Unajua ni kwanini watu wengi wanakosa fuaraha katika maisha ?
Kuwa na furaha ya kweli sio mchakato wa hatua moja. Ni kubadilisha mfumo wa maisha ulio nao sasa, ni kutambua nini unapaswa kufanya na nni haupaswi.
Sio jambo rahisi ,lakini maramoja tu mchakato utakapoanza ,wewe mwenyewe utajiuliza kwanini usingeyafanya mabadiriko haya yote mapema .
Basi haya ni baadhi ya mambo ambayo ukiyazingatia katika maisha ,hakika utakuwa ni mtu mwenye furaha zaidi katika maisha yako.
1. Jihusishe mwenyewe kwenye maisha
Unatakiwa kuachana na vijitabia vya kitoto na kuangalia katika maisha yako zaidi Usijihusishe na vitu ambavyo havihusiani na maisha yako , badala yake unapaswa kuangalia maisha yako na namna ya kujikwamua katika maisha yako mwenyewe.
2.Epuka Kuwa na matarajio yasiyo na mantiki
Matarajio yasiyo na mantiki ni chanzo cha kukata tamaa katika maisha , unaweza kujikatisha tamaa kwa kuweka shinikizo kubwa katika jambo au hali fulani ambayo haina mantiki yoyote.
3.Kutulia
Unatakiwa kutulia katika mahusiano yakao ,kazi yako au urafiki. bila kutulia katika mahusiano, kazi yako huwezi kuwa na fuaraha hata siku moja.
4. Jifunze kusema hapana
Usiwe mtu wa kukubali kila kitu. Unatakiwa kufanya kitu unachopenda na kufurahia Jifunze kusema hapana pale unapotakiwa kufanya hivyo itakusaidia .Kusema hapana kutakufanya uwe huru zaidi. Hwezi kuwa na furaha hata siku moja endapo utakuwa mtu wa kukubaliana na vitu ambavyo viko nje ya uwezo wako.
5. Epuka Kufanya vitu kupita kiasi....
Fanya vitu kwa kiasi , kufanaya baadhi ya mambo kupindukia hufanya usiwe na furaha, mambo kama ulevi kupindukia, matumizi mabaya ya madawa,....
7. Achana na mambo yaliyopita
Sahau yaliyopita ,uanchotakiwa kufanya ni kauachana na yaliyopita na kuangalia yambele. Watu wengi huumia kwa kuendelea kushikilia yaliyopita ,ingawa baadhi ya mambo yaliyopita ni funzo katika maisha. Ukitaka kuwa na furaha unatakiwa kusahau yaliyopita na kuangalia yajayo.
8. Epuka Kuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye si sahihi kwako
Kwanini upoteze muda wako kuwa na mtu ambaye sio chaguo lako wakati unahitaji kuwa na furaha?
Watu wengi wanakosa fuaraha kwasababu wako kwenye mahusiano na watu ambao sio sahihi kwao ,kwakuwa hujiona wameridhika na maisha yanaenda hata kama hawafurahishwi. Furaha huletwa kwa kuwa na mtu sahihi katika mahusiano.
9. Epuka Kujikosoa sana
Kujitafakari mwenyewe ni chombo kikubwa sana katika maisha , lakini inakuwa tofauti pale unapojikosoa mno hadi unajishusha chini mwenyewe. Kutumia mda wako mwingi kujiona haufai na kujikosoa sana sio njia nzuri ya kujihamasisha .Tafakari vizuri ,fungua mawazo yako zingatia kujiboresha mwenyewe kuliko kujichukia.
10. Epuka kujitenga
Wakati mwingine Kutulia peke yako ukipata hewa nzuri ni vizuri zaidi lakini ni tofauti sana kuishi maisha ya kujitenga. Watu wenye furaha hupenda kujichanganya na watu wengine kwasababu wanaweza kujifunza mengi kupitia wenzao. Ni kweli kuna baadhi ya mambo ni vizuri kuyafanya mwenyewe lakini ni furaha zaidi kufanya vitu vingi ukiwa na watu wengine .
11. Usihukumu wengine
Kwanini unahukumu wengine? Hujui chochote kuhusu maisha ya watu wengine na ni mangapi wamepitia. Hebu waache watu waishi watakavyo na ishi maisha yako. Siku zote ukiwa ni mtu wa kufuatilia maisha ya watu huwezi kuwa na furaha hata siku moja.Angalia maisha yako utaishi kwa furaha daima.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo ukijaribu kuyafuatilia kiumakini na kuyazingatia basi kwa namna moja au nyingine utakuwa ni mtu mwenye furaha daima.