Mama sitakusahau

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Maneni haya aliyasema Stella alimtamkia mama yake. Stella alizaliwa kijijini huko Kaliua, alikuwa msichana mwenye sura ya kawaida lakini mwenye akili sana darasani. Alimudu vizuri hesabu na masomo ya sayansi.

Stella alilelewa katika misingi ya dini. Akiwa kidato cha sita alipata boy friend, waliahidiana wataoana. Stella alifanya tendo la ndoa blew mara ya kwanza na kijana yule.

Baada ya mitihani ya six form, Stellea alijikuta ana mimba. Marafiki walimshauri
aitoe mimba ile alikataa kwani alifahamu dini inakataza kuua uhai.

Stella alifaulu vizuri mitihani hivyo haikuwa shida hata alivyoairisha mwaka wa masomo Muhimbili. Stella alijifungua salama mtoto wa kiume. Stella kuwa na mimba boyfriend aliiona ni mzigo hivyo alizima mawasiliano.

Mama yake Stella alimlea mtoto wakati Stella akiwa Muhimbili masomoni. Baada ya kumaliza shule, Stella alipata ajira, alimchukua mwanae wakati huo akiwa darasa la kwanza.

Stella alikwenda Australia kusomea shahada ya uzamili. Mama na mtoto walibaki nyumbani kwa Stella na baba kutoka Kaliua aliwatembelea. Stella alimaliza shule na kurudi nyumbani.

Asante aliyoipanga kumpa mama yake kwanza ilikuwa holiday kwenye hoteli vya nyota tano wao wawili kwa wiki moja. Dada wa kazi alibaki na mtoto.

Mama alishindwa kushika umma na kisu wakati wa kula. Pia vyakula mama hakuwa amevizoea. Stella alinnunua hot pots na kuhakikisha ananunua vyakula mtaani anamletea mama yake chumbani na kumwambia mama haya ni maisha yanupande wa pili na wewe yaonje.
 
Kama Bongo Movie, nilitaraji kuona reputation na kijana mtia mimba nilitaka kujua changamoto za malezi na ni namna gani alipata ufadhili so far...by the way uhusika wa babake stella ni kutembelea tu means Stella alimthamini zaidi mama...kweli wanaume tutafute hela watoto ni wa mama!
 
Na aisome Edward Lowasa kwa kutelekeza mtoto wake wa damu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…