiita wanaimani ni wanafiki maisha yao sirini ni reciprocal na maneno yao.
Inahitaji imani kuwa inawezekana ili vitu visivyowezekana viwezekane.
Faith in action == experiments and findings
Imani kwa jinsi ilivyo haina shida bali kwa jinsi inavyokuwa effected.
Imani ya Columbus iliegemea juu ya uelewa wake wa dunia, bahari na navigational skills zake.....Tofauti ni imani kwa Mungu au Shetani ambazo hazieleweki na hazina uthibitisho wowote.

Kusema kwamba mwamini hafanikiwi sababu ya matendo yake ni kisingizio cha kushindwa tu.
 
Ukwasi ni uwanja wa kujidai shetani, ukiwa nao kina masogange na sepetu watakubinukia kwa kadri utakavyowaelekeza, mara nyingi kama sio zote utatumia kwa vitu chukizo kwa waaminio uwepo wa Mungu.
Sasa ukiwa nazo huwi umejika joho la shetani?

Usipokuwa na ukwasi hutacheza midundo ya shetani. Ni rahisi kumtafakari Mungu ukamuelewa kwa uzuri ukiwa masikini. Hutatamani kumpa rushwa ili uishi milele, hutatamani kumpa lifti Mungu kwenye Range Rover yako. HUTAMKUFURU ROHO MTAKATIFU. (kama alivyofanya makonda kwenye hotuba yake ya maigizo ya mpambano wa madawa ya kulevya eti....... Anawashindia vita hii)
 
Leo mtu akijibidiisha akafanikiwa akawa na Pesa nyingi, midomo inaanza ahaa yule Mchawi ...alienda kwa mganga ndio akawa tajiri.

But mtu anapokuwa mzembe na kugubikwa na umaskini uliodhariri utaskia ooooh "Tumuachie Mungu" yeye ndio anajua

Au ajali ajali imetokea na watu wamejeruhiwa au hata kufa utasikia "Kazi ya Mungu"

Why mambo mazuri ya kimafanikio yanahusishwa na SHETANI na Mabaya yanahusishwa na MUNGU??

We should stop living by this nonsense philosophy.

When you are poor no one questions your poverty but the moment you get rich everyone starts questioning your wealth.
Umasikin ni laana bro. Mungu alipomaliza kuumba alisema vyote ni vyema akimaanisha kila kitu kwa asili kimewekewa tayar baraka mbele.
 
Mungu hakumuumba mtu yeyote awe maskini. Kila mtu ana kipawa alichopewa na Mungu ili kimfanye asiwe maskini. Tatizo watu wengi sana hawajui wala kutumia vipawa vyao kuondokana na umasikini. Shetani ndiye anayeharibu maisha ya watu (kupitia mawakala wake kama wachawi, waganga n.k.) Hata vifo vingi si amri ya Mungu bali ni mpango wa shetani unaofanikiwa kwa sababu mtu amekosa ulinzi wa Mungu. Utajiri wowote kutoka kwa shetani unapatikana kwa umwagaji damu. Na hao wanaomwaga damu hivyo mwisho wao ni mbaya
 
linganisha na hii.."..UKIOMBA BAYA LITATOKEA MAPEMA NA UKIOMBA ZURI LITACHELEWA.."...tafakari...
 
Unajua mchakato wa kutafuta mafanikio mpaka kujakuyapata ni mgumu sana wengi wanaishia njiani na wengine hawaoni hata pakuanzia.. Inapotokea mtu kafanikiwa mwingine inamshitua sana tena sana sana maskini ndio wanasemaga amenda kwa Mganga... Yani ukifanikiwa huwashitui wenye mafanikio unawashitua wasio na mafanikio kwa kias kikubwa sasa kutokana na mshtuko wanaanza ku reason mambo mbali mbali kama ka defence flan
 
Pengine wana amini upendo wa Mungu kwa watu ni hafifu kuliko wa Shetani,

Ndio maana baya likimpata mtu anasema ni kazi ya Mungu.

Mfano ukikutana na mtu zezeta anayemwaga udenda hadi miguuni utasikia ni mpango wa Mungu.

Lakini sii mara moja watu wamesikia kauli kama ''Ronaldo, Messi, Rihanna au celeb yeyote akiitwa devil worshiper.

Nadhani pia ni kwa sababu watu hawaamini kama ukisali utafanikiwa maana kuna waliosali kwa zaidi ya miaka 20 au 30 lakini maisha yao yapo vile vile.
Lakini ukiwachunguza watu wa namna hiyo utagundua kwamba wengi ni wale walio opt kutumia imani badala ya kufikiri wafanyapo jambo lolote kwenye maisha yao sababu imani inapeleka majukumu kwingine.....Kwahiyo kuamini ni kukwepa majukumu.

Wanapokuja kupima matokeo ya mwaamini na mfikiriaji, wanao amini hujikuta wamepigwa gap na hapo ndo wivu huanzia kwa kuwaita wengine ni waabudu Shetani.
Post of the day! Imekaa vizuri sana kwa tafakuri.
 
Back
Top Bottom