mama zetu!!!

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,469
281
Nikiwa nimetulia pahala napata 'urithi wetu'...:A S-coffee:!! kaingia braza mmoja kapaki mkoko, akakaa meza ya jirani kaanza kuagiza kinywaji!! muda mfupi kaungana na kundi la watu watau akiwemo mama amabaye kwa kumuangalia aonekana kukaribia miaka ya sitini.. wakaendeleza kinywaji kama kawa!!

haukupita muda mrefu.. jamaa wa kwanza akaomba bili, akaletewa na mhudumu.. kaisoma na hakuridhika na hesabu aloandikiwa.. akamwambia mhudumu akaiangalie upya kabla hajamlia... KIMBEMBE kikaanzia kwa yule mama mtu mzima... aliporomosha maneno, kamchamba dada wa watu hadi unyayo, tukana meneja, kaponda glasi walizotumia za bia akidai za 'mchina'. wengine wote waliokuwa nae mezani kimyaaaaa... nyuso chini, sie wengine macho tumbwi eneo la tukio!!

Mawazoni likaja swali.. kama mama ni hivi... watoto wakoje? huo ugonvi ni kilevi, ndo tabia zake au ndo kutaka kuung'ang'ania ujana wakati umri ushakwenda!!...? sina jibu hadi sasa...

utafanyaje hali hyo ikikukuta, na mama anaeropoka ovyo ni mkweo... na mwanae ndo mwaelekea kuoana...?!WEEKEND NJEMA WAPENDWA!! :thumb:
 
Usikute mama mwenyewe "mama kijana" alikuwa na "vijana" wake huyo, sasa anataka kujionyesha naye "cool" and all.

Mambo kama haya unawaachia wenyewe tu, ukiya mind utakuwa hulali.
 
Back
Top Bottom