Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Mambo 10 ya kufahamu kutoka kwenye hotuba ya Jakaya Kikwete leo February 6 katika maadhimisho ya CCM
February 6 Chama Cha Mapinduzi CCM kilifanya maadhimisho ya miaka 39 ya chama hiko katika uwanja wa Namfua Singida, maadhimisho ya miaka 39 ya CCM yalihudhuriwa na viongozi na makada mbalimbali wa chama hicho, miongoni mwa watu waliohudhuria ni Rais wa awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli na Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Kikwete ambaye ni mwenyekiti wa chama hicho. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee mambo 10 ya kufahamu kutoka kwenye hotuba ya Jakaya Kikwete
1- “CCM ilihasisi na kuendelea kusimamia vyema mageuzi ya kisiasa kiuchumi na kijamii hapa nchini, kama sio uamuzi wa CCM vyama vingi visingekuwepo, ilikuwepo tume ya jaji Nyalali watanzania asilimia 85, walitaka mfumo wa chama kimoja uendeleee lakini kwa busara na hekima ya CCM tukaamua kuingiza mfumo wa vyama vingi” >>> Jakaya Kikwete
2- “Katika maadhimisho ya mwaka jana wakati ule nilikuwa na wasiwasi nilisema kuweni watulivu, chama kitawaletea wagombe wazuri wa nafasi zote, na nilisema hakuna litakalohariba chini ya uenyekiti wangu na chama hiki kikongwe, nilisema kwa kujidai nikiamini CCM ina utaratibu mzuri wa kuapta wagombea wake” >>> Jakaya Kikwete
3- “Kiukweli wapo waliofikiria kwa tutaharibikiwa wakati wa kuteua wagombea katika mkutano wa NEC, lakini niliingia pales sikuhamaki, mimi nilipoingia na kutulia kwenye kiti kuliwafanya watu wote wapate amani lakini kama ningehamaki mtihani ungekuwa mgumu ila nikasema tu haijapata kutokea” >>> Jakaya Kikwete
4- “Utabiri wa watu wengi kuwa CCM itagawanyika haukutokea tunajua wengine walihama chama na wengine walibaki ndani ya chama kama mamluki lakini utabiri wao haukutokea” >>> Jakaya Kikwete
5- “Wapo watu wanajaribu kujenga hoja kama CCM imeharibikiwa hawa hawajui hesabu, maana mtu hawezi kushinda kwa asilimia 73 viti ya viti halafu unasema CCM imeharibikiwa, wanabidi wawe wakweli tu kuwa wanasafari ndefu kuishinda CCM wana haraka” >>> Jakaya Kikwete
6- “Ndugu zangu naomba nieleze masikitiko yangu ya kutokamilika kwa uchaguzi Zanzibar, uamuzi wa tume ya uchaguzi Zanzibar kufuta uchaguzi na kutangaza kufanyika March 20, ni kinyume kabisa na matarajio yetu kwa sababu sisi tuliajiandaa kushangilia tunaona wana tuchelewesha kama CCM tungependa kutorudiwa kwa sababu uchaguzi ni jambo lenye usumbufu na gharama kubwa” Jakaya Kikwete
7- “Wakati wote hata kama mtu awe mkubwa kiasi gani na anapeswa asiachwe kuwa mubwa kuzidi chama siku zote chama kiwe kikubwa kuliko mtu au kiongozi yoyote, pamoja na kuibuka mambo mengi nawapongeza wote waliovunja makundi na kuungana licha ya kuwa kulikuwa na usaliti kwa baadhi ya wanachama lakini chama kiliibuka mshindi, siri kuu ni umoja” >>> Jakaya Kikwete
8- “Orodha ya mambo kutoka katika ilani ya chama Rais Magufuli ameanza kuyafanyia kazi, wengine wanashangaa mbona Magufuli kafanya hivi mwingine mbona kafanya vile, jamani anachofanya kipo katika ilani ya chama ni maagizo yetu, mimi huwa nawaambia kasome ilani ya chama lakini wapinzani wanasema anatekeleza ilani yao sasa mbona wanatoka bungeni” >>>Jakaya Kikwete
9- “Lakini tuepuke watu wenye mawazo hasi maarifa mafupi na wale wanaotaka uongozi wachama kama ngazi ya kupatia vyeo na kuendeleza maslahi binafsi na wakikosa vyeo basi hadha kubwa, halikadharika tuwanyapae watu ambao wakikosa vyeo wanahama vyama au wanasaliti” >>> Jakaya Kikwete
10 “Lazima tutambue jukumu la kukiwezesha chama kifedha ni jukumu letu kwa kulipa ada ya uanachama, lakini naomba tutambue uhai wa chama upo mashakani bila kuwa na fedha, masikitiko yangu kwa baadhi ya viongozi ndani ya chama kutotilia mkazo suala la chama kijitegemee lakini pia baadhi yao kuhujumu” >>> Jakaya Kikwete
Chanzo: Mambo 10 ya kufahamu kutoka kwenye hotuba ya Jakaya Kikwete leo February 6 katika maadhimisho ya CCM (+Audio) - TZA_MillardAyo