TANZIA Mama yake Hayati John Pombe Magufuli (Rais wa Awamu ya 5 wa JMT) afariki Dunia

TANZIA Mama yake Hayati John Pombe Magufuli (Rais wa Awamu ya 5 wa JMT) afariki Dunia

Inside10

Platinum Member
Joined
May 20, 2011
Posts
34,738
Reaction score
42,829
Mama Mzazi wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati John Pombe Magufuli, Suzana Magufuli amefariki dunia leo Mei 25, 2026, Chato Mkoani Geita baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akizungumza na AyoTV kwa njia ya simu, Mtoto wa Hayati Magufuli, Jesca Magufuli amethibitisha kutokea kwa msiba huo akieleza kuwa Bibi Suzana amefariki saa 1 usiku Nyumbani kwake Chato.

“Bibi yetu (Suzana Mussa) amefariki saa moja nyumbani kwake Chato baada ya kuugua kwa muda mrefu, taratibu za msiba familia itawajulisha, Bwana ametoa na Bwana ametwaa” Jesca.

Screenshot 2026-05-25 222526.png

 
Back
Top Bottom