Mambo ambayo hayafai katika Katiba ya Nchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mambo ambayo hayafai katika Katiba ya Nchi

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by RGforever, Aug 2, 2012.

 1. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Mambo ambayo hayafai katika Katiba ya Nchi​

  Kuna vikundi mbalimbali vimejitokeza nchini vinavyowashawishi wananchi kutoa Maoni yao kulingana na Maslahi yao Binafsi. Vikundi hivyo vinawashawish watoe Maoni bila kujali maslahi ya Watanzania wote ila Yao binafsi na watu wao. Wanajaribu kuleta Ubaguzi na Kuvunja haki za kibinadamu.

  Watanzania kwa Ujumla tulikemee hili kwa Nguvu zetu zote bila kuona uwoga wowote ule wa viongozi hao na wananchi wao katika Mchakato wa Katiba Mpya

  TUKEMEE YAFUATAYO AMBAYO HAYANA TIJA KWA WATANZANIA​

  UDINI

  Kamwe watanzania wenzangu tusikubali nchi yetu iongozwe kwa Matakwa ya Udini,iwe ukristo,uislam,upagani n.k... Katika katiba Mpya Nchi hii ibaki bila kuwa Na Dini.. Bali Dini iwe maamuzi ya mtu binafsi bila kubugudhi/kuathiri uhuru wa mtu Mwingine yoyote yule...ambaye ni tofauti na Imani yako

  MAHAKAMA ZA KIDINI

  Kuna Vikundi vinaamasisha watu, kuwa katika katiba mpya kuwepo na Mahakama za Dini ambazo zitagharamiwa kwa kodi za mtanzania. Ndugu zangu kamwe usikubali hili... Mahakama za kidini hazina Maslahi kwa Mtu ambaye si wenye Dini husika. Ni kwa maslah ya Dini yenyewe. Katiba ya Nchi hii ni kwa Maslahi ya wote si ya watu fulani. Mahakama hizo zitakuwa zinahusika na Mambo ya Kidini.

  Je! Kwa mtu ambaye hana Dini kodi yake ikalipe viongozi wa kwenye Mahakama hizo???. Ni kitu ambacho hakiwezekani hata siku Moja. Tulikemee kwa Nguvu zote watu wa katiba Mpya wakija

  KUWE NA UHURU na HAKI

  Katika hili niweke msisitizo kabisa. MTANZANIA yoyote yule awe na uhuru wa Kufanya Atakavyo ili mradi asivunje Katiba na Sheria za nchi husika...

  Imetokea kuwa kuna Sheria inayowakataza Watanzania Wengine Kuchinja na Kuuza Bidhaa za Nyama kwa Jamii,bali anayetakiwa kuchinja ni Mwislam pekee[mfano mzur ni katika machinjio mbalimbali hapa nchini] na ikitokea hivyo amefanya hivyo anakamatwa na Polisi... Huku ni kuweka Nchi katika tabaka la Udini na kuona wengine hawana Maana.. Kwahiyo katika Katiba Mpya tukemee hili na Mtu yeyote yule awe MWISLAM,MKRISTO, MPAGANI awe huru na MALI YAKE mwenyewe na kufanya atakavyo

  MADARAKA KIDINI

  Kumetokea Watu wanaotaka madaraka kulingana na Dini zao.. Kwamba Rais akiwa Dini X mwaka huu Basi Mwakani awe Dini Y au Z.. Na iwe hivyo kuanzia Juu mpaka yule wa chini kabisa. Mf Mwalimu mkuu akiwa dini X basi mwl.mkuu msaidizi awe dini Y,daktar,Nesi,n.k bila kujali elimu zao. Kamwe kwenye katiba Mpya kupigwe Marufuku watu kumchagua Mtu kwa sababu ya Dini yake. Bali achaguliwe kulingana na Sifa zake na Uwezo wake na Kwa kura za Watanzania

  Pia Mtu yeyote yule aliye na sifa za Uongozi Mtanzania kutoka sehemu yeyote ile awe na haki ya kikatiba kugombea Uongozi

  ADHABU YA KIFO

  Katika katiba mpya, mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa Mujibu wa Sheria na Angetakiwa kupata adhabu ya kifo hasiuawe Bali Afungwe kifungo cha MAISHA pekee

  SHULE ZA SERIKALI

  Katika katiba Mpya Shule zote za Serikali ziweke Utaratibu wa Sare kwa Ajili ya Wanafunzi wote na zifuatwe. Kamwe Shule za Serikali zenye michanganyiko za Dini mbali mbali Pasiwe na Sare tofauti kwa wanafunzi.. Kuwe na Sare inayotambulika shule husika.

  HABARI ZA UOCHOCHEZI/KUVUNJA AMANI

  Si kitu cha kushangaza Watanzania wa Leo kupata habari kwa urahisi zaidi. Lakini je! Habari hizo zinaukweli ndani yake??. Na je anayezitoa Amefanya Research?....Mfano mzuri ni Kuhusu Idadi ya Watu, Matamko ya uchochezi,Kutukana Viongozi Waliopita,Kutukana Bunge n.k n.k. Katika Katiba Mpya Tukemee Habari ambazo hazina ukweli ndani yake na hakuna Research iliyofanyika[NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK] na Vyombo hivyo vipewe Onyo na kama Vikikaidi basi vifungiwe  ASANTENI

  KATIBA MPYA KWA WATANZANIA WOTE
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ntarudi . . . . .
   
 3. waziri/saidi

  waziri/saidi Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  waislamu wenzangu mafala kwani wanatuhimiza tuutetee mahakama ya kadhi wakati haiwahusu madhehebu mengine..nasikitika hata tume imejaa waislamu so sina imani na rais wangu dhaifu na uadilifu wake wa udini..somalia itahamia tz sasa...
   
 4. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Taratibu Mkuu. Ndo Maana Nimesema Tupinge Mambo hayo. We Watu wa Katiba Wakija Waambie Nchi hii isiwe na Dini Watanzania Wote tuwe wamoja kwa Mshikamano.
   
 5. C

  CUF Ngangari JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakristo wenzangu mafala sana inabidi tume ikija ikija tupinge MEMORUNDUM OF UNDERSTANDING ambapo msaada huu unasaidia dini moja sisi wakristo, na iwe hakuna MISAMAHA YA KODI KWA DINI ZOTE. tupinge kwa sana.
   
 6. t

  thatha JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu mada yako eyenyewe mbona kama inaegemea kupendelea upande mmoja wa kiimani. Umesbabisha hata wachangiaji wamekosa mwelekeo wameanza kutukana, na kusema hovyo tu humu JF asubuhi yoye hii.
   
 7. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Sijapendelea Upande wowote ule ukiona hivyo ujue hao ndo Wadini. Mimi nimepinga haya
  ¤Udini
  ¤Mahakama za kidini
  ¤Watu wawe na uhuru/haki
  ¤Adhabu ya Kifo ifutwe
  ¤Shule za Serikali ziwe na Sare maalum
  ¤Habari za Chuki na Kuvunja Amani

  HEBU NIAMBIE SEHEMU AMBAYO NIMEPENDELEA UPANDE MMOJA.?

  Nitofautishe Mimi na Mtu anayesema hivi:

  ¤Tunataka Mahakama za X au Y ziingie kwenye katiba. Wakati Watanzania wengine hawana Dini. Je nani atawatetea?

  ¤Tunataka Katika katiba Itambue uwepo wa Mungu![jiulize Mungu gani?]. Na yule ambaye hana Mungu je?

  ¤Tunataka Raisi atoke Dini X au Y. je! Wale ambao hawana Dini Wametendewa haki?

  ¤Tunataka Awamu za Urais ziwe kwa zamu! Akitoka X aje Y. Je! Mtu ambaye hana Dini atakuja Kutawala Lini.. Na tunawanyima haki zao maana Wanajua hakutakuw na Rais Daima

  HEBU Tujadili kwa Hoja si Kwa sababu Mi ni Dini X Au Y
   
 8. I

  Ibnu Mussa Member

  #8
  Aug 20, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada umekosa kujielewa. Hutakiwi kupinga maoni ya watu, kama wewe ni mjanja toa maoni yako. Ala! Huu wako wewe sasa ufala eti.
   
 9. Uncle Kaso

  Uncle Kaso JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 205
  Trophy Points: 60
  Nadhani umeshndwa kabisa kumwelewa mtoa mada,mbona yuko sahihi kabisa? Au ww unatakaje? Maoni gani unayoyataka ww? Au amekutouch? Toa point nawe tukuelewe kwm mtoa mada ametoa hoja zinazoeleweka! Do the same!
   
 10. Apolinary

  Apolinary JF-Expert Member

  #10
  Aug 20, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 4,698
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na kweli mtoa mada umegusa penyewe hasa hapo kwenye machinjio eti Peter akichinja Hamad hawez kula huu ni udini na katiba ikatae kabisa mambo haya!
   
 11. cabhatica

  cabhatica JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 1,074
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Wengine wanasema katiba mpya itamke haki za mwanamke, haki za walemavu, haki za watoto, haki za vijana....mbado kusikia haki za wanaume.....
  Kwangu huu wote ni ubaguzi. Napendekeza katiba itamke haki za MTANZANIA bila kujali jinsia, ulemavu, umri, dini n.k Kuwa mtanzania kutoshe kupata hizo haki period.
   
 12. P

  Pure Number Member

  #12
  Sep 8, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa mada ebu rudi kusoma MoU kisha ujue kua fedha zinazopelekwa ktk kanisa katoliki kupitia MoU ni za watz au watu gani???sasa kama mahakama ya kadhi hamtaki serkali ihudumie et kisa haina maslai kwa wengne na ni kodi ya wa-TZ,MoU kodi yake sio ya wa-Tz?mbona dini zingine hazifaidiki kutokana na MoU??
   
 13. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #13
  Sep 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  UNGEJUA HAKUNA PADRI/ASKOFU HATA MMOJA ANAYEGUSA HIZO PESA, ZINAENDA KUNUNUA MADAWA NA KUWALIPA WATANZANIA MADAKTARI HATA WAISLAM WOTE WALIOPO MAHOSPITALINI , Usipende kuchukua kila kitu kutoka kwa Sheikh bila kufikiria na wewe mwenyewe, madaktari waislam wapo BuGANDO na KCMC PIA


  Chuo cha Morogoro Kinapata Ruzuku kutoka Serikalini Mbona hauongei, ila MOU ndo unaona kosa kubwa. Kikwete aliwapa Fursa ya kujenga mahospitali na Mashule yasiyo na ubaguzi wowote ili awape na Nyie MOU, MKAKATAA manataka Ubaguzi wa kuwatibu waislam wenzenu pekee na mashule yenu tu. Mmejaa ubaguzi Mioyoni mwenu

  Hebu Niambie hiyo mahakama itamwajiri mtu ambaye si mwislam?
  Itakuwa inatoa Hukumu kwa Mtu ambaye si Mwislam?. Ndo Mana Waislam wenye Akili kama Kikwete aliwaambia MTAJIHUDUMIA wenyewe bila serikali kutia mkono wake Maana haina Faida kwa Watanzania

  Kikwete Ameongeza Pesa kutoka Bil 64 mpaka bil 74 kwa Huduma za Afya zitolewazo na Makanisa kwa Watanzania wote si Kwa wakristo pekee.. Na ataongeza pale inapowezekana maana ameona ninyi ni walalamikaji na Wabaguzi
   
 14. H

  HAPPY MAKUKU Senior Member

  #14
  Sep 9, 2012
  Joined: Dec 27, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nijuavyo mimi hela ya serikali lazima iafnyiwe auditing sasa mbona maaskofu walipinga ukaguzi wa hela za MOU ili kubaini kama zinaenda kuimarisha huduma za kijamii na sio makanisa? je unajua nchi inaendeshwa kidini tena kikatoliki? kwa sababu papa anawakilishwa na balozi hapa tz mbona shekhe wa makha hawakilishwi na balozi Tz, kwanini OIC inapingwa na wakatoliki wakati wao wana uhuru na umoja na makampuni ya kidini na misaada mbalix2, sasa kwanini kwa wakatoliki isiwe udini na iwe udini kwa waislam na OIC na kadhi? usawa uko wapi? nyie pingeni tu madai ya waislamu lkn hatma ya yote mtalaumiwa ninyi wakatoliki kwa sababu nyie itakuwa ndo chanzo cha kukosekana kwa amani kwa sababu ya ubinafsi na taamaa za umimi mlizonazo, yangu macho na kwaherini. Mungu Ibariki tz, na watu wake pia. mungu ibariki Africa.
   
 15. d

  dev senior JF-Expert Member

  #15
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 12, 2012
  Messages: 323
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 80
  hivi wewe kweli unafahamu chanzo cha kuanzishwa kwa MoU au unakurupuka?MoU ilianzishwa baada ya serikali kuzichukua shule,hospitali,zahanati zilizokuwa chini ya kanisa na kufanya ziwe chini ya serikali. Hayo yalifanywa na serikali kwa kuwa ilikuwa ina upungufu mkubwa wa huduma za kijamii kwa wananchi na kanisa pekee ndilo lilokuwa limefika maeneo mengi tena ya ndanindani.Kuhusu swala la elimu,serikali ilifanya hivyo ili kumsaidia muislam,mpagani apate elimu kwa kuwa wazazi wengi wakiislam walikataza watoto wao wasiende kwenye shule izo kwa kuwa wangelishwa nguruwe.Sasa wewe unataka hayo mashule,hospitali,zahanati zilizojengwa kwa sadaka za wakristo zisifidiwe? tatizo lenu kila jambo mnaliangalia kidini, hiyo ni hatari maana muda mwingine mnatishia hata amani ya nchi kwa kuingiza udini sehemu isiyostahili.
   
Loading...