Mambo ambayo hutakiwi kufanya ukiwa unaendesha gari la Manual

Joseverest

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
52,526
70,671
Pale unapoendesha gari ya manual ile gear lever inawezekana ikawa kama kitu kigumu kwako, lakini unapoizoea ni kitu cha kufurahisha na starehe kucheza nacho hasa unapokuwa barabarani. Kuna baadhi ya mambo ya kuzingitia kabla au hata baada ya kujua kuendesha gari ya manual ili kujiweka salama barabarani na kukilinda chombo chako.

1. Kamwe usitumie gear lever kama egesho la mkono wako

Tunaiona gear lever na kuitumia bila kujua nini kinafanyika nyuma ya pazia. Pale tunapotumia gear lever kubadilisha gear, selector fork ambayo huwa haizunguki huwa inakandamizwa kwenye collar inayozunguka na ile collar huwa inagandamizwa kwenye gear plate unayotaka kubadilisha. Kuweka mkono kwenye gear lever kwa muda mrefu kunasababisha kusagika kwa ile selector fork taratibu na kupunguza urefu wa maisha yake.

2. Usikanyage Clutch wakati gari linapoteremka katika mteremko ili kuongeza mwendo

Kukanyaga clutch wakati gari linateremka kwa kasi mteremkoni sio jambo la kufanya wakati unaendesha gari la manual. Hii itachangia sana kusaga baadhi ya maeneo katika mfumo wa gear wa gari lako. Pia itapelekea gari lako kukosa balance wakati wa kushuka katika mteremko. Cha kuzingatia ni makadirio ya mwendokasi, gear uliyopo na muda wa kuachia clutch husika.

3. Usiweke mguu wako muda wote juu ya pedeli ya Clutch

Kuweka mguu wako muda wote kwenye pedeli ya clutch kutaifanya clutch yako kuengage partially na kusababisha kutereza kwa clutch kila mara. Hii inapelekea kusagika kwa clutch na muda mwingine kunapelekea kupoteza kiasi kikubwa cha mafuta kwa sababu ya kupoteza transimission energy kubwa.

4. Usikanyage Pedeli ya Accelerator mpaka mwisho pale unapokuwa kwenye gear ndogo

Kukanyaga pedeli ya Accelerator (mafuta) mpaka mwisho pale gari lako linapokuwa katika mwendo mdogo sio vizuri kwa sababu kutapelekea kutumia kiasi kikubwa cha mafuta bila sababu. Unashauriwa kukanyaga pedeli yako ya mafuta mpaka mwisho pale tu unapokuwa katika gear za kasi ili kulifanya gari lako litembee katika mwendokasi mkubwa.

5. Usibadili Gear bila kukanyaga clutch

Clutch inasaidia kutenganisha injini na gear box kila muda inapokanyagwa. Ni muhimu kukanyaga clutch kwanza kabla ya kujaribu kubadili gear yoyote ili kuipa maisha marefu gear box yako. Clutch Unit hutumika kusafirisha mzunguko wa injini kutoka kwenye injini kwenda kwenye transmission.

6. Usibane brake wakati wa kusimama bila ya kukanyaga Clutch

Wakati unapotaka kusimama ni muhimu sana kukanyaga clutch. Cha kuzingatia hapa ni muda wa kubana clutch, jaribu kupunguza mwendo mpaka pale unapoona sasa unahitaji kusimama na hapo unaruhisiwa kukanyaga clutch na kulifanya gari lako kusimama.

Kumbuka Clutch ni kila kitu linapokuja suala la gari za manual, hakikisha umepata mafunzo ya kutosha kabla ya kuanza kutumia gari la manual katika barabara kuu.

Credits: swahilitech.com
 
We mtoa post inaonekana ujawaienesha gari umbali mrefu pia umeendesha hizi gari auto hyo Namba (1 ) gari kama Faw na Howo au lori za kichina n pasua kichwa mda wote mkono upo kwenye gear Lever ahaaaaaa ahaa hyo namba (5) baba angu hzo gari nimetaja kuna gia inabid tu uskizie RPM unakanyagia tu bila clutch ukisema utie gia zote 12 ndugu yangu mguu 1 utakua ka Mua mwingine ka mgomba ingawa walioeleza yote ndo utaratibu ila kiukweli kuna mambo inabidi uachane nayo safari ufike. Imargin safari ya 2000+ KMs
 
Ahaa kumbe...mi nimezoea haya magari madogo tu..sasa magari kama FAW na HOWO...MMMH Ngoma nzito ile aisee
 
Ahaa kumbe...mi nimezoea haya magari madogo tu..sasa magari kama FAW na HOWO...MMMH Ngoma nzito ile aisee

Hayo wanakuambia kungoa mihogo clutch jiwe acceletor jiwe af kila mahali road ni tuta punguza ongeza lazma gia utumie RPM kuingiza la sivo ukisimama mahala miguu yote inauma mkono unauma acha kabisa jamaa wana pata tabu sana
 
Yeah...ndio maaan niliwahi kusikia kuwa hawa madereva wanaoendesha magari makubwa wanapata tabu safari ni na kuchoka...kumbe ndio maana
 
Yeah...ndio maaan niliwahi kusikia kuwa hawa madereva wanaoendesha magari makubwa wanapata tabu safari ni na kuchoka...kumbe ndio maana

Chinese trucks ndio zina majanga hayo ila hizi za ulaya siku izi zote ni automatic kiti full upepo AC af booster za kutosha kwnye cabin kwahyo kuchoka si saana kma hzo za kichina viti ka umekalia Stuli no AC humo
 
Kama wale SCANIA wapo vizuri kweli
 
Iwe scania volvo benz daf Renault na mengineyo yako hvo
Yeah hizi European brands hawataki kabisa mchezo mchezo..wanaboresha ili kukidhi mahitaji ya soko kubwa...

BTW hizi kampuni za Europa si ndio zinaongoza mauzo kuliko hizo za china? au siko sawa?
 
Yeah hizi European brands hawataki kabisa mchezo mchezo..wanaboresha ili kukidhi mahitaji ya soko kubwa...

BTW hizi kampuni za Europa si ndio zinaongoza mauzo kuliko hizo za china? au siko sawa?

Chinese anaweza kua anauza tu hapo kwenu mana ndio jalala la kila takataka hata yeye kwao anatumia europe trucks sio takataka zake hzo.
 
Kaongea ukweli kabisa ila kaongelea gari tani 3 kushuka chini aje kwenye beiben 2528 au stear andeshe namna hiyo anavyoelezea usipomkuta salanda au senkenke kaning'inia
 
1. Kamwe usitumie gear lever kama egesho la mkono wako

Tunaiona gear lever na kuitumia bila kujua nini kinafanyika nyuma ya pazia. Pale tunapotumia gear lever kubadilisha gear, selector fork ambayo huwa haizunguki huwa inakandamizwa kwenye collar inayozunguka na ile collar huwa inagandamizwa kwenye gear plate unayotaka kubadilisha. Kuweka mkono kwenye gear lever kwa muda mrefu kunasababisha kusagika kwa ile selector fork taratibu na kupunguza urefu wa maisha yake.
Nah mkuu si kweli, Hakuna kitu kama icho kusagika kwa selector, haukana any effect unapoegesha mkono, hata ukiweka tofali juu ya gear lever haiwezi kufanya chochote kwasababu mgandamizo wake hauna effect ya kusukuma chini hio lever. mkono usieke kwenye gear kwa sababu ya safety issue tu.

2. Usikanyage Clutch wakati gari linapoteremka katika mteremko ili kuongeza mwendo

Kukanyaga clutch wakati gari linateremka kwa kasi mteremkoni sio jambo la kufanya wakati unaendesha gari la manual. Hii itachangia sana kusaga baadhi ya maeneo katika mfumo wa gear wa gari lako. Pia itapelekea gari lako kukosa balance wakati wa kushuka katika mteremko. Cha kuzingatia ni makadirio ya mwendokasi, gear uliyopo na muda wa kuachia clutch husika.

Again Mkuu hii nayo sio sawa na pia more of a safety issue. Unapokanyaga clutch manake una disconnect engine na transmission, huo usago utatokea wap? remember the clutch is always working, and one of its work is to do that. Ukiteremka mlima usikanyage clutch, wacha iteremke ikiwa katika gear, hii inasaidia sana pale unapotaka kubrake
 
Back
Top Bottom