Mambo matano ya kipekee kwenye apple watch

Mambo matano ya kipekee kwenye apple watch

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159

Hatimae baada ya miaka miwli na ushee Apple wametoa saa ya smart. Saa hii sio tu itaimarisha mauzo ya iPhone bali pia inakuwa ni gajeti ya kwanza ya aina mpya kutolewa na Apple tangu Tim Cook kuwa Afisa Mtendaji mkuu wa Apple kufuatia kifo cha liyekuwa mwanzilishi wa kampuni hiyo Steve Jobs.

Apple wamechelewa sana katika uwanja huu, hasa ukizingatia kampuni kama vile Samsung wameshatoa saa zaidi ya tano, huku Sony wakitangaza saa yao ya tatu itayoingia mauzoni mwezi ujao. Swali la msingi la kujiuliza ni kitu gani kitakachoifanya Apple Watch iwe ya namna ya kipekee? Tutazungumzia mambo matano muhimu.

Kioo

Apple Watch inakuwa saa aina ya smart ya kwanza kutumia kioo cha sapphire ambacho hakiathiriki na kupindwa (flexible).

Kioo hichi kina umadhubuti wa hali ya juu Apple wametumia vilivyo uwezo wa kioo hichi kupinga kwa kuweka amri za "touch" na "tap" katika namna ile ile kifungo (home button) cha iPhone 6 na 6 Plus kinavyoweza kupokea amri za tap na touch na kutoa matokeo tofauti. Mtindo huu inaifanya Apple Watch kuwa saa ya kwanza yenye sifa hii.


Crown Jewel
Huu ni ufunguo wa kuzungusha wa saa kama funguo za kawaida lakini Apple wameufanya ufunguo huu wa ki-dijitali. Tunathubutu kusema kwamba hii ndio sifa kuu yenye kuvutia kwenye saa hii. Apple huwa kila wanapotoa gajeti aina mpya hutoa UI ya aina yake, Mouse ilianza na Macintosh, Wheel ilianza na iPod,
Touch screen ilikuja na iPhone hivyo Crown Jewel ndio ingizo jipya katika UI ya saa. Hii unaweza kuitumia mathalani ku-zoom, kubadili menu, ku-click na kadhalika.

Pia hutumika kwa kuzungusha na kubonyeza. Iwapo unahitaji kutumia saa hii bila ya kutumia kioo ili kuepuka kuzinga unachohitaji kukiona kwenye kioo, Crown Jewel itarahisisha kazi yako.


Mtindo (Design)

Apple wametoa saa zenye aina mbili katika tofauti kwa ukubwa. Kubwa ikiwa na 24 mm na ndogo ina 38 mm. Zote unaweza kuzibadili kuvaa ama mkono wa kulia au wa kushoto. Pia kwa upande wa matoleo, Apple wametoa matoleo matatu tofauti, Apple Watch, Apple Watch Sport na Apple Watch Edition.

Apple Watch Edition ni ya dhahabu halisi yenye kareti 18, bila ya shaka hii itakuwa ndio ghali kuliko zote. Hii ni kwa wale wanaohitaji kuvaa saa kwa ajili ya"kupata heshima zaidi".


Apple Watch Sport imetengenezwa kwa anodised aluminium ambayo Apple wanadai ina umadhubuti wa 60% zaidi kuliko alloy na ni nyepesi kwa 30% zaidi kuliko steel.

Bila ya shaka hili ni chaguo bora kwa wanamichezo hasa unapoweka mkanda wa plastiki (sports band) ili kupunguza uzito zaidi. Huna haja ya kuwa na wasi wasi wa kuvunjika unapokuwa mchezoni ukizingatia kwamba kioo chake ni Sapphire.


Nayo Apple Watch imetengenezwa kwa Stainless Steel huku ikiwa na aina tatu za mikanda tofauti , mkanda wa ngozi, mkanda wa steel na milanese loop.

Tunaamini kwamba hii ndio itakuwa chaguo la wengi na pia ndio itakayokuwa rahisi kwa bei, ukizingatia kwamba saa hizi zitauzwa kuanzia $350.00 hata ya rahisi haitokuwa rahisi.


Hivyo ukiunganisha aina mbili za ukubwa, aina tatu za mikanda na aina tatu za matoleo, kutakuwa na jumla ya Apple Watch aina kumi na nane tofauti. Bila shaka kila mmoja atapata kile ambacho anakipenda yeye katika aina kumi na nane hizi.


Apple Pay


Ni lazima tukiri kuwa Apple wametoa funzo kwa Google na Samsung juu ya jinsi ya kutekeleza malipo kwa kutumia teknolojia ya NFC, baada ya Google Wallet na Samsung Wallet kufeli vibaya, Apple tayari wameshaingia mkataba na mabenki na watoa kadi bali mbali kama vile Barclyacard, Capital One, Citi na Bank of America, pia maduka makubwa, supermarket na wauzaji wengine kushiriki katika malipo haya. Kuna maduka 220,00 tayari yamekubali kushiriki kwenye Apple Pay.


Na vile vile Apple Pay itakuwa kwenye simu na saa ambapo, Apple ndio wa kwanza kufanya ubunifu wa aina hii.

Gajetek tunatabiri itachukua chini ya miaka 5 Apple Pay kuwa maarufu kuliko Paypal kwa namna nyingi, hasa ukizingatia mpaka leo Payplal hutumika zaidi mtandaoni tu, ingawa ni muda mrefu tangu Paypal waanze juhudi za kutaka malipo yao yafanyike hata kwenye matumizi ya kawaida, lakini juhudi hizo bado zimegonga ukuta.



Matumizi
Saa hii haitakuwa inatumika peke yake, ingawa imewekewa bluetooth, akselerometa, gyroscope na kipima mapigo ya moyo, mtumiaji wa saa hii lazima awe na iPhone ambapo kuanzia iPhone 5 kwenda mbele zote zitakuwa zinafanya kazi na saa.

Apple Watch itaitegemea iPhone kwenye GPS, na pia itapokea taarifa (notification) mbali mbali kutoka kwenye iPhone. Saa hii haina port za kawaida, chaji yake itakuwa inaingia kwa kutumia circular magsafe connector, hivyo hii inaingia katika kundi la wireless charging.

Tunaamini apps zitamiminika kwa kasi kubwa kwenye saa kutokana na wingi wa watengeneza apps huvutika na soko la Apple.



Ingawa Apple wamechelwa mno katika uwanja huu, bado wameweza kuleta mabadiliko makubwa, hasa katika Apple Pay, Kioo cha Sapphire na mitindo mbali mbali katika saa hivyo kuanzia mkanda, ukubwa na hata malighali ya kutengenezea.

Kikubwa zaidi saa hiyo itatoka ikiwa na Apps nyingi tayari ikiwa ni pamoja na ramani, lakini tunaamini kwa vile hili ni toleo la kwanza bado kutakuwa na uboreshwaji mkubwa wa saa hii hapo miaka ya baadae kwenye toleo la pili kwenda mbele.

Hatuna budi kusema kwamba Apple wameanza vizuri mno katika uwanja wa smartwatch. Ukweli zaidi utajitokeza wakati saa hizo zitakapoingia madukani hapo mwanzoni mwa mwaka ujao.

Chanzo:gajetek.com

 
6- itakua inahitaji daily charge kwa matumiz ya kawaida. kila siku before hujalala make sure unaiweka near device yake for wireless charging. hilarious.
 
6- itakua inahitaji daily charge kwa matumiz ya kawaida. kila siku before hujalala make sure unaiweka near device yake for wireless charging. hilarious.

Mi naona Android zote zinahitaji kuchajiwa daily kama inayumika siku nzima,
 
6- itakua inahitaji daily charge kwa matumiz ya kawaida. kila siku before hujalala make sure unaiweka near device yake for wireless charging. hilarious.
Sony Smartwatches - Daily charging
Samsung Gear Watch - Daily Charging
LG G Watch - Daily Charging

Pebble Watch - Weekly charging (roughly) - Ubovu wake hii haina touch screen, mbaya zaidi inatumia monochrome e paper display, rangi haina. That is the sacrifice you need to make kuepuka kuchaji kila siku.

The new Samsung Gear S Samsung inachukua siku mbili, well ina ukubwa wa 2" na pana, hivyo if you are ready for this giant on the wrist then yes you will alternate days between charging.
 
Mi naona Android zote zinahitaji kuchajiwa daily kama inayumika siku nzima,

pebble hauchaji kila siku si android si iwatch lakini unatumia na os zote.

saa zao zinakaa na chaji wiki nzima ila sababu si kampuni kubwa(ni kickstart project) hamna anaewatangaza, kila mtu galaxy gear na iwatch.
 
pebble hauchaji kila siku si android si iwatch lakini unatumia na os zote.

saa zao zinakaa na chaji wiki nzima ila sababu si kampuni kubwa(ni kickstart project) hamna anaewatangaza, kila mtu galaxy gear na iwatch.
hapo umesem ukwel mkuu.
 
In my opinion I think wireless charging of Apple watch will wear off the phone battery in a short period of time. Not practically proven for now but I guess that's what it will be.
Unless there is any evidence to prove otherwise
 
Back
Top Bottom