Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,059
- 79,412
MAMBO AMBAYO YATAKUFANYA UWE A BROKE MAN (MWANAUME ALIYEFELI).
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Kuna mambo ukifanya unauhakika WA kujikuta kuwa miongoni mwa wanaume waliofeli, walioshindwa ndio Broke Man.
Mwanaume aliyefeli ni mwanaume ambaye Kwanza Kabisa Hana uwezo wa kujisimamia na kujitunza yeye mwenyewe.
Kula vizuri, kuvaa vizuri na sehemu ya Kulala.
Pili, Mwanaume ambaye watu wanakudharau kutokana na kuwa huna sifa za kuwa Mwanaume, kama kujisimamia, kujitegemea, Msimamo na utambuzi.
Tatu, mwanaume ambaye sio Mwanaume unayesimamia kile unachokiongea, yaani unajiongeza vitu ambavyo hujui hata ilikuwaje ukatamka. Ni kwamba huwezi kujidhibiti.
Sitaki kukuchosha, yafuatayo ni mambo ambayo Mwanaume ukiyafanya unajiweka kwenye mazingira ya kuwa Mwanaume aliyefeli, mwanaume aliyeshindwa, aliyevunjika alimaarufu A Broke Man.
1. Kukimbizana na Wanawake badala ya Kutafuta Fursa na kujijenga kiuchumi
Muda wote unafikiri kutongoza tongoza wanawake.
Muda wote unakimbizana na wanawake.
Uhakika ni kuwa ni nadra Sana kukimbizana na Wanawake na hapohapo ukawa mwanaume mwenye kipato kinachoeleweka.
Kwanza kukimbizana na Wanawake ni Moja ya dalili kuwa wewe ni Broke Man.
Kikawaida Broke Man ndiye anakimbizana na wanawake.
Wanawake ndio hutakiwa kukukimbiza wewe kukuwaza wewe, kutumia Muda wao mwingi kutaka uwe nao.
Na ili Wanawake wakukimbilie ni lazima uwe mwanaume Halisi, mwanaume mwenye nguvu.
Nguvu ya Akili, nguvu ya mvuto(umaarufu), nguvu ya kipato.
Nguvu ya Mamlaka au cheo.
Kadiri unavyokosa Muda na wanawake ndivyo upo kwenye Nafasi nzuri ya kufanikiwa. Na kadiri unavyokimbizana na wanawake tayari upo kwenye anguko.
Acha Umalaya, kama kuna ulazima Sana tafuta mwanamke Mmoja ambaye atakusikiliza na kukuheshimu kama hayupo Baki pekeako. Nunua Makahaba angalau mara mbili kwa mwezi.
2. UVIVU
Uvivu wa mwili na AKILI.
Unasema hakuna Kazi wakati Kazi zipo. Ajira ndio hakuna. Huo ni uvivu wa mwili na AKILI.
Kupenda visingizio huo ni uvivu wa mwili na AKILI.
Kutapeliwa na waganga na Manabii Fake huo ni uvivu wa Akili.
Kupenda kitonga na kutegemea watu huo ni uvivu.
Mwanaume mzima, hauumwi, unaafya Tele Kazi kutegemea vizinga au washikaji. Huo ni uvivu.
Mbona Watibeli Sisi ni mahandsome Boy na Kazi ngumu tunafanya?
Tunatembeza karanga, tunauza nguo za mitumba, tunauza Dagaa, tunafanya udalali, tunafanya uwinga. Kwako kipi ni spesho mpaka hautaki kufanya Kazi ili ujitegemee mwenyewe?
Kama ni kusoma Sisi tumesoma, kama ni kufaulu tulifaulu kwa viwango vya DARAJA la juu kabisa, lakini tunafanya Kazi yoyote halali.
Kijana, maisha ni mindsets, Kazi ni Kazi. Acha uvivu.
Kama ni kumtegemea na kumwomba Mungu hata Sisi Watibeli tunafanya hivyo na hatujisikii vibaya kwa maisha tuliyonayo bila kujali wengine watayatafsiri kwa namna Yao kuwa ni magumu au mazuri. Bila kujali kipato ni cha namna gani.
Muhimu tunafanya Kazi, hatuwi Mzigo kwa yeyote. Tunalisha familia zetu. Na huo ndio uanaume.
Kijana, Acha kuwaza Mawazo ya tamaa, kujilinganisha, kuishi Mawazo ya watu wengine kwamba watakudharau. Hiyo ni dhana potofu.
Fanya Kazi yoyote iliyokatika mazingira yako iliyohalali. Jitegemee na tunza familia yako. Full stop.
Huwezi kuwa Mwanaume aliyefeli kama sio mvivu. Hubagui Kazi(hunadharau). Tabia ya kudharau Kazi ni mbaya Sana.
3. KUWA MWOGA (KUTOKUTHUBUTU)
Wewe ni mwanaume. Acha uoga.
Hivi unaogopaje kufanya Jambo ambalo sio kosa kisheria Wala sio dhambi? Hivi uliwahi kujiuliza?
Unaogopa kujitegemea? Unaogopa kuanza Maisha ya pekeako?
Unajiuliza itakuwaje? Je ukishindwa? Kwa nini usiwaze je ukiweza?
Huna sababu hata Moja ya kuogopa kujaribu. Jaribu kufanya Jambo hata mara Mia Moja. Usiogope kushindwa.
Mtu anayejifunza Jambo hashindwi Bali yupo kwenye mafunzo.
Mbinu za kutokuwa MWOGA;
a) Jitambue.
Jua nguvu na udhaifu wako. Jua thamani yako. Jua wajibu na majukumu yako. Jua mipaka yako. Jua malengo yako.
b) tafuta maarifa na Elimu
Ni kweli unaakili lakini lazima utafute Elimu, maarifa na ufahamu wa mambo Mbalimbali. Elimu na maarifa hayo lazima yawe sahihi.
Kadiri unavyopata maarifa ndivyo Hofu na woga vinavyozidi kupungua.
c) Tafuta Uhuru(jitegemee)
Ukishajitambua, kisha ukapata maarifa na Elimu automatically utaona umuhimu wa kuwa HURU. Kujitegemea kiakili, Kihisia, Kimwili na kiroho. Hapa uchumi utahusika.
Elimu na maarifa itakusaidia Kupata Uhuru sahihi na Kuishi maisha mazuri.
Uhuru wa Kweli.
Utambua umuhimu wa Uhuru wako, kujua mipaka ya Uhuru wako na mipaka ya Uhuru wa watu wengine wanaokuzunguka.
d) Kutambua watu na mazingira yanayokuzunguka.
Watu wengi ni waoga wa kuthubutu kwa Sababu hawajitambui na kama wanajitambua Basi hawatambui mazingira na watu wengine wanaowazunguka.
Kuwajua watu vizuri ni kusema kutowaogopa.
Lazima ujifunze Saikolojia ya Watu na viumbe. Uielewe.
Huwezi kuogopa watu unaowafahamu, huwezi kuogopa mazingira unayoyajua.
Ukiwa MWOGA kwa maana ya kushindwa kuthubutu (to take Risk) unajiweka kwenye mazingira ya kushindwa na kuwa Broke Man.
4. Kuendeshwa na Mihemko
Wewe ni mwanaume. Hupaswi kuendeshwa na hisia zako.
Kuendeshwa na Mihemko ni kuruhusu wengine wakutawale, wakuendeshe.
Unahasira za kijingajinga kama mtoto wakike. Unaudhika hovyohovyo kama lijinga. Unasusa hovyohovyo kama Mtu usiyeweza kujidhibiti.
Unapigana hovyohovyo kama mpumbavu.
Waliosema hasira hukaa vifuani mwa wapumbavu ni kweli asilimia 100.
Mihemko yako ya kijinga itakufanya ushindwe kila kitu.
Mihemko itakufanya ushindwe kwenye;
a) mahusiano kazini au kwenye biashara.
Unabishana na wateja, mara unatukanana nao. Tumia AKILI. Unajibizana na maboss wako mwishowe unafukuzwa Kazi. Tumia AKILI boya wewe
b) Utafeli kwenye Mahusiano ya ndoa na Familia.
Ndoa na familia ni taasisi. Taasisi haziongozwi na Mihemko yako kenge wewe. Taasisi yoyote inayoingozwa na Mihemko inaanguka. Taasisi inamiongozo, Sheria na Kanuni.
Wekeni Sheria, miongozo na Kanuni ambayo mtairejelea inapoibuka migogoro.
Sio kitu kidogo mnapigana kama majingajinga.
Kitu kidogo mnatukanana kama wehu.
Mtavunja nyumba wajinga nyie.
Mwishowe utakuwa broke man na mwanamke utakuwa Broke woman.
Ukishajua umekasirika usifanye maamuzi. Hiyo ni Akili na itachukuliwa unauwezo wa kudhibiti Mihemko yako.
Subiri hisia zako zishuke, urudi kwenye Hali ya kawaida kisha jadilianeni mpate ufumbuzi. Hakikisha miongozo, Kanuni na Sheria zinafuatwa.
Kanuni na miongozo na Sheria lazima ziwe na HAKI, KWELI na AKILI na upendo.
5. Huna Maono, malengo na mikakati.
Mwanaume kuitwa kichwa ni kumaanisha wewe ndiye Mbeba Maono ya familia unayoenda kuianzisha.
Lazima uwe na Maono, malengo na mikakati.
Bila kujali upo katika Hali gani.
Mafanikio ya Mtu yapo kwenye Maono yake. Maono ya Mtu yapo kwenye Akili yake.
Niliwahi kusema, macho hayaoni kinachoona ni Akili (Ubongo). Ukiyaruhusu macho yaone na kuacha ubongo uone umeshafeli.
Kwa sababu macho hayana uwezo wa kuona Kesho na Kesho kutwa. Macho yanaona Leo tuu. Lakini Ubongo(Akili) unauwezo wa kuona Miaka Mia ijayo.
Kuona future ndio MAONO yenyewe.
Macho ya sasa yataona wewe huna lolote lakini Ubongo wako unaweza kuona unalolote au hauna lolote.
Ni suala la uchaguzi tuu kwamba unataka kuona nini.
Watu kama Rais Samia Suluhu kama ungemuuliza Miaka 30 iliyopita macho yake yalikuwa yanaona hapa alipo atakuambia kwa kweli Hapana. Ila Akili na Ubongo wake huenda viliwahi kufika hapa alipo.
Maono Chanya huunda mtazamo Chanya.
Mtazamo ni nini?
Mtazamo ni kile unachozungumza, unachotaka kukiona kwenye maisha yako, vile maisha unavyoyachukulia na kuamini.
Mtazamo ndio huamua future yako iweje.
Usipokuwa na Maono unakuwa kama Kipofu wa nafsi. Hujui wapi unaenda na hujui nini unataka kwenye maisha yako.
Ndugu yangu, nimeandika Sana na sitaki uchoke. Kwa Leo itoshe kusema, usikubali kuwa mtu aliyeshindwa, aliyefeli.
Mimi acha nipumzike sasa.
Robert Heriel
Taikon Master
Kwa sasa Dar es salaam