KAFA.cOm
JF-Expert Member
- Jun 22, 2013
- 1,301
- 739
Watu wengi hupenda kutembelea nchi mbalimbali kufanya utalii lakini mara nyingi hujikuta kwenye mikono ya sheria pindi wanapofanya makosa ambayo yamekatazwa katika nchi husika bila kujua, ili kujihadhari leo nimekuletea sheria ndogo kumi zilizopitishwa kwenye nchi mbalimbali ambazo unaweza usizijue.
1: Huruhusiwi kwenda dukani na sarafu (Coins) ukiwa Canada.
Kupitia sheria ya fedha nchini Canada “Canada currency Act” muuzaji yoyote anaruhusiwa kukataa kumuuzia mtu kitu chochote pindi anapokwenda kununua bidhaa akiwa na sarafu zaidi ya 25. Sheria hii ilipitishwa ili kuepuka upotezaji wa muda na usumbufu kwa wauzaji, hivyo ukitembelea nchi hiyo jitahidi kuwa na noti.
2: Ni kosa kutembea na Biblia hadharani ukiwa Maldives
Maldives ni Kisiwa kinachopendwa na watalii wengi kutoka sehemu mbalimbali Duniani ambacho kipo kusini-magharibi mwa Sri Lanka ambapo kina watu takribani 394,451 kati ya hao zaidi ya asilimia 99 ni Waislamu, huruhusiwi kutembea na Biblia hadharani kufanya hivyo ni kosa kisheria.
3: Usivute bangi ukiwa Jamaica
Hii inaweza kushangaza watu wengi ambao hudhani bangi inaruhusiwa nchini Jamaica kutokana na mmea huo kuwa maarufu zaidi nchi humo. Tangu mwaka 1913 bangi ilipigwa marufuku rasmi nchini humo, hivyo kuwa makini unapotembelea Jamaica na ujihadhari na kuvuta bangi.
4: Ni marufuku kula au kunywa nje ya makanisa na majengo ya umma ukiwa Italia
Italia ni miongoni mwa nchi zenye makanisa mengi ya zamani ambayo hutembelewa na watalii wengi, lakini ukiwa nchini Italia ni kosa kisheria kwa mwenyeji au mgeni kula au kunywa ukiwa pembezoni mwa majengo ya umma au makanisa.
5: Ni kosa kisheria kukumbatiana na kushikana mikono hadharani ukiwa Falme za Kiarabu
Falme za Kiarabu ni muungano wa nchi takribani saba na Dubai ikiwemo ambapo ndiyo nchi inayopendwa kutembelewa na watalii kutoka nchi mbalimbali duniani, lakini watalii wengi wamejikuta kwenye mkono wa sheria kwa kutokujua sheria hii.
6: Ni marufuku kutumia dawa ya mafua yenye vicks ndani yake ukiwa Japan
Kupitia sheria ya kuzuia madawa nchini Japan ni marufuku kutumia dawa yoyote ya mafua yenye kemikali ya vicks na ukikamatwa dawa yoyote yenye vicks unaweza kujikuta kwenye mkono wa sheria, kutokana na Japan walisaini sheria ya kupinga dawa zote zinazosisimua mwili ikiwemo vicks na dawa za kulevya.
7: Ni kosa la kisheria kulisha njiwa ukiwa Francisco
Watalii wengi hupenda kulisha ndege katika maeneo mengi ya kupumzikia lakini katika mji wa Francisco ni kosa la kisheria kwa watu kulisha njiwa ambapo unawza kufungwa jela na kulipa faini ukikutwa na kosa hilo. Sheria hii ilipitishwa baada ya kugundilika njiwa husambaza magonjwa kwa kasi sana.
8: Usipige picha ukitembelea Kazakhstan
Ni kosa kisheria kupiga picha majengo ya kiserikali, Uwanja wa Ndege na kambi za kijeshi ukitembelea nchini Kazakhstan. Ukikutwa na kosa hilo unaweza kufungwa jela.
9: Ni marufuku kutupa makapi ya jojo ‘bubble gum’ au big G ukiwa Singapore.
Unaweza ukaona ni kitu kidogo sana hasa ukiwa Tanzania lakini nchini Singapore ni kosa kubwa la kisheria ukitupa Big G iliyotumika na unaweza kupata adhabu ya kifungo kirefu.
10: Ni kosa kuvaa nguo za kuogelea mita 100 kutoka ilipoishia bahari nchini Hispania.
Ukitembelea nchini Hispania nguo za kuogelea zinaruhusiwa mita miaa kutoka ilipoishia bahari na kosa la kisheria kuvaa nguo hizo mitaani au sehemu mbali na ilipo bahari hivyo ukitembelea nchi hii kuwa makini mtu wangu.
Note: Jamaica pamenishangaza.