Mambo 21 ya kufanyiwa marekebisho ya kisheria katika mchakato wa Uteuzi wa wagombea Urais, Ubunge na Udiwani

Matojo Cosatta

JF-Expert Member
Jul 28, 2017
234
390
MAMBO 21 YA KUFANYIWA MAREKEBISHO YA KISHERIA KUHUSU MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA URAIS, UBUNGE NA UDIWANI.

"Good laws emanate from worst conducts of human beings".

Uchaguzi Mkuu ni mchakato (process) ambao una vijichakato (sub-processes) kadhaa ikiwemo kuandikisha wapiga kura, kutoa elimu kwa wapiga kura, uteuzi wa wagombea, kampeini za Uchaguzi, kupiga kura, kuhesabu kura, kujumlisha kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi. Kwa leo nitajikita katika kutoa mapendekezo ya kuboresha kijichakato kimoja tu ambacho ni Uteuzi wa Wagombea katika ngazi ya Tume ya Taifa ya uchaguzi na vijichakato vingine vya mchakato wa uchaguzi mkuu nitavifanyia kazi siku za usoni katika awamu kadhaa na tofauti

Kutokana na matukio ambayo tumeshuhudia mpaka sasa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ngazi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mapendekezo yangu kuwa sheria za Uchaguzi zifanyiwe marekebisho kama ifuatavyo;

(1) Kwanza, Sheria iweke ukomo wa muda wa Tume ya Uchaguzi kufanya uamuzi wa rufaa za wagombea, kuwepo na time limit vinginevyo Tume ya Uchaguzi inaweza kufanya uamuzi wa rufaa baada uchaguzi mkuu kufanyika. Who knows?, tume ya Uchaguzi inaweza kufanya uamuzi wa rufaa za mwaka huu mwaka ujao mwezi August, 2021 na bila kuvunja sheria. Kwa mfano, wiki 1 ikihesabiwa tokea siku ya uteuzi iwe ni muda wa kuweka na kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi ya wagombea na wiki 2 tokea Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kufanyia uamuzi mapingamizi ya wagombea uwe ni muda wa kusikiliza na kufanyia uamuzi rufaa za wagombea.

(2) Pili, iwe ni marufuku kisheria kwa Kampeini za uchaguzi kuanza kabla ya Tume ya Uchaguzi kusikiliza na kuamua rufaa zote za wagombea kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi . Kampeini za uchaguzi zianze baada ya rufaa zote kuwa zimefanyiwa uamuzi ili wagombea wote wapate muda sawa na unaolingana kufanya Kampeini za uchaguzi na kuepuka kuvuruga Ratiba ya kampeini za uchaguzi (Cordinated Election Campaign Time Table). Sheria iweke marufuku uchaguzi kufanyika na kampeini za uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani kuanza kabla ya Tume ya Uchaguzi kusikiliza na kufanyia uamuzi rufaa za wagombea

(3) Tatu, makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi ikome kuwa sababu ya kutengua uteuzi wa mgombea badala yake mgombea apewe muda wa kuzifanyia marekebisho fomu ya Uteuzi na fomu zingine za Uchaguzi.

(4) Nne, uteuzi wa mgombea Urais au ubunge utenguliwe tu kutokana na mgombea kukosa sifa za kugombea Urais au ubunge ambazo zimetajwa bayana au waziwazi na masharti ya Ibara ya 67 (1) na (2) na 39 (1) na (2) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano na sio kutokana na makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(5) Tano, sifa za mtu kugombea Udiwani ziwekwe kwenye Katiba na uteuzi wa mgombea udiwani utenguliwe tu kutokana na mgombea kukosa sifa za kugombea udiwani ambazo zimetajwa bayana au waziwazi na katiba na sio kutokana na makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(6) Sita, tuache huu utamaduni wa kuwa na siku moja ya kurudisha fomu na siku moja ya uteuzi wa wagombea wote ili kupunguza hatari (risky) ya wagombea kuvamiwa, kujeruhiwa na kutekwa kwa kwa lengo la kuharibu au kunyang'anywa fomu ya Uteuzi na mahasimu wake wa kisiasa na ili kutoa fursa kwa wagombea kukosoa makosa kwenye fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(7) Saba, tuwe na deadline tu ya kurudisha fomu za uteuzi na tuwe na na deadline tu ya uteuzi ili mgombea apate fursa ya kurudisha fomu ya uteuzi wakati wowote kabla ya deadline na ateuliwe wakati wowote kabla ya deadline. Hii itatoa fursa kwa mgombea kurekebisha makosa yake kwenye fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kabla ya deadline iwapo kuna makosa kwenye fomu hizo ambayo yamegundulika baada ya kurudisha fomu na pia hii itasidia kufanya watu wenye nia mbaya wanaotaka kumpokonya fomu ya Uteuzi mgombea kushindwa kujua muda ambao mgombea atarudisha fomu, hivyo, utaratibu huu utapunguza au kuondoa kabisa vitendo vya kuteka au kuvamia wagombea kwa lengo la kuharibu au kuwanyang'anya fomu za Uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(8) Nane, swala la mgombea kwenda kuchukua fomu ya Uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa Tume ya uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Saidizi wa Uchaguzi iwe ni hiyari (option) na isiwe lazima, hivyo, fomu zote za Uchaguzi ikiwemo Fomu za Uteuzi ziwekwe kwenye website ya Tume ya Uchaguzi na mgombea waruhusiwe kupakua (download) fomu hizo kwenye website ya tume ya Uchaguzi na kuzijaza na kuzirudisha kwenye Tume ya Uchaguzi bila kuwepo sharti la kuchukua fomu hizo kutoka kwa Tume ya uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi. Hii, itaondoa changamoto ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na Maafisa wengine wa Tume ya uchaguzi kukataa kwa nia mbaya kutoa fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa mgombea na watu wahalifu kuchukua fomu za mgombea halali aliyeteuliwa na chama cha siasa kwa nia mbaya ya kumzuhia asiteuliwe na tume ya uchaguzi au Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi.

(9) Tisa, wagombea wapewe fursa ya kurudisha fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa njia ya kielektroniki katika mfumo wa nakala laini (soft copy) kupitia njia za e-mail, fax nakadhali kwa masharti kwamba nakala halisi (original copy) za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwenye umbo la nakala ngumu (hard copy) zirudishwe kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ndani ya 7 baada siku ya mwisho (deadline) ya kurudisha fomu. Utaratibu huu unatumiwa na Chama cha Mawakili wa Tanganyika (Tanganyika Law Society) na unatambuliwa na Kanuni ya 17 ya Kanuni za Uchaguzi za Chama cha Mawakili wa Tanganyika, 2018 (Tangazo la Serikali Na 116 la 2018) yaani the Tanganyika Law Society (Elections) Regulations, 2018 . Pia, hata njia ya registered mail inaweza kutumika kupitia shirika la Posta. Utaratibu huu utandoa changamoto ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kujificha au kukataa kwa nia mbaya kupokea fomu siku ya mwisho (deadline) au siku zingine kabla ya siku mwisho ya kurudisha fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(10) Kumi, Sheria imtake kwa lazima kuwa mgombea anayeweka pingamizi lazima apeleke nakala ya mapingamizi kwa mgombea mwenzake anayemwekea pingamizi na kama ikishindwa kumpata mgombea basi kwenye ofisi za chama chake cha siasa za ngazi husika kabla ya kupeleka pingamizi hilo kwa Tume ya Uchaguzi au Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ili kuondoa changamoto ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kula njama na baadhi ya wagombea kwa kuwawekea wagombea wengine mapingamizi baada ya siku ya mwisho (deadline) ya kuweka mapingamizi kupita au kuwa time barred.

(11) Kumi na moja, Sheria ipige marufuku kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea yoyote kutokana na makosa ya kujaza fomu yaliyofanywa wa watu wengine wanaohusika na uchaguzi kama vile wadhamini (nominators), Afisa Viapo (Hakimu), maafisa na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwemo Wasimamizi na Wasimamizi wa Saidizi wa Uchaguzi na viongozi wa vyama vya Siasa kama vile Katibu wa Wilaya na Katibu Mkuu wa chama cha siasa.

(12) Kumi na mbili, Kamishna wa Viapo (Commissioner for Oaths) wote wakimemo Majaji, mahakimu mawakili wa kujitegemea na wanasheria wa serikali waruhusiwe kushuhudia kiapo na kuwaapisha wagombea Urais, Ubunge, na Udiwani katika mchakato wa kujaza fomu za uteuzi. Tuache utamaduni wa kuwatumia mahakimu na majaji pekee kama Kamishna wa Viapo katika wa kujaza fomu za uteuzi. Hii, itampa fursa mgombea kutumia Kamishna wa Viapo ambaye ana imani naye na ambaye anafikika kirahisi na mgombea (accessible) na kwa muda wowote.

(13) Kumi na tatu, wakati wa kufanya uamuzi kuhusu mapingamizi iwe ni marufuku kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi, Msimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea kwa msingi wa tuhuma za kosa la jinai ambazo ama bado hazijafanyiwa uamuzi na Mahakama au hakuna kesi yoyote iliyowahi kufunguliwa Mahakamani kuhusu tuhuma hizo. Sheria ipige marufuku kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea kutokana na tuhuma tu za kutenda kosa la jinai bila mgombea aliyepiga pingamizi kuambatanisha hukumu ya Mahakama ambayo ilimtia hatiani kwa kutenda kosa la jinai mgombea mwenzake ambaye amewekewa pingamizi.

(14) Kumi na Nne, tuache utamaduni wa kutoa haki ya kuweka mapingamizi kwa wagombea pekee na kuwanyima haki hiyo wapiga kura. Wapiga kura wote waruhusiwe kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani ili kuondoa hatari (risk) ya kumteka au kumyang'anya fomu ya Pingamizi mgombea ili asiweke mapingamizi dhidi ya mgombea mwingine.

(15) Kumi na tano, iwapo mgombea mmoja tu ndo ameteuliwa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Msimamizi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kugombea nafasi ya ubunge au Udiwani basi apigiwe kura za ndio na hapana, hivyo, utaratibu wa mtu kuwa mbunge bila kupigiwa kura na wananchi ukomeshwe. Na pia iwapo mgombea mmoja tu ndo ameteuliwa kugombea nafasi ya ubunge au Udiwani na Msimamizi au Msimamizi Msaidizi mtawalia basi sheria iruhusu kuwepo na mgombea kivuli wa ubunge au udiwani na mawakala vivuli ambao watalinda kura na maslahi ya wapiga kura ambao watapiga kura za hapana.

(16) Kumi na sita, mgombea wa nafasi ya Rais ambaye uteuzi wake umekataliwa au umetenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi apewe haki ya kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi katika Baraza la Migogoro ya Uchaguzi (Election Disputes Tribunal) ambalo litaundwa na watu 5 wenye sifa za kuwa majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa. Pia, mchakato wa uchaguzi wa Rais ikiwemo kampeini za uchaguzi lazima usimame mpaka Baraza la itakapotoa uamuzi wake. Pia, Wabunge na Madiwani ambao hawajaridhishwa na maamuzi ya Rufaa zao ambayo yamefanywa na tume ya taifa ya uchaguzi wapewe haki na fursa ya pili ya kukata rufaa kwenye Baraza la Migogoro ya Uchaguzi.

(17) Kumi na saba, mgombea wa chama cha siasa akijitoa kwenye uchaguzi basi chama cha siasa husika kipewe fursa ya kuteua mgombea mwingine kuziba pengo lililoachwa na mgombea ambaye amejitoa kwenye uchaguzi tofauti na sasa ambapo sheria inasema kuwa mgombea akijitoa ndo imetoka hiyo chama cha siasa hakiwezi kuteua mgombea mwingine ili kuondoa uwezekano wa Mgombea kuongwa au kutishwa ili ajitoe kwenye kushiriki uchaguzi.

(18) Kumi na nane, muda wa kukata Rufaa kwenda Tume ya Uchaguzi dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi uanze kuhesabiwa tokea siku ambayo mgombea amepata uamuzi wa maandishi wa kutengua uteuzi wake au kukataa pingamizi lake na sio tokea siku ya uamuzi kwa sababu mgombea akichelewa kupatiwa uamuzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi atajikuta nje ya muda wa kukata rufaa au akipewa uamuzi masaa machache kabla ya muda wa rufaa kuisha hatapata muda wa kutosha kuaandaa rufaa yake.

(19) Kumi na tisa, muda wa kukata Rufaa kwenda Tume ya Uchaguzi dhidi ya uamuzi wa Msimamizi na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi uongezwe kutoka siku moja walau mpaka siku 3 tokea mgombea alipota uamuzi wa kutengua uteuzi wake au kukataa pingamizi lake ili wagombea wapate muda wa kutosha kuandaa rufaa zao.

(20) Ishirini, liondolewe kwenye sheria sharti la mgombea udiwani kuwasilisha Hati kutoka kwa Afisa Usajiri wa Wapiga Kura wa Kata kudhibitisha wadhamini wa mgombea ni wapiga kura ambao wameandikishwa katika Daftari Wapiga Kura katika Kata husika. Msamimizi Msaadizi wa Uchaguzi ndo adhibitishe swala hili kwenye fomu ya Uteuzi.

(21) Ishirini na moja, wagombea wapewe haki ya kuwakilishwa na wanasheria katika mchakato mzima wa Uchaguzi hususani katika kuweka, kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi na kukata na kusikiliza rufaa ili kutenda haki kwa wagombea ambao sio wanasheria wakati wanapokabiliana na wagombea ambao ni wanasheria. Piga picha mgombea ambaye sio Mwanasheria akutane na mgombea ambaye ni mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi kwenye shauri la kusikiliza mapingamizi mbele ya Tume ya Uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi.

Imeandikwa na Matojo M. Cosatta.
 
Umeandika Mambo mazuri na ndo inavyotakiwa nasikitika tu mawazo mazuri kama haya kwa wenye mamlaka hawawezi kukubaliana na wewe. Nasikitika tu

Tanzania bado sana mh kikwete kidogo tu amalize matatizo haya kwa katiba mpya ila ndo ivyo ilivyokua
 
Andiko Bora kabisa la siku.

Tatizo ni kuwa kwa sasa nchi ipo chini ya mtu mmoja tu. Yeye ndio Alfa na Omega mwanzo na mwisho amejaa hila uonevu visasi na chuki.

Jiwe ni sikio la kufa ambalo halisikii dawa.
 
..subiri matusi toka kwa wana-ccm.

..nadhani Dr.Bashiru amedunga sindano ya kufyonza akili vijana wa ccm.
 
Asante sana kweli hii Timu ya Ubaguzi inafanya uchaguzi kuwa kama kamchezo ka watoto inaudhi sana. Bila nguvu ya umma mtaani hakuna mabadiliko.
 
Umeandika Mambo mazuri na ndo inavyotakiwa nasikitika tu mawazo mazuri kama haya kwa wenye mamlaka hawawezi kukubaliana na wewe. Nasikitika tu

Tanzania bado sana mh kikwete kidogo tu amalize matatizo haya kwa katiba mpya ila ndo ivyo ilivyokua

Mabadiliko ni mchakato, ipo siku maoni yangu yatafanyiwa kazi na serikali, bunge, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wengine kama vyama vya siasa, wagombea nakadhalika.
 
Hujawahi kuandika au kuposti mambo ya hovyo wewe....

Asante sana kwa andiko zuri uliloliandika kwa lugha fasaha, rahisi na yenye kueleweka...

Haingii akilini hata kidogo kumwengua ama kumnyang'anya mtu haki yake ya kuchaguliwa kuwa kiongozi eti kwa kukosea spellings za jina lake au kukosea kuandika tarehe tu...!!

Haya ni makosa ya kawaida yanayoweza kurekebishwa mbele ya msimamizi wa mchakato huo na actually ndiyo maana akaitwa "msimamizi wa uchaguzi".....

Maana yake ahakikishe kila mtu anakamilisha taratibu kwa ufasaha ikibidi kwa kumsaidia kwa kumwelekeza mahali asipoelewa...

Lakini wasimamizi wa sasa ni kama mbwa wa polisi tu wanaonusa na kutafuta makosa ya wagombea kwa makusudi ili wawaengue...
 
MAMBO 21 YA KUFANYIWA MAREKEBISHO YA KISHERIA KUHUSU MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA URAIS, UBUNGE NA UDIWANI.

"Good laws emanate from worst conducts of human beings".

Uchaguzi Mkuu ni mchakato (process) ambao una vijichakato (sub-processes) kadhaa ikiwemo kuandikisha wapiga kura, kutoa elimu kwa wapiga kura, uteuzi wa wagombea, kampeini za Uchaguzi, kupiga kura, kuhesabu kura, kujumlisha kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi. Kwa leo nitajikita katika kutoa mapendekezo ya kuboresha kijichakato kimoja tu ambacho ni Uteuzi wa Wagombea katika ngazi ya Tume ya Taifa ya uchaguzi na vijichakato vingine vya mchakato wa uchaguzi mkuu nitavifanyia kazi siku za usoni katika awamu kadhaa na tofauti.

Kutokana na matukio ambayo tumeshuhudia mpaka sasa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ngazi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mapendekezo yangu kuwa sheria za Uchaguzi zifanyiwe marekebisho kama ifuatavyo;

(1) Kwanza, Sheria iweke ukomo wa muda wa Tume ya Uchaguzi kufanya uamuzi wa rufaa za wagombea, kuwepo na time limit vinginevyo Tume ya Uchaguzi inaweza kufanya uamuzi wa rufaa baada uchaguzi mkuu kufanyika. Who knows?, tume ya Uchaguzi inaweza kufanya uamuzi wa rufaa za mwaka huu mwaka ujao mwezi August, 2021 na bila kuvunja sheria. Kwa mfano, wiki 1 ikihesabiwa tokea siku ya uteuzi iwe ni muda wa kuweka na kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi ya wagombea na wiki 2 tokea Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kufanyia uamuzi mapingamizi ya wagombea uwe ni muda wa kusikiliza na kufanyia uamuzi rufaa za wagombea.

(2) Pili, iwe ni marufuku kisheria kwa Kampeini za uchaguzi kuanza kabla ya Tume ya Uchaguzi kusikiliza na kuamua rufaa zote za wagombea kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi . Kampeini za uchaguzi zianze baada ya rufaa zote kuwa zimefanyiwa uamuzi ili wagombea wote wapate muda sawa na unaolingana kufanya Kampeini za uchaguzi na kuepuka kuvuruga Ratiba ya kampeini za uchaguzi (Cordinated Election Campaign Time Table). Sheria iweke marufuku uchaguzi kufanyika na kampeini za uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani kuanza kabla ya Tume ya Uchaguzi kusikiliza na kufanyia uamuzi rufaa za wagombea.

(3) Tatu, makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi ikome kuwa sababu ya kutengua uteuzi wa mgombea badala yake mgombea apewe muda wa kuzifanyia marekebisho fomu ya Uteuzi na fomu zingine za Uchaguzi.

(4) Nne, uteuzi wa mgombea Urais au ubunge utenguliwe tu kutokana na mgombea kukosa sifa za kugombea Urais au ubunge ambazo zimetajwa bayana au waziwazi na masharti ya Ibara ya 67 (1) na (2) na 39 (1) na (2) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano na sio kutokana na makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(5) Tano, sifa za mtu kugombea Udiwani ziwekwe kwenye Katiba na uteuzi wa mgombea udiwani utenguliwe tu kutokana na mgombea kukosa sifa za kugombea udiwani ambazo zimetajwa bayana au waziwazi na katiba na sio kutokana na makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(6) Sita, tuache huu utamaduni wa kuwa na siku moja ya kurudisha fomu na siku moja ya uteuzi wa wagombea wote ili kupunguza hatari (risky) ya wagombea kuvamiwa, kujeruhiwa na kutekwa kwa kwa lengo la kuharibu au kunyang'anywa fomu ya Uteuzi na mahasimu wake wa kisiasa na ili kutoa fursa kwa wagombea kukosoa makosa kwenye fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(7) Saba, tuwe na deadline tu ya kurudisha fomu za uteuzi na tuwe na na deadline tu ya uteuzi ili mgombea apate fursa ya kurudisha fomu ya uteuzi wakati wowote kabla ya deadline na ateuliwe wakati wowote kabla ya deadline. Hii itatoa fursa kwa mgombea kurekebisha makosa yake kwenye fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kabla ya deadline iwapo kuna makosa kwenye fomu hizo ambayo yamegundulika baada ya kurudisha fomu na pia hii itasidia kufanya watu wenye nia mbaya wanaotaka kumpokonya fomu ya Uteuzi mgombea kushindwa kujua muda ambao mgombea atarudisha fomu, hivyo, utaratibu huu utapunguza au kuondoa kabisa vitendo vya kuteka au kuvamia wagombea kwa lengo la kuharibu au kuwanyang'anya fomu za Uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(8) Nane, swala la mgombea kwenda kuchukua fomu ya Uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa Tume ya uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Saidizi wa Uchaguzi iwe ni hiyari (option) na isiwe lazima, hivyo, fomu zote za Uchaguzi ikiwemo Fomu za Uteuzi ziwekwe kwenye website ya Tume ya Uchaguzi na mgombea waruhusiwe kupakua (download) fomu hizo kwenye website ya tume ya Uchaguzi na kuzijaza na kuzirudisha kwenye Tume ya Uchaguzi bila kuwepo sharti la kuchukua fomu hizo kutoka kwa Tume ya uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi. Hii, itaondoa changamoto ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na Maafisa wengine wa Tume ya uchaguzi kukataa kwa nia mbaya kutoa fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa mgombea na watu wahalifu kuchukua fomu za mgombea halali aliyeteuliwa na chama cha siasa kwa nia mbaya ya kumzuhia asiteuliwe na tume ya uchaguzi au Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi.

(9) Tisa, wagombea wapewe fursa ya kurudisha fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa njia ya kielektroniki katika mfumo wa nakala laini (soft copy) kupitia njia za e-mail, fax nakadhali kwa masharti kwamba nakala halisi (original copy) za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwenye umbo la nakala ngumu (hard copy) zirudishwe kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ndani ya 7 baada siku ya mwisho (deadline) ya kurudisha fomu. Utaratibu huu unatumiwa na Chama cha Mawakili wa Tanganyika (Tanganyika Law Society) na unatambuliwa na Kanuni ya 17 ya Kanuni za Uchaguzi za Chama cha Mawakili wa Tanganyika, 2018 (Tangazo la Serikali Na 116 la 2018) yaani the Tanganyika Law Society (Elections) Regulations, 2018 . Pia, hata njia ya registered mail inaweza kutumika kupitia shirika la Posta. Utaratibu huu utandoa changamoto ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kujificha au kukataa kwa nia mbaya kupokea fomu siku ya mwisho (deadline) au siku zingine kabla ya siku mwisho ya kurudisha fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(10) Kumi, Sheria imtake kwa lazima kuwa mgombea anayeweka pingamizi lazima apeleke nakala ya mapingamizi kwa mgombea mwenzake anayemwekea pingamizi na kama ikishindwa kumpata mgombea basi kwenye ofisi za chama chake cha siasa za ngazi husika kabla ya kupeleka pingamizi hilo kwa Tume ya Uchaguzi au Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ili kuondoa changamoto ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kula njama na baadhi ya wagombea kwa kuwawekea wagombea wengine mapingamizi baada ya siku ya mwisho (deadline) ya kuweka mapingamizi kupita au kuwa time barred.

(11) Kumi na moja, Sheria ipige marufuku kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea yoyote kutokana na makosa ya kujaza fomu yaliyofanywa wa watu wengine wanaohusika na uchaguzi kama vile wadhamini (nominators), Afisa Viapo (Hakimu), maafisa na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwemo Wasimamizi na Wasimamizi wa Saidizi wa Uchaguzi na viongozi wa vyama vya Siasa kama vile Katibu wa Wilaya na Katibu Mkuu wa chama cha siasa.

(12) Kumi na mbili, Kamishna wa Viapo (Commissioner for Oaths) wote wakimemo Majaji, mahakimu mawakili wa kujitegemea na wanasheria wa serikali waruhusiwe kushuhudia kiapo na kuwaapisha wagombea Urais, Ubunge, na Udiwani katika mchakato wa kujaza fomu za uteuzi. Tuache utamaduni wa kuwatumia mahakimu na majaji pekee kama Kamishna wa Viapo katika wa kujaza fomu za uteuzi. Hii, itampa fursa mgombea kutumia Kamishna wa Viapo ambaye ana imani naye na ambaye anafikika kirahisi na mgombea (accessible) na kwa muda wowote.

(13) Kumi na tatu, wakati wa kufanya uamuzi kuhusu mapingamizi iwe ni marufuku kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi, Msimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea kwa msingi wa tuhuma za kosa la jinai ambazo ama bado hazijafanyiwa uamuzi na Mahakama au hakuna kesi yoyote iliyowahi kufunguliwa Mahakamani kuhusu tuhuma hizo. Sheria ipige marufuku kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea kutokana na tuhuma tu za kutenda kosa la jinai bila mgombea aliyepiga pingamizi kuambatanisha hukumu ya Mahakama ambayo ilimtia hatiani kwa kutenda kosa la jinai mgombea mwenzake ambaye amewekewa pingamizi.

(14) Kumi na Nne, tuache utamaduni wa kutoa haki ya kuweka mapingamizi kwa wagombea pekee na kuwanyima haki hiyo wapiga kura. Wapiga kura wote waruhusiwe kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani ili kuondoa hatari (risk) ya kumteka au kumyang'anya fomu ya Pingamizi mgombea ili asiweke mapingamizi dhidi ya mgombea mwingine.

(15) Kumi na tano, iwapo mgombea mmoja tu ndo ameteuliwa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Msimamizi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kugombea nafasi ya ubunge au Udiwani basi apigiwe kura za ndio na hapana, hivyo, utaratibu wa mtu kuwa mbunge bila kupigiwa kura na wananchi ukomeshwe. Na pia iwapo mgombea mmoja tu ndo ameteuliwa kugombea nafasi ya ubunge au Udiwani na Msimamizi au Msimamizi Msaidizi mtawalia basi sheria iruhusu kuwepo na mgombea kivuli wa ubunge au udiwani na mawakala vivuli ambao watalinda kura na maslahi ya wapiga kura ambao watapiga kura za hapana.

(16) Kumi na sita, mgombea wa nafasi ya Rais ambaye uteuzi wake umekataliwa au umetenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi apewe haki ya kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi katika Baraza la Migogoro ya Uchaguzi (Election Disputes Tribunal) ambalo litaundwa na watu 5 wenye sifa za kuwa majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa. Pia, mchakato wa uchaguzi wa Rais ikiwemo kampeini za uchaguzi lazima usimame mpaka Baraza la itakapotoa uamuzi wake. Pia, Wabunge na Madiwani ambao hawajaridhishwa na maamuzi ya Rufaa zao ambayo yamefanywa na tume ya taifa ya uchaguzi wapewe haki na fursa ya pili ya kukata rufaa kwenye Baraza la Migogoro ya Uchaguzi.

(17) Kumi na saba, mgombea wa chama cha siasa akijitoa kwenye uchaguzi basi chama cha siasa husika kipewe fursa ya kuteua mgombea mwingine kuziba pengo lililoachwa na mgombea ambaye amejitoa kwenye uchaguzi tofauti na sasa ambapo sheria inasema kuwa mgombea akijitoa ndo imetoka hiyo chama cha siasa hakiwezi kuteua mgombea mwingine ili kuondoa uwezekano wa Mgombea kuongwa au kutishwa ili ajitoe kwenye kushiriki uchaguzi.

(18) Kumi na nane, muda wa kukata Rufaa kwenda Tume ya Uchaguzi dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi uanze kuhesabiwa tokea siku ambayo mgombea amepata uamuzi wa maandishi wa kutengua uteuzi wake au kukataa pingamizi lake na sio tokea siku ya uamuzi kwa sababu mgombea akichelewa kupatiwa uamuzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi atajikuta nje ya muda wa kukata rufaa au akipewa uamuzi masaa machache kabla ya muda wa rufaa kuisha hatapata muda wa kutosha kuaandaa rufaa yake.

(19) Kumi na tisa, muda wa kukata Rufaa kwenda Tume ya Uchaguzi dhidi ya uamuzi wa Msimamizi na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi uongezwe kutoka siku moja walau mpaka siku 3 tokea mgombea alipota uamuzi wa kutengua uteuzi wake au kukataa pingamizi lake ili wagombea wapate muda wa kutosha kuandaa rufaa zao.

(20) Ishirini, liondolewe kwenye sheria sharti la mgombea udiwani kuwasilisha Hati kutoka kwa Afisa Usajiri wa Wapiga Kura wa Kata kudhibitisha wadhamini wa mgombea ni wapiga kura ambao wameandikishwa katika Daftari Wapiga Kura katika Kata husika. Msamimizi Msaadizi wa Uchaguzi ndo adhibitishe swala hili kwenye fomu ya Uteuzi.

(21) Ishirini na moja, wagombea wapewe haki ya kuwakilishwa na wanasheria katika mchakato mzima wa Uchaguzi hususani katika kuweka, kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi na kukata na kusikiliza rufaa ili kutenda haki kwa wagombea ambao sio wanasheria wakati wanapokabiliana na wagombea ambao ni wanasheria. Piga picha mgombea ambaye sio Mwanasheria akutane na mgombea ambaye ni mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi kwenye shauri la kusikiliza mapingamizi mbele ya Tume ya Uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi.

Imeandikwa na Matojo M. Cosatta.
Hayo yanahitaji ccm iondolewe madarakani kwanza, vinginevyo hayatekelezeki. Lakini unaiondoaje ccm bila kuwa na hayo? Kipi kilitangulia, kuku au yai?
 
..subiri matusi toka kwa wana-ccm.

..nadhani Dr.Bashiru amedunga sindano ya kufyonza akili vijana wa ccm.

Sitarajii kitu kama hicho unachosema kinaitwa matusi kutoka kwa wana CCM maana nimeandika kwa maslahi mapana ya taifa na bila kupendelea upande wowote na nimetumia lugha ya staha.
 
..ccm wanataka mambo yanayowafaidisha wao peke yao.

..hawataki mambo yanayowafaidisha wao, vyama mbadala, na watanzania ktk ujumla wetu.

..as long as wanaoathirika negatively na mapungufu ya sheria za uchaguzi ni wapinzani, basi usitegemee kupata ushirikiano toka kwa ccm kurekebisha hali hiyo.

..ccm watahakikisha hii hoja yake haipewi nafasi. na ukijitia kichwa ngumu they will fix you very badly.
 
MAMBO 21 YA KUFANYIWA MAREKEBISHO YA KISHERIA KUHUSU MCHAKATO WA UTEUZI WA WAGOMBEA URAIS, UBUNGE NA UDIWANI.

"Good laws emanate from worst conducts of human beings".

Uchaguzi Mkuu ni mchakato (process) ambao una vijichakato (sub-processes) kadhaa ikiwemo kuandikisha wapiga kura, kutoa elimu kwa wapiga kura, uteuzi wa wagombea, kampeini za Uchaguzi, kupiga kura, kuhesabu kura, kujumlisha kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi. Kwa leo nitajikita katika kutoa mapendekezo ya kuboresha kijichakato kimoja tu ambacho ni Uteuzi wa Wagombea katika ngazi ya Tume ya Taifa ya uchaguzi na vijichakato vingine vya mchakato wa uchaguzi mkuu nitavifanyia kazi siku za usoni katika awamu kadhaa na tofauti

Kutokana na matukio ambayo tumeshuhudia mpaka sasa katika mchakato wa uteuzi wa wagombea ngazi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ni mapendekezo yangu kuwa sheria za Uchaguzi zifanyiwe marekebisho kama ifuatavyo;

(1) Kwanza, Sheria iweke ukomo wa muda wa Tume ya Uchaguzi kufanya uamuzi wa rufaa za wagombea, kuwepo na time limit vinginevyo Tume ya Uchaguzi inaweza kufanya uamuzi wa rufaa baada uchaguzi mkuu kufanyika. Who knows?, tume ya Uchaguzi inaweza kufanya uamuzi wa rufaa za mwaka huu mwaka ujao mwezi August, 2021 na bila kuvunja sheria. Kwa mfano, wiki 1 ikihesabiwa tokea siku ya uteuzi iwe ni muda wa kuweka na kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi ya wagombea na wiki 2 tokea Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kufanyia uamuzi mapingamizi ya wagombea uwe ni muda wa kusikiliza na kufanyia uamuzi rufaa za wagombea.

(2) Pili, iwe ni marufuku kisheria kwa Kampeini za uchaguzi kuanza kabla ya Tume ya Uchaguzi kusikiliza na kuamua rufaa zote za wagombea kupinga maamuzi ya Wasimamizi wa Uchaguzi . Kampeini za uchaguzi zianze baada ya rufaa zote kuwa zimefanyiwa uamuzi ili wagombea wote wapate muda sawa na unaolingana kufanya Kampeini za uchaguzi na kuepuka kuvuruga Ratiba ya kampeini za uchaguzi (Cordinated Election Campaign Time Table). Sheria iweke marufuku uchaguzi kufanyika na kampeini za uchaguzi wa Rais, Mbunge na Diwani kuanza kabla ya Tume ya Uchaguzi kusikiliza na kufanyia uamuzi rufaa za wagombea

(3) Tatu, makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi ikome kuwa sababu ya kutengua uteuzi wa mgombea badala yake mgombea apewe muda wa kuzifanyia marekebisho fomu ya Uteuzi na fomu zingine za Uchaguzi.

(4) Nne, uteuzi wa mgombea Urais au ubunge utenguliwe tu kutokana na mgombea kukosa sifa za kugombea Urais au ubunge ambazo zimetajwa bayana au waziwazi na masharti ya Ibara ya 67 (1) na (2) na 39 (1) na (2) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano na sio kutokana na makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(5) Tano, sifa za mtu kugombea Udiwani ziwekwe kwenye Katiba na uteuzi wa mgombea udiwani utenguliwe tu kutokana na mgombea kukosa sifa za kugombea udiwani ambazo zimetajwa bayana au waziwazi na katiba na sio kutokana na makosa ya kujaza fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(6) Sita, tuache huu utamaduni wa kuwa na siku moja ya kurudisha fomu na siku moja ya uteuzi wa wagombea wote ili kupunguza hatari (risky) ya wagombea kuvamiwa, kujeruhiwa na kutekwa kwa kwa lengo la kuharibu au kunyang'anywa fomu ya Uteuzi na mahasimu wake wa kisiasa na ili kutoa fursa kwa wagombea kukosoa makosa kwenye fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(7) Saba, tuwe na deadline tu ya kurudisha fomu za uteuzi na tuwe na na deadline tu ya uteuzi ili mgombea apate fursa ya kurudisha fomu ya uteuzi wakati wowote kabla ya deadline na ateuliwe wakati wowote kabla ya deadline. Hii itatoa fursa kwa mgombea kurekebisha makosa yake kwenye fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kabla ya deadline iwapo kuna makosa kwenye fomu hizo ambayo yamegundulika baada ya kurudisha fomu na pia hii itasidia kufanya watu wenye nia mbaya wanaotaka kumpokonya fomu ya Uteuzi mgombea kushindwa kujua muda ambao mgombea atarudisha fomu, hivyo, utaratibu huu utapunguza au kuondoa kabisa vitendo vya kuteka au kuvamia wagombea kwa lengo la kuharibu au kuwanyang'anya fomu za Uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(8) Nane, swala la mgombea kwenda kuchukua fomu ya Uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa Tume ya uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Saidizi wa Uchaguzi iwe ni hiyari (option) na isiwe lazima, hivyo, fomu zote za Uchaguzi ikiwemo Fomu za Uteuzi ziwekwe kwenye website ya Tume ya Uchaguzi na mgombea waruhusiwe kupakua (download) fomu hizo kwenye website ya tume ya Uchaguzi na kuzijaza na kuzirudisha kwenye Tume ya Uchaguzi bila kuwepo sharti la kuchukua fomu hizo kutoka kwa Tume ya uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi. Hii, itaondoa changamoto ya Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na Maafisa wengine wa Tume ya uchaguzi kukataa kwa nia mbaya kutoa fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa mgombea na watu wahalifu kuchukua fomu za mgombea halali aliyeteuliwa na chama cha siasa kwa nia mbaya ya kumzuhia asiteuliwe na tume ya uchaguzi au Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi.

(9) Tisa, wagombea wapewe fursa ya kurudisha fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwa njia ya kielektroniki katika mfumo wa nakala laini (soft copy) kupitia njia za e-mail, fax nakadhali kwa masharti kwamba nakala halisi (original copy) za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi kwenye umbo la nakala ngumu (hard copy) zirudishwe kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ndani ya 7 baada siku ya mwisho (deadline) ya kurudisha fomu. Utaratibu huu unatumiwa na Chama cha Mawakili wa Tanganyika (Tanganyika Law Society) na unatambuliwa na Kanuni ya 17 ya Kanuni za Uchaguzi za Chama cha Mawakili wa Tanganyika, 2018 (Tangazo la Serikali Na 116 la 2018) yaani the Tanganyika Law Society (Elections) Regulations, 2018 . Pia, hata njia ya registered mail inaweza kutumika kupitia shirika la Posta. Utaratibu huu utandoa changamoto ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kujificha au kukataa kwa nia mbaya kupokea fomu siku ya mwisho (deadline) au siku zingine kabla ya siku mwisho ya kurudisha fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.

(10) Kumi, Sheria imtake kwa lazima kuwa mgombea anayeweka pingamizi lazima apeleke nakala ya mapingamizi kwa mgombea mwenzake anayemwekea pingamizi na kama ikishindwa kumpata mgombea basi kwenye ofisi za chama chake cha siasa za ngazi husika kabla ya kupeleka pingamizi hilo kwa Tume ya Uchaguzi au Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ili kuondoa changamoto ya Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kula njama na baadhi ya wagombea kwa kuwawekea wagombea wengine mapingamizi baada ya siku ya mwisho (deadline) ya kuweka mapingamizi kupita au kuwa time barred.

(11) Kumi na moja, Sheria ipige marufuku kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea yoyote kutokana na makosa ya kujaza fomu yaliyofanywa wa watu wengine wanaohusika na uchaguzi kama vile wadhamini (nominators), Afisa Viapo (Hakimu), maafisa na wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwemo Wasimamizi na Wasimamizi wa Saidizi wa Uchaguzi na viongozi wa vyama vya Siasa kama vile Katibu wa Wilaya na Katibu Mkuu wa chama cha siasa.

(12) Kumi na mbili, Kamishna wa Viapo (Commissioner for Oaths) wote wakimemo Majaji, mahakimu mawakili wa kujitegemea na wanasheria wa serikali waruhusiwe kushuhudia kiapo na kuwaapisha wagombea Urais, Ubunge, na Udiwani katika mchakato wa kujaza fomu za uteuzi. Tuache utamaduni wa kuwatumia mahakimu na majaji pekee kama Kamishna wa Viapo katika wa kujaza fomu za uteuzi. Hii, itampa fursa mgombea kutumia Kamishna wa Viapo ambaye ana imani naye na ambaye anafikika kirahisi na mgombea (accessible) na kwa muda wowote.

(13) Kumi na tatu, wakati wa kufanya uamuzi kuhusu mapingamizi iwe ni marufuku kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi, Msimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea kwa msingi wa tuhuma za kosa la jinai ambazo ama bado hazijafanyiwa uamuzi na Mahakama au hakuna kesi yoyote iliyowahi kufunguliwa Mahakamani kuhusu tuhuma hizo. Sheria ipige marufuku kwa Tume ya Taifa ya uchaguzi, Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kutengua uteuzi wa wagombea kutokana na tuhuma tu za kutenda kosa la jinai bila mgombea aliyepiga pingamizi kuambatanisha hukumu ya Mahakama ambayo ilimtia hatiani kwa kutenda kosa la jinai mgombea mwenzake ambaye amewekewa pingamizi.

(14) Kumi na Nne, tuache utamaduni wa kutoa haki ya kuweka mapingamizi kwa wagombea pekee na kuwanyima haki hiyo wapiga kura. Wapiga kura wote waruhusiwe kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea wa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani ili kuondoa hatari (risk) ya kumteka au kumyang'anya fomu ya Pingamizi mgombea ili asiweke mapingamizi dhidi ya mgombea mwingine.

(15) Kumi na tano, iwapo mgombea mmoja tu ndo ameteuliwa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Msimamizi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi kugombea nafasi ya ubunge au Udiwani basi apigiwe kura za ndio na hapana, hivyo, utaratibu wa mtu kuwa mbunge bila kupigiwa kura na wananchi ukomeshwe. Na pia iwapo mgombea mmoja tu ndo ameteuliwa kugombea nafasi ya ubunge au Udiwani na Msimamizi au Msimamizi Msaidizi mtawalia basi sheria iruhusu kuwepo na mgombea kivuli wa ubunge au udiwani na mawakala vivuli ambao watalinda kura na maslahi ya wapiga kura ambao watapiga kura za hapana.

(16) Kumi na sita, mgombea wa nafasi ya Rais ambaye uteuzi wake umekataliwa au umetenguliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi apewe haki ya kupinga uamuzi wa Tume ya Uchaguzi katika Baraza la Migogoro ya Uchaguzi (Election Disputes Tribunal) ambalo litaundwa na watu 5 wenye sifa za kuwa majaji wa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufaa. Pia, mchakato wa uchaguzi wa Rais ikiwemo kampeini za uchaguzi lazima usimame mpaka Baraza la itakapotoa uamuzi wake. Pia, Wabunge na Madiwani ambao hawajaridhishwa na maamuzi ya Rufaa zao ambayo yamefanywa na tume ya taifa ya uchaguzi wapewe haki na fursa ya pili ya kukata rufaa kwenye Baraza la Migogoro ya Uchaguzi.

(17) Kumi na saba, mgombea wa chama cha siasa akijitoa kwenye uchaguzi basi chama cha siasa husika kipewe fursa ya kuteua mgombea mwingine kuziba pengo lililoachwa na mgombea ambaye amejitoa kwenye uchaguzi tofauti na sasa ambapo sheria inasema kuwa mgombea akijitoa ndo imetoka hiyo chama cha siasa hakiwezi kuteua mgombea mwingine ili kuondoa uwezekano wa Mgombea kuongwa au kutishwa ili ajitoe kwenye kushiriki uchaguzi.

(18) Kumi na nane, muda wa kukata Rufaa kwenda Tume ya Uchaguzi dhidi ya uamuzi wa Msimamizi wa Uchaguzi uanze kuhesabiwa tokea siku ambayo mgombea amepata uamuzi wa maandishi wa kutengua uteuzi wake au kukataa pingamizi lake na sio tokea siku ya uamuzi kwa sababu mgombea akichelewa kupatiwa uamuzi kutoka kwa Msimamizi wa Uchaguzi atajikuta nje ya muda wa kukata rufaa au akipewa uamuzi masaa machache kabla ya muda wa rufaa kuisha hatapata muda wa kutosha kuaandaa rufaa yake.

(19) Kumi na tisa, muda wa kukata Rufaa kwenda Tume ya Uchaguzi dhidi ya uamuzi wa Msimamizi na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi uongezwe kutoka siku moja walau mpaka siku 3 tokea mgombea alipota uamuzi wa kutengua uteuzi wake au kukataa pingamizi lake ili wagombea wapate muda wa kutosha kuandaa rufaa zao.

(20) Ishirini, liondolewe kwenye sheria sharti la mgombea udiwani kuwasilisha Hati kutoka kwa Afisa Usajiri wa Wapiga Kura wa Kata kudhibitisha wadhamini wa mgombea ni wapiga kura ambao wameandikishwa katika Daftari Wapiga Kura katika Kata husika. Msamimizi Msaadizi wa Uchaguzi ndo adhibitishe swala hili kwenye fomu ya Uteuzi.

(21) Ishirini na moja, wagombea wapewe haki ya kuwakilishwa na wanasheria katika mchakato mzima wa Uchaguzi hususani katika kuweka, kusikiliza na kufanyia uamuzi mapingamizi na kukata na kusikiliza rufaa ili kutenda haki kwa wagombea ambao sio wanasheria wakati wanapokabiliana na wagombea ambao ni wanasheria. Piga picha mgombea ambaye sio Mwanasheria akutane na mgombea ambaye ni mwanasheria mbobezi wa sheria za uchaguzi kwenye shauri la kusikiliza mapingamizi mbele ya Tume ya Uchaguzi, Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaadizi wa Uchaguzi.

Imeandikwa na Matojo M. Cosatta.
Andiko bora kabisa la mwezi huu, hongera sana mkuu. Ushauri naomba ulipeleke Twitter, Facebook na kwingineko huko ili watanzania wengi waione. Natamani JF wangekuwa na utaratibu wa kutoa zawadi au nishani kwa maandiko bora kama haya....
 
22. Kuondolewa kwa ukomo wa kugombea Urais,
Nimechomekea tu, akimaliza 10 tumzawadie 10 mingine hata kama hataki, au sio ?
 
Mawazo yako yote ni mazuri sana kwa utawala wenye nia njema. NEC ya CCM na ya Kaijage wanayajua vizuri sana haya. Ila kwa sababu wanafanyakazi ya shetani, ni vigumu kukuelewa. Wakifuata ushauri wako, akina Majaliwa watapitaje bila kupingwa?
(6) Sita, tuache huu utamaduni wa kuwa na siku moja ya kurudisha fomu na siku moja ya uteuzi wa wagombea wote ili kupunguza hatari (risky) ya wagombea kuvamiwa, kujeruhiwa na kutekwa kwa kwa lengo la kuharibu au kunyang'anywa fomu ya Uteuzi na mahasimu wake wa kisiasa na ili kutoa fursa kwa wagombea kukosoa makosa kwenye fomu za uteuzi na fomu zingine za uchaguzi.
 
Andiko Bora kabisa la siku.

Tatizo ni kuwa kwa sasa nchi ipo chini ya mtu mmoja tu. Yeye ndio Alfa na Omega mwanzo na mwisho amejaa hila uonevu visasi na chuki.

Jiwe ni sikio la kufa ambalo halisikii dawa.

Jiwe + CCM = Burundi.
 
Mawazo yako yote ni mazuri sana kwa utawala wenye nia njema. NEC ya CCM na ya Kaijage wanayajua vizuri sana haya. Ila kwa sababu wanafanyakazi ya shetani, ni vigumu kukuelewa. Wakifuata ushauri wako, akina Majaliwa watapitaje bila kupingwa?
Ni imani yangu kuwa haya mawazo hiko siku yatafanyiwa kazi.
 
Mabadiliko ni mchakato, ipo siku maoni yangu yatafanyiwa kazi na serikali, bunge, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Wadau wengine kama vyama vya siasa, wagombea nakadhalika.
Mambo kama haya yanahitaji mchakato gani.Nikiasi cha maamuzi tu.Labda uwe mchakato wakuruhusu vichwa vyetu vifikirie sawasawa.Kwasababu ukiangalia yanayofanyika unajiuliza kama kweli tuna vichwa vinavyofikiri nakutenda sawasawa.
 
Back
Top Bottom