Mambele vs Jf

plan z

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2019
Posts
1,395
Reaction score
1,439
Hello, Naitwa Sandra, Nipo New York, nampenda mume wangu Sana, naweza kufanya chochote ili nimridhishe na kumfurahisha.. Lakini hivi karibuni, nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Tena mapenzi mazito.. Naombeni ushauri nifanyeje?

*WACHANGIAJI WA KIMAREKANI:*

*JAMES SILVER:* Nadhani unapaswa kuongea na mumeo, kwa sababu ndoa ni kushea kila jambo.

*SARAH WATER:* OH my dear, sorry.. Imewahi kunitokea hiyo hali na mie. Ilinilazimu nijifunge kibwebwe kuiepuka ili kulinda ndoa.

*GENIUS JR[emoji257]:* Ondosha fikra zako kwa huyo BINAMU wa mumeo.. Mfanye mumeo yale unayoyaona kwa huyo binamu yake..

*MADA HIYO HIYO KWENYE JAMII FORUM, BONGO INAKUWA HIVI:*
Hello, ( Jina siri yangu), Naishi Unga Limited, Arusha. Nimeolewa na Nina mtoto mmoja. Nimetokea kumpenda binamu wa mume wangu.. Nifanyeje, naombeni ushauri..

*WACHANGIAJI WA KIBONGO, MAJIBU YAO:*

* plan z*
Nawahi siti.

*EVARIST MASSAWE:* Huna akili mpumbavu wee. Tumbili mkubwa, nyau wa kike.. YAANI unataka uanze balaa kwa binamu wa mumeo?

*JOYCE MPIGAUZI:* Unatutia aibu na kutudhalilisha wanawake wenzako loooh
Na vile Unga Limited ilivyo ndogo, tutakujua tu.

*SELE MPEMBA:*
Hivi Simba wanakipiga lini na TP Mazembe?

*ANDENDEKISYE MWAKIFUGE:* Kama ukiona binamu wa mumeo anazingua, mie nipo available 0685108913 . Nipo Mwanjelwa.

*JONES RUTTA:*
Sio kosa lako. Ni kosa la wazazi wako.. Hawakutumia akili wakati wa kukuzaa.

*TZ SWAG:*
Wazee Nani Ana chaja ya smartphone? Simu yangu imeisha chaji.

*ANDREW THE DON:*
Wow.. Mtoto uko Bomba.. Ni add please..
*MTUMISHI:*

Wewe ni kahaba uliyeshindikana, unatakiwa Uokoke.. Njoo ufanyiwe maombi.

*MWAJEY MIKIDADI:* Pumbaaaaaf.

*DEVOTA JILANGILA:*
Napita tuuu.

*DULLA BOY:*
Mie huwa sichangiaji post za kijinga kama hii...

 
Si hatupo sirias katk jambo sirias ila tuankua sirias kwa jambo la mzaha
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…