Mambo machache niliyoyaona kwa tingatinga

Mambo machache niliyoyaona kwa tingatinga

H20

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2013
Posts
341
Reaction score
170
Tumeona kampeni kwa vyama vya siasa kwa muda wa mwezi mmoja na ushee. Bado siku chache uchaguzi ufanyike tumpate rais wa JMT. Mambo machache niliyoyaona kwa tingatinga na mengine niliyokuwa nayafahamu.

1. Uuungwana kwa maneno: Amekuwa anatumia lugha ya staha bila kuwatukana wapinzani wake

2. Vitendo visivyo vya kiungwana: Dhihaka ya afya ya mwenzako kwa kupiga push up ni ishara ya kukosa uungwana
kwa vitendo. Waungwana husema haja ya mja hunena, muungwana ni vitendo. Kama vitendo vyako si vya kiungwana
ni dhahiri kabisa hata namba moja hapo juu inafutika.

3. Kukosa dira...... Ukiwa kama kiongozi mtarajiwa wa nchi, kwenye kampeni badala ya kuwa inovative kwenye mambo ya kuwavutia wasikilizaji wako, unacopy n paste za wapinzani wako ni kukosa dira na tunapata hofu ya kuwa na raisi asiye na uwezo wa kutupeleka mbele.

4. Kukurupuka. Ikiwa unaweza kumtaja mtu hadharani kwamba anakuhujumu bila kuwa na uhakika na baadaye
kubadilisha jina na kwenda kumkumbatia ni ishara mbaya sana kwa kiongozi unayetarajia kushika madaraka yaa juu kabisa na tena kuwa amiri jeshi mkuu. Hii inatuonesha kuwa tabia ya kukurupuka imo nawe na hivyo kutupa mashaka. Hata kote ulipopita ulikuwa unakurupuka kwa kutoa maamuzi yasiyo na tija mfano uvunjwaji wa nyumba za watu na kauli nyingine za chuki mfano ulipowaambia wa kigamboni wakikosa pesa ya kivuko wapige mbizi.

5. Uwelewa wa mambo. Inaonekana mambo ya kidiplomasia na siasa za nje ya nchi yako huyajui kabisa, yaani uwelewa wako uko kwenye mambo ya ujenzi tu? vipi afya, elimu, biashara, uchumi, kilimo nk? Hata hujui watu maarufu kama Ghadafi na Saddam walikuwa wa nchi gani? Je unamfaha Xi Jinping? Obama ni rais wa ngapi wa Marekani? Vipi sera za nje za Tanzania? Unahitaji kuwa global na up to date. Sio mabarabara tu.

Haiwezekani wewe ni mjumbe wa baraza la mawaziri hujui wamachinga na mama lishe wananyanyaswa, tembo wanauliwa na mhusika mkuu ni katibu mkuu wako, twiga kutoroshwa, mishahara hewa, hospitali kukosa dawa na mambo mengine mengi ambayo yanaonekana kukushangaza. Sasa ikiwa uko huko kwenye serikali kwa miaka 20 mfululizo huelewi mambo unahitaji miaka 10 kujifunza au kufanya nini? Unatia shaka mheshimiwa ni bora ukae kimya kuliko kushangaa.

Na hayo yote unavyoyafanya unakurupuka kabisa kama yule BRAZA K wa FUTUHI.
 
Back
Top Bottom