(Makala hii na nyingine kama hii zinapatikana katika tovuti ya: Uwekezaji Tanzania)
Sokoni ni eneo ambalo wauzaji wa bidhaa na wanunuzi wa bidhaa hukutana kubadilisha thamani vitu.
Katika nyakati hizi soko la bidhaa linaweza kuwa ni kwa njia ya mtandao hivyo sio lazima mnunuzi na muuzaji wa bidhaa kukutana uso kwa uso.
Kipindi hiki ni zama za sayansi na teknolojia ambazo zimetoa matumizi makubwa ya mtandao katika shughuli za mwanadamu hususani biashara hivyo kuna biashara nyingi zinafanyika kwenye mtandaoni (Online).
Ninaamini wengi wetu tumeingia katika shughuli za ujaseriamali kwa dhumuni la kuongeza kipato hatimaye kuwa na maisha mazuri.Hivyo basi swala la soko katika biashara yako ni muhimu sana kwasababu bidhaa unazozalisha ni kwaajili ya kuuza na kupata faida.Katika biashara ya aina yoyote mzalishaji hana budi afahamu mambo kadhaa ya msingi kuhusu soko la bidhaa yake au huduma na kisha kumsaidia kufanya maamuzi ya kumuwezesha kupata faida ya juu katika biashara anayoifanya.

- Unahitaji kufanya utafiti wa kina juu ya soko la bidhaa zako ilikujua ni bidhaa gani inayohitajika sokoni ?.Utafiti ndio utakao kupa jawabu la aina ya bidhaa ambayo inahitajika sokoni hivyo kama mjasiriamali usikurupuke tuu bila kuwa na uhakika wa aina ya bidhaa au huduma ambayo inahitajika sokoni.
- Je soko la bidhaa yako ni wapi na hali ya miundombinu za kulifikia iko vipi pia itakusaidia ufahamu gharama ya kufika sokoni kama utaamua kuuzia sokoni ,kama bidhaa yako itakuwa inauzika katika eneo la uzalishaji inamaana swala la gharama za usafirishaji utaliepeuka lakini kwa mjasiriamali ambaye hazalishi bidhaa kwake swala la gharama ya usafiri wa kupeleka bidhaa yake sokoni ni muhimu sana kulifahamu.Mfano kama unanunua alizeti Singida ni vizuri kujua gharama ya usafiri kutoka Singida kwenda kwenye soko husika la hiyo bidhaa.
- Bidhaa inahitajika kwa wingi kiasi gani na wakati gani sokoni ni vizuri kufahamu mambo hayo mawili muhimu ilikuepeka na uzalishaji mwingi ambao utapelekea kushusha bei ya bidha yako na kupunguza faida pili ni kuzalisha bidhaa yako sawasawa na majira ya soko mfano huwezi kuuza masweta na makoti wakati wa joto hivyo itakulazimu kusubiri nyakati za baridi kwasababu mzunguko wa bidhaa hizo huwa ni mkubwa wakati huo.
- Soko linahitaji bidhaa yenye sifa zipi,siku zote mfanya biashara huwa anazalisha bidhaa zenye kukidhi matakwa ya mteja sokoni hivyo ni vizuri kufahamu wateja wako ni kina nani na je wanahitaji bidhaa zenye ubora gani ? .Mfano kama wateja wako ni wanawake ni lazima bidhaa yako iendane na mahitaji yao kwa wakati huo (fashion).
- Kama wanunuzi watakuwa na utayari kununulia unakozalishia, je unao uwezo wakutosheleza mahitaji yao wewe pekee yako .Kama huwezi kukidhi kiwango ili uweze kujipanga kukidhi mahitaji kwa kuongeza uzalishaji au kwa kuungana na wazalishaji wengine.
- Linganisha bei ya bidhaa sokoni na bei ya kuuzia unakozalishia (ili ujue palipo na faida zaidi kwako baada ya kuondoa gharama ya kupeleka bidhaa zako sokoni ) Ila ukiamua kuuzia sokoni hakikisha unakuwa na uwezo wa kushindana na wauzaji wengine huko sokoni katika ubora wa bidhaa na wakati mwingine ushindani katika bei ya bidhaa .