Kanyegelo, mada yako ni nzuri ila hapo unapo-generalize kwa kusema nyumba au kiwanja ni Assets hapo inategemeana na matumizi ya hizo mali.
Asset ni mali/kitu ambacho kinakuingizia kipato,, sasa kama umejenga/kumiliki nyumba kwa kuishi wewe mwenyewe basi hio nyumba ni LIABILITY kwasababu haikuingizii pesa yoyote isipokuwa itakuwa inakukamua hela kwa maintanance& repairing, kulipia kodi ya majengo nk, so haitokuwa tofauti na kumiliki gari la kutembelea cuz nalo linahitaji huduma za repairing, bima, wese kila liwapo road.
Ila kama utajenga nyumba kwa matumizi yoyote ya kibiashara kama kupangisha, hotel, lodge etc basi hio nyumba ni Asset kwasababu itakuingizia kipato.
Kwa kumalizia tu, ASSET ni mali/ kitu chochote kinachopelekea wewe mmiliki kuingiza kipato wakati LIABILITY ni mali/vitu vinavyonyonya pato lako!!!