GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,212
Nilisikitika sana nilipokusikia jana ukiwa kama Mgeni rasmi pale uwanja wa Uhuru ( Shamba la Bibi ) katika maazimisho ya Sherehe za May Day uliposikika ukisema tena bila hata ya ' chembe ' ya ' aibu ' kuwa ungependa wale wote waliotajwa katika Kikosi cha 9,932 ( wagushi Vyeti waliotukuka Serikalini ) na ambao wameitumikia nchi kwa miaka 30+ basi ' wafikiriwe ' na kama vipi ' wasamehewe ' ili walipwe viinua mgongo vyao.
Sikuwahi kutegemea kama Mama ambaye nilikuwa ' nakuheshimu ' wakati unajua kabisa kuwa hao Watu ndiyo wameliingizia Taifa hili ' hasara ' kubwa na pengine hadi kutusababishia leo kuwa wadaiwa ' Sugu ' Kimataifa na nchi kuwa bado nyuma Kimaendeleo hivi leo ( jana ) ungesimama pale uwanjani na kuwatetea.
Ile ' Kauli ' yako ya jana imenifanya niwaze kufikiria yafuatayo kuwa labda:
Rais Magufuli ' tunyooshe ' tu Baba mpaka tuheshimiane mjini hapa!

- Nawe uliwahi kuufanya huo mchezo.
- Umeguswa kwa namna moja au nyingine Kifamilia au hata Kiukoo.
- Unatetea hii tabia mbaya ambayo pia ni kinyume na Sheria za nchi.
- Huna huruma na Watanzania wenye Sifa stahili wapate Ajira kihalali.
- Kuna Siri kubwa unayoijua juu ya hii tabia ambayo inasemekana ni ya muda mrefu.
- Umetumwa ' kiaina ' kuwasemea hao ' walioidanganya ' nchi kwa muda mrefu.
- Unatafuta tu ' turufu ' yako ya Kisiasa kwa faida zako unazozijua Wewe.
Rais Magufuli ' tunyooshe ' tu Baba mpaka tuheshimiane mjini hapa!