Mambo 18 yanayoweza kukufanya kuwa Strong

Mambo 18 yanayoweza kukufanya kuwa Strong

Ghost MVP

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2022
Posts
440
Reaction score
740
1. Hakuna wakati sahihi
Kulazimisha kufanya mambo vile unahisi ni sahihi kwa kigezo kuwa wakati sahihi utafika kutakufanya dhaifu na usiweze kuendelea kimaisha

2.Hatuwezi Ku-Control ou past
Kilicho pita Kimepita, Hatupaswi kuipa nafasi historia iliopita mana utajikuta unapoteza muda mwingi kwa kuhofia kupoteza muda, na kuwaza yaliopita kunaweza kukuzuia kuendelea kiakili na kimaisha.

3.Maneno yananguvu ya kuumiza
Maneno Makali, Ya kikatili Unayoweza ongea ukiwa kwenye hasira yanaweza kumuumiza mwingine na yakawa yakimtesa maishani, hivyo tumia maneno yako Kuwatia moyo, Kuwapooza.

4.Kushindwa Mapema Hukaa Moyoni
Kunapotusua Maisha huwa inakaa moyoni na tukishindwa hutuumiza na kukaa moyoni pia, hivyo tunapaswa kuwa naimani pale tunaposhindwa na kushukuru pale tunapo fanikiwa.

5.Mawazo Ya Namna ya kupa furaha
Tunapoteza muda mwingi kuwaza juu ya namna gani tutapata fura na hutupatia matokeo hasi ambayo yataishia kutuumiza pia, Unapaswa jikubali na kukubali kile unachoweza kupata hakika furaha utaipata kama utaamua kuiacha ije kwako.

6.Matumizi Ya Vifaa Ya Teknolojia Yaliopitiliza
Ukiwa na watu wape muda na umakini achana na kujipa ubize na simu yako au earphones zako au kuwa busy kutumia vifaa ulivyonavyo, ongea uso kwa uso, Kisha Endelea na Mambo yako baada ya kumalizana nao.

7.Tusihuku Mtu kwa Matendo Yake
Tunajiona sahihi kwa mawazo yetu na kuwaona wengine wabaya kwa matendo yao, Mafano unajiona upo sahihi Kulala mapema, na unachukizwa na wanaopiga kelele muda huo, bila kujua muda wako sio muda wa wengine, hivyo unapaswa kuelewa usawa kwa bila kumlaumu mtu kwa matendo yake.

8.Huzuni Ukikosa Pale Unapotoa
Usiwe na matarajio ya kulipwa wema pale unapotenda wema, sio kila mtu anaweza kutoa pale anapo pokea, tujifunzie kutoa kwa moyo bila tarajio la kulipwa kutokana na tulichotoa.

9.Hakuna unaemdai katika maisha
usianze kulaumu watu kwa kutokusaidia, kwasababu msaada sio lazima, anza shughulikia matatizo na maisha yako peke yako bila kutegemea watu wengine.

10.Wote Tutakufa
Watu husahau hili lakini tukae tukijua ipo siku utakufa, hivyo ishi maisha yako halisi ambayo hutajutia pale utakapofariki, na ishi kwa malengo sio kwa maigizo na ku-impress wengine, maisha feki huaribu future za wengi.

11.Zitambue Faida za kile unachohitaji katika maisha
Tunapaswa kukubali gharama za kupata kile tunachohitaji, na unapaswa kuwa tayari kufanya lolote sahihi na kutoa chochote sahihi ili kufanikisha lile unalohitaji.

12.Wajibika Kwa Matatizo Yako
Ukipata matatizo usikimbilie kwa wengine kupata attention yao, bali jitahidi kuwajibika kwa matatizo utakayokutana nayo bila kukwepa, ili kukusaidia kupunguza majukumu na kuongeza watu wanaojua matatizo yako zaidi ya wewe.

13.Usipotoshe na faraja
faraja isikuzuie kuwaza zaidi na kuwaza namna ya kupambana na kumove on, faraja kuna muda inaweza kukuponza na kukufikisha pabaya kama utaendelea kukumbatia mabaya yasiofaa kwa kujipa faraja kuwa yatafaa.

14.Mambo mazuri hayaji kiurahisi
Tunapaswa Kupambana juu ya kile tunachohitaji kwasababu mambo mazuri yanahita nguvu na jitihata ya kuyapata hivyo tujitoe kupambana ili kupata kile tunachohitaji.

15.Sio Kila Mtu Atakusaidia Kufikia ndoto zako
Kuna watu tunapaswawaondoa katika maisha yetu haijalishi nafasi zao mana hata ndugu anaweza asiwwe msaada na wewe na kama tunavyojua adui ni mtu wa karibu hivyo punguza watu wasio na msaada na wewe mana watakuja kuwa wabaya kwko, heri kuwa na watu wachache wanaokuamin na kukusaidia pale unapowahitaji ili kuweza kumove fast.

Till Next Time.
 
Back
Top Bottom