Mambo 5 yanayosababisha biashara za Wanawake kufa

puker

JF-Expert Member
Nov 22, 2018
393
1,000
Hivi leo wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahi na kufanyia kazi fursa mbalimbali.

Fursa hizo ni pamoja na uwekezaji katika biashara ndogo na za kati. Ni dhahiri kuwa mama ndiye nayeumia zaidi pale familia inapokuwa na uchumi mbaya. Mama hapendi kuona watoto wanakosa mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, mavazi, elimu, matibabu n.k.

Hivyo suala la kuboresha kipato cha familia limewafanya wanawake wengi kutafuta njia mbalimbali za kujipatia kipato ikiwemo njia ya kufanya biashara.

Hata hivyo pamoja na jitihada hizi zinazofanywa na wanawake, bado biashara zao ngingi hufa kutokana na sababu kadha wa kadha. Fuatana nami katika makala hii ufahamu mambo matano yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa.

1. Kukosa maarifa na elimu ya biashara
Kitu chochote au kazi yoyote inahitaji maarifa stahiki ili uweze kuifanya kwa kwa ufanisi. Ni dhahiri kuwa wanawake wengi huanzisha biashara pasipo kujiandaa kimaarifa au kutafuta ujuzi unaohitajika katika kuendesha biashara husika. Kumbuka hapa sizungumzii elimu ya sekondari au chuo kikuu bali maarifa yatakayokuwezesha kuendesha biashara husika kwa ufanisi. Kwa mfano unahitaji kupata maarifa yatakayokuwezesha kufanya haya yafuatayo:
 1. Utunzaji wa fedha (ikiwemo mikopo kama utakopa)
 2. Utunzaji wa taarifa za biashara
 3. Utafutaji wa wateja
 4. Uandaaji na uboreshaji wa bidhaa, huduma n.k
Haya ni baadhi tu ya maarifa ya msingi ambayo mfanyabishara anatakiwa kuwa nayo. Mwanamke anayefanya biashara akijipatia maarifa haya ya kutosha hakika uendeshaji wa biashara yake utakuwa bora na wa uhakika; hivyo biashara yake itadumu zaidi. Maarifa haya yanaweza kupatikana bure katika taasisi zinazowawezesha wanawake pamoja na kwenye mtandao.

2. Kukosa msaada na ushirikiano
Ili kufanikiwa katika mambo kadha wa kadha tunahitaji ushirikiano ua msaada wa watu wengine kwa namna moja au nyingine. Simaanishi kuwa tuwategemee watu wengine kwa kila kitu; bali ukumbukue tu kuwa huwezi kufanya kila kitu peke yako. Wanawake wengi hukosa ushirikiano hasa katika ngazi ya familia.

Badala ya mume au wanafamilia wengine kumpa mwanamke huyu ushirikiano katika biashara yake wao huwa ni wa kwanza kumkejeli, kumkatisha tamaa, kumsema, kumlundikia mambo na hata kumwachia kila kitu peke yake. Matokeo yake mwanamke huyu huzidiwa na kushindwa kumudu biashara yake.

3. Kuiga au kukosa ubunifu
Wanawake wengi wanapoanzisha biashara hawatumii ubunifu bali wao hukurupuka kwa kuona biashara za wengine pekee. Kabla hujaanzisha biashara hakikisha unatumia ubunifu kubuni biashara yako.

Epuka kuiga kwani hujui ndani ya biashara unayoiga kuna nini; inawezekana kuna changamoto usizoziweza. Usione tu biashara kwa nje na kuirukia; hakikisha pia biashara unayoichagua unaipenda kutoka moyoni mwako.

4. Tamaa
Wanawake wengi huvutiwa na vitu mbalimbali hata kama hawavimudu kifedha. Leo umemwona rafiki yako ana simu au mkoba au hereni au viatu ama hata nguo fulani nawe unatamani kuwa nayo bila hata kujua gharama zake zikoje na utapataje pesa hizo. Hili limewapelekea wanawake wengi kutumia mitaji yao ya biashara kwa ajili ya tamaa na mashindano.

Mara kadhaa utasikia mwanamke anasema “nimekula mtaji”; kulikuwa na shunguli fulani au kitu fulani kilinigharimu. Hakika ukiendeleza taamaa hutoweza kuendesha biashara na ikafanikiwa. Ni lazima ujiwekee nidhamu katika matumizi yako ya fedha ili uweze kufanikiwa.

Mambo unayoweza Kufanya:
 1. Tambua uwezo wa kipato chako ili ujiwekee mipaka.
 2. Bainisha matumizi ya lazima.
 3. Tenga pesa za biashara na maisha yako binafsi.
 4. Weka akiba.
 5. Epuka tamaa na vishawishi vya marafiki.

5. Majukumu ya kifamilia
Kiafrika mwanamke ndiye mwenye jukumu kubwa la kuwa karibu na familia yake. Si rahisi kwa mwanamke wa kiafrika kushinda kwenye biashara kwa siku nzima bila kuwa na utaratibu mwingine wa kutunza familia yake.

Swala hili limekuwa likiwafanya wanawake kutokuwa na muda mwingi wa kutulia na kushughulikia biashara zao; jambo hili limeathiri kwa kiasi kikubwa biashara nyingi za wanawake. Hata hivyo unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kukabiliana na hili:

Tafuta usaidizi kwa baadhi ya majukumu yako ya biashara au ya nyumbani.

Tumia muda vyema (Punguza kazi zisizokuwa na ulazima – hakuna haja ya kukaa saluni siku nzima ukisuka wakati unaweza kupunguza nywele au kuzichana na kuzibana pekee.)

Shirikisha familia katika mgawanyo wa majukumu ili nao pia wakupunguzie kazi.

Chagua biashara ambayo unaipenda na unaimudu; hili litakupa ufanisi zaidi unapoifanyia kazi.

Hitimisho
Yaliyojadiliwa hapa ni baadhi ya mambo makubwa yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa. Hata hivyo njia za kukabiliana na mambo haya zimejadiliwa pia; hivyo ni swala la wewe tu kufanya maamuzi ili uweze kumudu na kufanikiwa katika malengo yako ya kibiashara. Weka malengo leo na uyafuate ndipo utakapoweza kufanikiwaSent using Jamii Forums mobile app
 
life is Short

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
4,736
2,000
Kwa mtazamo wangu binafsi:~ WANAWAKE WAFANYA BIASHARA kipato chao kipo ktk mzunguko wa fedha wa kila siku !!
Hiyo ni baraka kwa uchumi.... "kushika au kuzui fedha au kubana matumizi fulanifulani huo ni ubakhili"
Ndg puker hela za wakina mama huwagusa watu wengi kibiashara na kijamii..!!
 
Ubakhili ni moja ya sifa muhimu ya kufikia mafanikio

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
2,418
2,000
Biashara imekuwa ngumu bidhaa zinazotoka haraka sasa zinafaida ndgo hali ambayo kwa mwanamke kufanikiwa kwenye biashara ni ngumu kujibahilia hawawezi
asubuhi supu kongolo 2000
Boda boda kwenda kazini na kurudi 3000
Mchana chips mayai na soda 3000
Jumla 8000
Hapo gharama zingine za kuvaa wengi
kodi ya pango na serikali wengi hawawezi
 
highness long

JF-Expert Member
Sep 30, 2017
520
500

Hahahah, hatari Haya maisha ukusema ujibane sana unaweza hata usile siku nzima cha msingi ni budget nzuri tuu kwa matumizi ya kawaida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
C_O

Member
Jan 3, 2019
54
125
Ubakhili ni moja ya sifa muhimu ya kufikia mafanikio

Sent using Jamii Forums mobile app
Kibiashara ubahili sio sifa muhimu kufikia mafanikio.. ngoja nitete hoja yangu; unapoingia kweny biashara jua kuna matumizi ambayo hutakiwi kuyakwepa kwa hili pia itaendana na hali kiuchumi biashara yako iko sehem gani, nakuapa mfano mtu anae andika hapa ni mkinga kama mnawajua wachaga basi nitakwambia sifa alizo nazo mchaga ni saw na mkinga nina ndugu anejishughulisha na biashara ya wholesaling y nguo kariakoo hiv karbun alkuwa akijenga nyumba/ghorofa kwaajil ya biashar lakin TRA hawakubaki nyuma walimfuatilia kutak kujua amewezaj kujenga hilo ghorofa (labda mnaweza jua kwann walkuw wanmfuatlia) mwisho wa siku akatikia kulipa fine ya 100milioni aya turudi kweny point kwa yy kusave hela kuto kulipshwa tna anachotakiw kufany n kuwa serious na his financila books/report soo atatakiw kuajiri muhasibu pro kufanya kazi io sas ukisema ubahir mwngne anabania na kuona kumpa kazi muhasibu pro itamkata lakn mmeshaa ona mwsho wa siku nn kinaweza tokea

Conclusion: sio uwe bahiri though ni njia/tactic nzuri ila uwe na mfumo mzuri then kwa upande wangu nitasema io ndo sifa muim kufanikiwa kibiashara nirudie tna kibiashara sio kitu kingne

are just my thought
 
Nikusahishe kidogo mkuu, labda tuanzie kwenye maana halisi ya neno bahili,
BAHILI:- Ni yule mtu anebania pesa/mali yake yoyote kuitoa pasipokuwa na ulazima(bila mpangilio maalumu).

Naweza kukupa mfano, kula chakula na maji Ni muhimu lakini soda...sio lazima, hvy mtu bahili hawez kunywa soda na maji ilihali maji tu yanamtosha ile fedha la soda itaenda kufix mambo mengine...huo ni mfano upande wa matumiz kwenye chakula.

Pia mfano hata kwenye matumiz ya fedha katika ujenzi Jambo analoliona anaweza kulifanya, atafanya yeye Kama kibarua katika kumsaidia fundi ili ile hela atakayo lipwa kibarua ifanye mambo mengine.
Hivyo kiufupi ukiishi katika mfumo huo utajikuta unasave pesa nyingi itakayo sababisha kasi ya maendeleo yako kuongeza. Hiyo ndio sababu kubwa kwa hayo makabila mawili kuf
anikiwa zaidi katika biashara...maana pesa inahitaji nidhamu ya hali ya juu. Bila kusahau pia jitihada inahitajika.

Naamini nitakuwa nimekujibu ipasavyo boss.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 • Thanks
Reactions: C_O

Ofcoz umenijibu ila point yangu kubwa n kwamba watu wengi hawatofautishi vitu hivi viwili kuna personal issues na kuna business issues koo huwaga sana kwa upande wangu mtu akiongelea swala la saving kama ni key kwnye mafanikio ya kibiashara na doubt maan kuna maan mbili apo kuna mtu ukimwambia ivoo kchwani atafikiria matumizi yake binafsi (kama chakula,mavazi,usafiri na mengne) sas nachokiongerea mm n kwamb izoo ni personal expenses na ndo maan ukiwa unaanda income statement amna mahali expenses kama izo zina appear

Ndo maan nikasema mfumo/ how you scale your business ndo key factor kwa biashara kufanikiwa

Maana ukiwa na mfumo mzuri pia na management nzuri kweny biashara yyte the sky is a limit usishangae unavopewa report ya baadh ya biashara unakuta kweny miaka tu ya mwanzo ya kuanza biashara yao ilkuwa ina growth rate ya 500% though cjui kama kuna percentage ya aina io mifano hai ipo you name them
 
Nimekuelewa vyema boss... Asante kwa somo zuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
 • Thanks
Reactions: C_O

Kalpana

JF-Expert Member
Jun 16, 2017
6,387
2,000
Biashara imekuwa ngumu bidhaa zinazotoka haraka sasa zinafaida ndgo hali ambayo kwa mwanamke kufanikiwa kwenye biashara ni ngumu kujibahilia hawawezi
asubuhi supu kongolo 2000
Boda boda kwenda kazini na kurudi 3000
Mchana chips mayai na soda 3000
Jumla 8000
Hapo gharama zingine za kuvaa wengi
kodi ya pango na serikali wengi hawawezi
Umenchekeshaaa bado vocha ya kuperuzi page za umbea instagram
 
witnessj

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
17,741
2,000
Hivi leo wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika kuwahi na kufanyia kazi fursa mbalimbali.

Fursa hizo ni pamoja na uwekezaji katika biashara ndogo na za kati. Ni dhahiri kuwa mama ndiye nayeumia zaidi pale familia inapokuwa na uchumi mbaya. Mama hapendi kuona watoto wanakosa mahitaji yao ya msingi kama vile chakula, mavazi, elimu, matibabu n.k.

Hivyo suala la kuboresha kipato cha familia limewafanya wanawake wengi kutafuta njia mbalimbali za kujipatia kipato ikiwemo njia ya kufanya biashara.

Hata hivyo pamoja na jitihada hizi zinazofanywa na wanawake, bado biashara zao ngingi hufa kutokana na sababu kadha wa kadha. Fuatana nami katika makala hii ufahamu mambo matano yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa.

1. Kukosa maarifa na elimu ya biashara
Kitu chochote au kazi yoyote inahitaji maarifa stahiki ili uweze kuifanya kwa kwa ufanisi. Ni dhahiri kuwa wanawake wengi huanzisha biashara pasipo kujiandaa kimaarifa au kutafuta ujuzi unaohitajika katika kuendesha biashara husika. Kumbuka hapa sizungumzii elimu ya sekondari au chuo kikuu bali maarifa yatakayokuwezesha kuendesha biashara husika kwa ufanisi. Kwa mfano unahitaji kupata maarifa yatakayokuwezesha kufanya haya yafuatayo:
 1. Utunzaji wa fedha (ikiwemo mikopo kama utakopa)
 2. Utunzaji wa taarifa za biashara
 3. Utafutaji wa wateja
 4. Uandaaji na uboreshaji wa bidhaa, huduma n.k
Haya ni baadhi tu ya maarifa ya msingi ambayo mfanyabishara anatakiwa kuwa nayo. Mwanamke anayefanya biashara akijipatia maarifa haya ya kutosha hakika uendeshaji wa biashara yake utakuwa bora na wa uhakika; hivyo biashara yake itadumu zaidi. Maarifa haya yanaweza kupatikana bure katika taasisi zinazowawezesha wanawake pamoja na kwenye mtandao.

2. Kukosa msaada na ushirikiano
Ili kufanikiwa katika mambo kadha wa kadha tunahitaji ushirikiano ua msaada wa watu wengine kwa namna moja au nyingine. Simaanishi kuwa tuwategemee watu wengine kwa kila kitu; bali ukumbukue tu kuwa huwezi kufanya kila kitu peke yako. Wanawake wengi hukosa ushirikiano hasa katika ngazi ya familia.

Badala ya mume au wanafamilia wengine kumpa mwanamke huyu ushirikiano katika biashara yake wao huwa ni wa kwanza kumkejeli, kumkatisha tamaa, kumsema, kumlundikia mambo na hata kumwachia kila kitu peke yake. Matokeo yake mwanamke huyu huzidiwa na kushindwa kumudu biashara yake.

3. Kuiga au kukosa ubunifu
Wanawake wengi wanapoanzisha biashara hawatumii ubunifu bali wao hukurupuka kwa kuona biashara za wengine pekee. Kabla hujaanzisha biashara hakikisha unatumia ubunifu kubuni biashara yako.

Epuka kuiga kwani hujui ndani ya biashara unayoiga kuna nini; inawezekana kuna changamoto usizoziweza. Usione tu biashara kwa nje na kuirukia; hakikisha pia biashara unayoichagua unaipenda kutoka moyoni mwako.

4. Tamaa
Wanawake wengi huvutiwa na vitu mbalimbali hata kama hawavimudu kifedha. Leo umemwona rafiki yako ana simu au mkoba au hereni au viatu ama hata nguo fulani nawe unatamani kuwa nayo bila hata kujua gharama zake zikoje na utapataje pesa hizo. Hili limewapelekea wanawake wengi kutumia mitaji yao ya biashara kwa ajili ya tamaa na mashindano.

Mara kadhaa utasikia mwanamke anasema “nimekula mtaji”; kulikuwa na shunguli fulani au kitu fulani kilinigharimu. Hakika ukiendeleza taamaa hutoweza kuendesha biashara na ikafanikiwa. Ni lazima ujiwekee nidhamu katika matumizi yako ya fedha ili uweze kufanikiwa.

Mambo unayoweza Kufanya:
 1. Tambua uwezo wa kipato chako ili ujiwekee mipaka.
 2. Bainisha matumizi ya lazima.
 3. Tenga pesa za biashara na maisha yako binafsi.
 4. Weka akiba.
 5. Epuka tamaa na vishawishi vya marafiki.

5. Majukumu ya kifamilia
Kiafrika mwanamke ndiye mwenye jukumu kubwa la kuwa karibu na familia yake. Si rahisi kwa mwanamke wa kiafrika kushinda kwenye biashara kwa siku nzima bila kuwa na utaratibu mwingine wa kutunza familia yake.

Swala hili limekuwa likiwafanya wanawake kutokuwa na muda mwingi wa kutulia na kushughulikia biashara zao; jambo hili limeathiri kwa kiasi kikubwa biashara nyingi za wanawake. Hata hivyo unaweza kufanya mambo yafuatayo ili kukabiliana na hili:

Tafuta usaidizi kwa baadhi ya majukumu yako ya biashara au ya nyumbani.

Tumia muda vyema (Punguza kazi zisizokuwa na ulazima – hakuna haja ya kukaa saluni siku nzima ukisuka wakati unaweza kupunguza nywele au kuzichana na kuzibana pekee.)

Shirikisha familia katika mgawanyo wa majukumu ili nao pia wakupunguzie kazi.

Chagua biashara ambayo unaipenda na unaimudu; hili litakupa ufanisi zaidi unapoifanyia kazi.

Hitimisho
Yaliyojadiliwa hapa ni baadhi ya mambo makubwa yanayosababisha biashara nyingi za wanawake kufa. Hata hivyo njia za kukabiliana na mambo haya zimejadiliwa pia; hivyo ni swala la wewe tu kufanya maamuzi ili uweze kumudu na kufanikiwa katika malengo yako ya kibiashara. Weka malengo leo na uyafuate ndipo utakapoweza kufanikiwaSent using Jamii Forums mobile app
Namba 4 hasa hasa ndo the main source...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Clkey

JF-Expert Member
May 29, 2014
5,476
2,000
4 na 5 ni changamoto kwangu jamani, hasa 4 najkutaga nishakula mtaji hata nilivyokula nakuwa sielewi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom