Green Bird
Senior Member
- Jan 26, 2016
- 101
- 81
1. KUPUUZA SAIKOLOJIA YA MWANAMKE
Kitu muhimu sana anachotakiwa kukifahamu mwanaume katika uhusiano ni suala la saikolojia ya mwanamke na kujua kuchagua muda muafaka wa tendo. Mwanamke hufurahi na kuhisi amani pindi anapohisi au kuona kuwa mume anamjali na anajali hali yake ya kisaikolojia pindi anapokuwa hayuko katika hali nzuri. Jambo hilo litamfanya amheshimu sana na kumfanya apate utulivu wa haraka kwa kuhisi upendo wake na kuhisi kuwa anajali hali yake.
2. KUANZA TENDO BILA KUCHEZEANA
Mwanamke hukerwa na mwanaume asiyemchezea kabla ya tendo. Hapendi kuona mwanaume asiyefanya juhudi za kumfurahisha wakati wa tendo.
3. KUMCHUKULIA KAMA CHOMBO
Mwanamke hapendi tendo la ndoa kuwa kama kazi fulani anayotakiwa kuitekeleza au jukumu alilolazimishwa kuifanya. Hali hiyo itamfanya awe na ubaridi mbele ya mumewe na kuwa kichocheo cha kuchukia kushiriki naye tendo la ndoa.
4. KUONESHA HAMU KWA UKALI
Jambo hili ni miongoni mwa mambo yanayosababisha ndoa nyingi kufeli. Hili linatokana na wanaume kupuuza maumbile ya hisia za mwanamke, ambapo mume anakuwa na ukali fulani katika kuelezea hitajio lake la tendo la ndoa kwa ukali na kwa namna ambayo haimfurahisi mke. Mume huonesha hamu yake kana kwamba ni kazi anayotakiwa kuimaliza haraka ili aendelee na mambo mengine ya muhimu.
5. MAZOEA
Wapo wanawake wengi wanaopata shida kutokana na namna waume zao wanavyofanya tendo la ndoa. Waume zao wanakuwa hawana jipya, wanafanya mambo yaleyale kiasi kwamba hata kabla ya tendo mwanamke anakua anajua kwamba mumewe atafanya nini kitandani. Hili ni jambo linalowakera wanawake wengi, kwa sababu nao wana haki ya kukata kiu na kupata furaha wakati wa tendo kama ilivyo kwa wanaume.
6. KUTOONESHA HISIA
Mume kutoonesha hisia zake wakati wa tendo la ndoa hulifanya tendo husika kukosa hamasa na msisimko. Kuonesha hisia hulifanya tendo liwe bora kwa kiwango kikubwa, na mwisho wa tendo huwa wenye raha na furaha kwa wote wawili.