Mambo 7/8 ya kufanya kabla na baada ya kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi

Chachasteven

JF-Expert Member
Jul 4, 2014
1,878
1,849
Nyie;

Wapendanao wote, wa jinsia zote, iwe wa kike au wa kiume au hata wasiojua jinsia zao husika wanapewa onyo kwamba, Mahusiano ya kimapenzi, pamoja na kuwa ni baraka yanaweza kuwa ni hatari pia - Hayatabiriki. Leo kicheko. Kesho kilio.!

Ndio hivyo, hutaki?? Umba dunia yako uweke sheria zako. Huko uweke furaha na vicheko tu bila vilio... Natania tu aisee. Teh teh teh!

Ngoja niwe serious. Huwa ipo hivi; Kwa yeyote ambaye ana mpango wa kupenda/kupendwa/kupendana anatakiwa aelewe kwamba anajiweka wazi na anakaribisha hatari ya wazi wazi kwenye mwili na roho yake. Hivyo basi, kwa namna yeyote, kwa kuwa mapenzi hayatabiriki, ikitokea la kutokea hakuna anaepaswa kumlaumu mwenzi wake.

Haiingii akilini naelewa na ni kwa sababu mara nyingi baada ya kasumba za mahusiano, wengi kama sio wote, hutoa maamuzi kwa kusikiliza hisia zao zaidi kuliko akili zao (Acting emotionally, rather than rationally.) - Ni kosa! Kwanini?? Kwa sababu wote mnapitia hatari zile zile. Kwa hivo huwa ni suala la timing tu - Yaani ukichelewa kumuacha mwenzio wewe ndiyo unaachwa alafu unalia ilihali angechelewa kukuacha wewe ndiyo ungemuacha.

Ni vigumu ku-deal na hizi hatari lakini inawezekana. Duniani, ukishafahamu tatizo ni nini basi umemaliza kila kitu labda utake mwenyewe kuendelea kusumbuliwa.

Kwa sababu hio, kuna vitu ambavyo ukivifanya kabla na wakati ambao unaanzisha hayo mahusiano vinaweza kupunguza au kuondoa hatari zilizomo kwenye mahusiano hayo - Hapa nimeweka vitu 7.

- 1) Mtu yeyote akionesha anakupenda hebu na wewe onesha kumpenda pia. Usijitie ugumu wa nazi. Humcheleweshi yeye, hapo unachelewesha watoto kuanza shule 😂😂

- 2) Kama unaemtaka yupo kwenye mahusiano mengine usijisumbue kumfanya aharibu mahusiano yake kwa sababu yako. Hii dunia inazunguka - Wewe ukiua kwa upanga utakufa kwa upanga pia.

Yaani ukimpata kwa kumwiba atakuja achukuliwe kutoka kwako kwa njia ile ile.

- 3) Hakuna kitu kama "tuwe marafiki, na taratibu taratibu tutakua wapenzi." Huko ni kupoteza muda.! Kwa ufupi tu, Jifunze kukubali kuwa mtu hakutaki alafu endelea na ishu zingine.

Kama ni huo urafiki usiwaze mapenzi ndani yake. Itaku-cost.!

- 4) Usianzishe mahusiano katika namna ambayo huwezi kumudu. Mara nyingi tunapomshawishi mtu mwingine atupende tunafanya vitu kibao, hadi vilivyo nje ya uwezo wetu.

Kwa mfano, ukianzisha mahusiano na mbwembwe za lunch box, Dinner dates kila ijumaa unatakiwa ujitahidi usikwame. Kwa lugha nyingine, ya kawaida, fanya yale unayoyaweza. Asiporidhika kubali she/he's way out your league - Tafuta saizi zako.

- 5) Mahusiano ya kimapenzi yanahitaji muda wako na pia yana gharama, nyingi zinahusisha pesa. Kwa hivo, ni vyema kujipanga na kuwa vizuri kiuchumi kabla ya kujihusisha na mapenzi.

Tukubali tukate, umaskini kwenye mapenzi huwa unavutia kuusoma kwenye riwaya/masimulizi au kuutazama kwenye filamu. Kwenye maisha halisi ni kinyaa. Taabu tupu!

Pia, unapokuwa kwenye mahusiano, hata yakunogee vipi usiache kutafuta hela. Mapenzi sio pesa ila pesa ina nafasi yake kwenye mapenzi.

- 6) Usiingie kwenye mahusiano ukiwa na wazo la kubadilisha tabia za huyo mwenzako. Wewe mtu mmoja sio ulimwengu na kwanza sio majukumu yako.!

Kama ulimkuta anakula bangi wewe jifunze kumpenda hivyo hivyo - ukijitia ufundi wa "walimu wa nidhamu" kitakachotokea sio lazima niandike.

Hata hivyo, hii point iko subjective. Kuna tabia inabidi u-deal nazo... KIAKILI.

Kwenye kesi nyingi, hii kurekebisha tabia ya mtu husababisha maugomvi au kupoteza maelewano na ndio inatupa point namba 7.

- 7) Wakati wa ugomvi/kutokuwepo maelewano jifunze kusuluhisha bila kurusha ngumi au makofi au matusi.

Wahenga walisema, "hasira hasara." Hapa ndipo pakuwa makini sana kwa sababu asilimia kubwa za uhusiano kufa zimelala hapa!!

Maneno na vitu unavyofanya ukiwa na hasara - Ni muhimu kujua namna ya kuiongoza hasira yako. Usiiruhusu ikuendeshe.

Ikikuendesha tu halafu mwenzio akajifanya anajikuna tu, atashangaa unachomoa betri ghafla na moto wake unalipua mwezi na sola sistimu yote. 😂😂

- 8) Hii ni rahisi na ngumu kufanya. Jipende! Jijali! Jiheshimu - Ipende na kuijali afya yako. Kula pamba safi mara kumi kumi baadala ya mara moja moja halafu kumbuka pamba safi sio lazima ziwe zenye gharama kubwa.

Ukijipenda. Ukajijali. Ukajiheshimu. Ukajali afya yako, hata kumpenda na kumheshimu mwenzako itakuwa rahisi.!

Halafu mara moja moja mtoe out - Hapa sio lazima muende five star hotels, kuna siku mnajiacha hata CHEKA TU. Siku nyingine ufukweni inatosha!! Mkitoka out mnazoeana zaidi na inasaidia sana kuimarisha uhusiano zaidi. Hata kiafya ipo poa sana.

Hitimisho: Hakuna guarantee ya moja kwa moja kwamba hivi vitafanya kazi kwa asilimia 100% kwa sababu ya hulka ya binadamu - hatujakamilika. Hivyo basi, ni vyema tuongeze point namba nane, kuwa mumuweke Mungu awe msimamizi wa hayo mahusiano yenu... Mkiwa na hofu ya Mungu ni vigumu hata kuchepuka.

Kama huamini katika Mungu, tafuta njia yako - Yaani ZA KUAMBIWA CHANGANYA NA ZAKO.
 
Back
Top Bottom