mama wa kambo ni mama lakini!?!!!!

Kwa kweli huyu mama anatakiwa apewe adhabu huko jela ya kuwanyonya wanawake woe atakaofungwa nao gereza moja, lol kwa genye gani hizo yaani sijui uso wake anauweka wapi saa hizi mtoto huyo atakuwa kavimba tumbo kabisa
 
Mungu wangu, yaani nasikia hadi kichwa kinaniuma! kweli ushetani gani huo jamani? inamaana hatosheki kwa mumewe, na hata kama hatosheki, huyo mtoto anamkomoa au ni ushirikina? Hebu apelekwe kwenye vyombo vya vyeria huyo ili sheria icukue mkondo wake, na alaaniwe milele!!!!!!!!!!!
 
huyo mwanaume kama ana habari mambo anayofanya mkewe (mama wa kambo) itabidi afanye taratibu za kumkeketa! si jambo la busara hata kidogo kufanyia mambo hayo mtoto mdogo!
 
Ni kweli kuna wa mama wanalea vizuri kuliko hata mama wazazi, wengine kama mama mzazi, wapo na wanolea kwa vile sio wake. Hivyo tuwape moyo mama wa kambo ili watulelee wana wetu angalau kaka mama mzazi. Hongereni sana wa mama mnaolea kama au zaidi ya mama mzazi, baraka zipo mbinguni na zinaanzia hapa duniani, hao wabaya adhabu zinaanzia hapahapa duniani, mmoja ni huyo
 
yaani umenitukana vibaya sana sana....mbona mnachuulia mambo kihivyo jamani, sio wote tupo hivyo, wengine tunawalea hao watoto kama wa kuwazaa vile, inategeemana na ubinadamu wa mtu jamani.

Take it easy mamy, unajua tatizo lililopo ni mara nyingi mabaya ya watu ndo huenezwa. Na ukizingatia mama wa kambo asilimia kubwa ni wakatili sana.
Huyo mama ni kesi tofauti kabisa, ushetani wake umevuka mipaka. Hopeful sababu imetoka TGNP watachukua hatua stahiki kama kuna ushahidi wa kutosha.

My take: Tuwaombee sana akina mama maana wanakuwa easly attacked by satan na kutokana na kuwa na moyo mwepesi wa kuelewa anawatransform vile yeye anataka, ndo maana mwanamke jambazi anakuwa mbaya kuliko maelezo.
 
Kuna watu wengineUtadhani walitapikwa na si kuzaliwa..Hata wanyama pori wana akili kuliko wao.Itakiwa vema kama akipelekwa kizimbani..
yaaaaaaaaani some people are living b'coz it is illegal to kill them!
 
Kusema ukweli mama wa kambo wengi ni wakatili kwa watoto wa waume zao. Na ndio maana ikitokea ukakuta mama wa kambo anaelea watoto kwa upendo basi utasikia jamii inashangaa "anawalea watoto kama wakwake mwenyewe" kwa kuwa ni exception. Tunakubali kuwa wapo wamama wenye roho nzuri ila ni wachache.

Kuna case nyingi sana za ukatili wa watoto ambazo nyingi tunazijua baada ya majirani kuchoka na kuamua kuingilia private lives za watu na kuwaanika kwenye vyombo vya habari.

My take: Wamama tujitahidi tunapoachika kwa wame zetu kulea watoto mpaka wafikie umri wa kujitambua ndio tuwarudishe ka baba zao. Na hao TGNP inabidi wapambane sheria ya talaka iruhusu mama kuwa na haki ya kukaa na mtoto kama nchi za wenzetu walau kwa kubadilishana kwa zamu. Nashangaa idadi ya wanawake bungeni inaongezeka lakini hatuoni inatusaidia vipi sisi kina mama. Au wameingia bungeni kuondoa umasikini wao binafsi na familia zao. Sheria zinanyanyasa sana kina mama.
 
Back
Top Bottom